Form ya mkopo

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 60

USIMZIMISHE

ROHO
MTAKATIFU
YALIYOMO

YALIYOMO ………………………………………………………………….3

TABARUKU. ……………………………………………………………………………………4

LENGO LA KITABU……………………………………………………………………………5

NINI MAANA YA KUMZIMISHA ROHO MTAKATIFU?..………………………6

DALILI ZA ROHO MTAKATIFU……………………….…………………………………11

MATOKEO YA KUTOKUZIZIMISHA DALILI …………………………………..56

KUHUSU MWANDISHI ……………………………………………………………………..59


TABARUKU
NI SHAUKU YA MOYO WANGU KUKISAIDIA KIZAZI
CHANGU KWA HABARI YA UFALME WA MUNGU NA
KUWEKA NJAA NA KIU YA KUMJUA MUNGU PIA
KUINUA WATU WALIO TAYARI KWA AJILI YA
MUNGU AMBAO HAWAJAJIKINAI YAANI ASKARI
WAAMINIFU HIVYO NI MATUMAINI YANGU KUPITIA
MAARIFA HAYA KUNA JESHI KUBWA LITAINUKA NA
KUFANYA KANISA KUTAWALA NA KUMILIKI KATIKA
TAIFA NA MATAIFA KUPITIA VITABU HIVI VYA KI-
ELECTRONIKI AMBAVYO NI BURE KABISA KWA KILA
ATAKAYE.

TANZANIA, WEWE NI JIKO LA KUPIKIA MAISHA


HALISI YA WOKOVU.
Lengo la kitabu hiki ni

Kumfanya kila mkristo aweze kujisimamia


mwenyewe na aweze kuwa na matokeo kama
yaliyokusudiwa na Mungu Juu ya maisha yake
pasipo makosa yoyote kwenye maisha yake na
kumfanya awe mshindi dhidi ya mipango na hila za
shetani

Kati ya mbinu kubwa ambayo shetani anaitumia


kuharibu Kizazi hiki ni ukosefu wa maarifa sahihi
kuhusu dalili za Roho Mtakatifu kama njia ya
maongozi.
SURA YA KWANZA
NINI MAANA YA KUMZIMISHA ROHO MTAKATIFU?
Ni kumzuia Roho Mtakatifu au kusitisha utaratibu
wa Roho Mtakatifu kwa kufahamu au
kutokufahamu.
Kizazi chetu kimekua muhanga wa habari nyingi
mnoo za kuhusu MUNGU hasa ni ROHO MTAKATIFU
ni atajwi sana makanisani wala watu hawana habari
kujua sana habari zake hivyo ni Kizazi
kinachomuhubiri Roho Mtakatifu wasiyemjua hivyo
makosa ni mengi Sana katika kizazi hiki hivyo
tunamzimisha sana Roho Mtakatifu

1 wathesalonike 5:19
Msimzimishe Roho;

Hesabu 11:26-29
[26]Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la
mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa
Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa
miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa
hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri
kambini.
[27]Mtu mmoja kijana akapiga mbio, akaenda
akamwambia Musa, akasema, Eldadi na Medadi
wanatoa unabii kambini.
[28]Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa
tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana
wangu Musa, uwakataze.
[29]Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa
ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa
BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA
angewatia roho yake.

Musa anaonesha kukasirishwa na kitendo cha vijana


wake kutaka kuwazuia wale wazee wasitabiri Musa
anawajibu waacheni maana alielewa kuwazuia
wazee wasitabiri ni kumzimisha Roho Mtakatifu na
Musa alikua anaona bora wote wangekua
wanatabiri yaani hawamzimishi Roho Mtakatifu
kama wale vijana, vivyo hivyo kwa sababu sisi ni
wachanga kwenye mambo ya kiroho basi tunamzuia
sana Roho Mtakatifu.

Unaweza kumzimisha Roho Mtakatifu kwa kujua au


kutokujua sasa leo natakami tuangalie vitu au dalili
za Roho Mtakatifu katika Maisha yetu ambavyo
inatupasa kuepuka kuvizuia maana tukivizuia huwa
tunamzimisha Roho Mtakatifu.

