Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

KATIBA YA KIKUNDI CHA KIKOBA SUNBANK LADIES

1:Jina la kikundi ni SUNBANK LADIES


Viongozi :zuhura bakari -mwenyekiti
-asnath mchangila -katibu
-shadya ndemeke -mweka hazina
-lilian rwegamba -nidhamu

2:Madhumuni ya kikundi
-kila mwanachama atapaswa kununua hisa kila mwezi,walau hisa 3 na jamii 1
-kila mwanachama atapaswa kuweka 50,000 kama ada ya kiingilio ,na 200,000 kwa wageni
itayolipwa ndan ya miezi 4
-kuelimishana na kuchukua hatua mbalimbali za kuinuana kiuchumi
-kutetea maslahi ya wanachama dhidi ya yoyote anaetaka kukwamisha maendeleo ya kikundi

3:MAMLAKA YA KIKUNDI
-kuwekeza,kukopesha wanachama ,kuadhibu wanachama na kudhibiti ulipaji wa mikopo kwa
mwanachama asielipa kwa wakati

4:UANACHAMA
-Sifa za mwanachama
(a) Awe mfanyakazi /muajiriwa wa sunbank
(b) Awe mwenye tabia njema na akili timamu
(c) Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli za kikundi
(d) Awe.tayari kufata masharti na kanuni za kikundi

5:HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA


-Wajibu wa mwanachama
(a) kulipa michango yote ya kikundi ikiwa hisa na jamii
(b) kulipa mkopo katika muda uliopangwa kulingana na kanuni na taratibu za kikundi
(c) kulipa mkopo alioudhamini iwapo mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake
(d) kushiriki shughuli za kikundi kwa kufuata masharti yake
(e) kutii na kutekeleza matakwa ya katiba hii

-Haki za mwanachama
(a) kutoa maoni/kero/dukuduku katika mikutano na kwenye group kwa kufata taratibu
(b) kusaidiwa na kikundi anapopata tatizo
(c) kuwa mdhamini wa mikopo kwa mwanachama mwengine
(d) Kukopa kwenye kikundi kwa kufuata kanuni

6:UKOMO WA UANACHAMA
(a) KIFO
-Endapo mwanachama atafariki hisa zake atapatiwa mrithi/warithi wake watapokea 100% na
faida ya mwanachama kama ipo baada ya makato ya malimbikizo ya madeni kama alikopa
-mrithi/warithi hatarudishiwa jamii wala kiingilio
-mwanachama ataondolewa kwenye uanachama pale tu taarifa ya kiifo takapopokelewa na
kuthibitishwa
(b) KUWA NA UGONJWA WA AKILI
(c) KUJIONDOA KWA HIARI
-mwanachama atakatwa 50% ya hisa zake na 50% atapatiwa pale kikoba kitakapovunjwa
-mwanachama hatorudishiwa faini
6:MICHANGO
Michango itakayotolewa na kikundi
(a) MSIBA
-wazazi,mume,mtoto
(b) UZAZI
-Kila tukio mwanachama atapewa ,300,000 na kikundi
Nb:mchango huu utapokea kwenye tukio 1 tu kwa msimu wa kikoba
-Asha,beatrice ,shadya wamepewa ruhusa ya kuchangiwa kwenye sherehe 1 tu inayohusu mtoto
endapo itatokea

7:MIKOPO
-mkopo ni mara 3 ya hisa zako
-riba ni 10%
(a) Aina za mikopo
(i) Mkopo mdogo wa dharura ni sh 100-300,000
-muda wa marejesho ni mwezi 1(inatoka jamii)

(III) Mkopo mkubwa wa maendeleo


(a)500,000-1,000,000…..miezi 6
(b)1,100,000-1,500,000…….miezi 9
(c)1,600,000-2,100,000……,miez 12
(d)2,200,000-3,000,000…….miez 18
(e)3,100,000-5,000,000……miez 24

IV) kila mwanachama anatakiwa kuingiza faida ya mikopo ,mwanachama ambae hatokua tayari
kukopa ataingiza faida ya sh 100,000
V) Sifa za kupata mkopo uwe umemaliza kiingilio na uwe na mdhamin 1 ,kwa mkopo wa zaidi ya
milion 3 wadhamin 2
VI) Mgawanyo wa faida 50% itaenda kwa mhusika na 50% itagaiwa kwa wanachama wote

8:MAKOSA YATAKAYOTOZWA FAIN


- kutohudhuria kwenye kikao,kuchelewa kwenye kikao na kuondoka kwenye kikao hakijaisha fain
ni sh 30,000
-lugha za kejeli ,lugha za uchochezi,kwenda nje ya makubaliano na kikundi ni sh 30,000
-kotoa siri za kikundi ni sh 50,0000
Nb:Udhuru wa kutohudhuria kwenyee kikundi utapokelewa na mwenyekiti ,ukiwa na
viambatanisho vya uthibitisho
-faini ya kuchelewa kwenye kikao na kutohudhuria kwenye kikao itatumika ku support kikao

9:kikao kitafanyika kila baada ya miezi 3

10:Kazi za viongozi
a) MWENYEKITI
-kusimamia na kuitisha vikao vyote vya kikundi
-kutoa taarifa ya mwanachama ya furaha au huzuni
-kusimamia utatuzi wa migogoro yote ya kikundi
b) KATIBU
-kutunza kumbukumbu zote za kikundi
-kuandika muhtasari wa vikao vya kikundi
-kuhamasisha ununuzi wa hisa na jamii pamoja na marejesho ya mikopo

c) MTUNZA HAZINA
-kutumza fedha za kikundi
-kutunza hesaba na kufatilia marejesho

d) NIDHAMU
-kusimamia maswala yote ya nidhamu na maadiili ya wanachama katika kikundi

11)MICHANGO YA KIKUNDI
- Hisa 1 ni sh elf 10,000 kiwango cha chini kununua hisa ni sh 30,000
-jamii 1 ni sh 10,000
-mwsho wa kuchanga ni tarehe 5
-faini ya kuchelewa kununua hisa ni sh 10,000 na faini ya kuchelewa jamii ni sh 10,000

12:katiba hii itabadilishwa au kuongezewa kutokana na makubaliano ya wanakikundi

You might also like