1 Samuel 19:23-24
[23]Basi akaenda Nayothi huko Rama, na roho ya
Mungu ikamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku
anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama.
[24]Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya
Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha
siku ile. Kwa hiyo watu husema, Je! Sauli pia yumo
miongoni mwa manabii?
Ukisoma kwenye Hili andiko utaona jinsi sauli
alivyofurikiwa na Roho Mtakatifu kuanzia mbali
kabisa, hii inaonesha hakuzuiliwa wala hakukatizwa
mpaka Roho Mtakatifu alipomaliza Kazi yake ndani
yake na hivi ndivyo tunavyotakiwa kumpa nafasi
huyu MUNGU Roho Mtakatifu bila kuwaza Kuwa
Muda umeenda au nipo ofisini au wataniona ni wa
kiroho sana au watu watanifikiria mimi sina
utaratibu au sio mstaarabu.

Ufahamu huu ungekua juu yetu unafikiri ni kwa


kiwango gani tungeona vitu vingi vya kiroho katika
Maisha Yetu
Watu wengi kwa kukosa kuzijua dalili au utaratibu
wa Roho Mtakatifu katika Maisha yetu.

1 wakorintho 2:4-5
[4]Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa
kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za
watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
[5]Ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu,
bali katika nguvu za Mungu. Hekima ya Kweli ya
Mungu
SURA YA PILI
DALILI ZA ROHO MTAKATIFU
1)Kunena kwa Lugha
Marko 16:17
[17]Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa
jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya;

Hii ni hali ambayo Mungu huitumia kwa kiwango


kikubwa Ili kutujenga na kutuokoka na hatari
tunazokutana nazo katika Maisha

Mfano;
Mwaka 2018 nikiwa kidato cha sita na nakaribia
kufanya mitihani ya Taifa nilienda DIT kwa rafiki
yangu Deo kumtembelea hivyo nililala hapo sasa
asubuhi yake nilipoamka nilisikia msukumo wa
ajabu wa kunena kwa Lugha hivyo nikaruhusu ile
hali yaani nikawa nanena kwa lugha tangu
nilivyoamka mpaka nikiwa naeleka Shuleni Tambaza
na nilivyofika maeneo ya pale faya mjini nikiwa
nataka kuvuka barabara gari ikasimama na dereva
akanionesha ishara ya kuniruhusu nipite na nikiwa
napita akatoa gari na kunigonga huku nikiwa
nanena kwa lugha unajua nini kilitokea sikuumia
wala kuchubuka na huku naendelea kunena kwa
lugha kwa sauti ya chini chini lakini nikiwa
nimemaanisha, Sikia shetani alipanga nipate ajali
lakini MUNGU akaepusha mauti Kupitia kunena kwa
lugha ndio maana Biblia inasema huwa tunaponena
ni Roho Mtakatifu akiwaombea watakatifu kwa
kuugua haleluya na mimi na wewe ni mmojawapo
wa watakatifu hivyo inaonesha kuwa tunaponena
kwa lugha tunatengeneza ulinzi kwa ajili yetu na
familia zetu.

Warumi 8:26
[26]Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,
kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa.

Mfano.
Nilikua nyumbani nafua mwaka 2018 baada ya
kumaliza kidato cha sita lakini nikasikia kunena kwa
lugha kwa msukumo wa ajabu sana na mimi
nikisikiaga hii hata nikiwa chooni huwa ninanena tu
kwa lugha hivyo nikaruhusu ile hali ya kunena kwa
lugha baada ya kumaliza kufua nikaenda kufunua
ndoo ya Maji ilikua imekaa vibaya yaani imegeuzwa
juu chini ile kuiinua tu nikamkuta nyoka akiwa
amejipanga kung’ata tayari nikakimbia kwa mstuko
mkubwa lakini baada ya Muda nikarudi nikamkuta
yule nyoka kama ameganda vilevile hivyo nikampiga
na jembe kisha nikamchoma moto sikia Roho
Mtakatifu alileta msukumo huu kwa sababu
Kikawaida nisingeweza kujua kilichopangwa na adui
lakini yeye anajua dakika kumi zijazo shetani alikua
amepanga nini hivyo akaleta hii hali ndio maana
Biblia inasema huwa tunanena mambo ya sirini na
Mungu wetu, haleluya Mungu ashukuriwe kwa
zawadi hii ya kunena kwa lugha.

1 Wakorintho 14:2
Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu,
bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye;
lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Kunena kwa lugha sio kwa watu fulani maalumu tu


bali ni kwa ajili ya kila mmoja wetu

Matendo ya mitume 2:37-39


[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao,
wakamwambia Petro na mitume wengine,
Tutendeje, ndugu zetu?
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila
mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la
dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho
Mtakatifu.
[39]Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa
watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na
kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu
wamjie.

Inawezekana na wewe roho Yako imechomwa


ilivyosikia haya maneno ila unaweza ukajaa Roho
Mtakatifu ikiwa kama utaokoka na kumwambia
Roho Mtakatifu nijaze.

Kuna aina katika kunena kwa lugha.


1.Lugha ya ujumbe
(Kusema kwa lugha nyingine)
Matendo ya mitume 2:4
[4]Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka.
Hapa mtu anaweza kunena kichina, kifaransa,lugha
yoyote hata kama haijui lakini ni ajili ya ujumbe tu
na baada ya hapo ile lugha Huwa hauifahamu tena

2.Lugha ya binafsi.
• Kuongea na Mungu

• Kujijenga kibinafsi
1 Wakorintho 14:4
[4]Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali
ahutubuye hulijenga kanisa.
• Kupambana na hila za adui.

3.Lugha za malaika.
1 Wakorintho 13:1
[1]Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za
malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo
na upatu uvumao.
Waebrania 1:7,14
[7]Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye
malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa
miali ya moto.
[14]Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa
kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Kuna mifumo katika kunena kwa lugha


Kuna kunena kwa lugha kwa ushirika na Mungu
hapa ndo unanena kistaarabu au kwa kulia machozi
kabisa hii ni mfumo wa unenaji wa lugha wa
kiushirika au kutubu.

1 Wakorintho 14:2
[2]Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu,
bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye;
lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
Kuna kunena kwa lugha kwa kupeleka maombi
mbinguni hii ni wewe na Roho Mtakatifu tu

Warumi 8:26
[26]Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,
kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa.

Ni Roho Mtakatifu ndiye akusaidiaye kuomba hapa


Yaani hukupa maneno ya kupeleka hoja zako kwa
YESU wetu.

Kuna kunena kwa lugha kule kunakotokana na


kujibiwa kwa maombi yako yaani unapewa ufunguo
wa kufungua mambo yako ndo hii isaya anaitaja
lakini hii ukisoma biblia ya kiingereza ndo utaipata
hii vizuri
Isaya 28:11
[11]La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa
lugha nyingine atasema na watu hawa;

Kwa kiswahili haijakaa vizuri kwa sababu lugha yetu


haijakua vya kutosha ila kiingereza kinatupa Neno
zuri la “Stammering” kama ifuatavyo

[11]For with stammering lips and another tongue


will he speak to this people.

Stammering kwa kiswahili ni kigugumizi.

Maana ya kigugumizi
Kigugumizi (kutoka kitenzi “kugugumia”, kwa
Kiingereza: “stuttering” au “stammering” ni shida ya
baadhi ya watu katika kusema:
Mhusika anajua la kusema, lakini maneno
yanamtoka tofauti, kwa mfano kuna:
• marudio ya fonimu, sehemu
ya maneno au sentensi
• mkwamo kabla ya maneno fulanifulani
• urefushaji wa sauti (hhhhhhhhhham badala
ya ham)
• kusimama
• kusema kitu tofauti na kilichokusudiwa
• kusita au kuhangaika ili kusema kitu

Maana ya stammering lips ni midomo ya kigugumizi


yaani ile hali ya kurudiarudia maneno kushindwa
kusema Neno jingine la mbele, sasa hata kunena
kupo kwa namna hii yaani mtu anashindwa
kubadilisha maneno utasikia tu

“laba laba laba laba laba laba laba laba laba laba
laba”
Ukiona hii ya kurudia rudia hasa baada ya kuomba
kwa muda fulani ujue sio kwamba wewe ni
mchanga kiroho ila Mungu anataka akuvushe
Mahali au kuna tatizo anataka ulishinde ndo
anakupa hii yaani hii ni kama funguo au kodi au
“password” tatizo tunatumia Sana hekima za
kibinadamu sikia kuna jambo unavushwa kuna
viwango unaingizwa huko kurudia rudia ndio
funguo yako sikia ukikuta simu yenye password ya
1111111 je utaandika moja tu na kusema nyingine
zinajirudia hapana utaandika zote Ili ukamilishe
password, sikia kule kurudiarudia ndio
kunakokamilisha funguo yako rohoni kwa sababu
sio wewe uliyetunga hayo maneno bali ni Roho
Mtakatifu hivyo yeye anakupa maneno hayo, hivyo
maneno yamepangiliwa na Roho Mtakatifu kabisa
na anaelewa anafanya nini
Matendo ya mitume 2:4
[4]Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka.
Haleluya Utukufu kwa YESU wetu

Mfano mzuri fimbo ya musa ni moja ila tu ila


iligeuka Kuwa nyoka, hiyo Hiyo iligeuka Kuwa fimbo
ya haruni hiyo Hiyo ndo ilipasua bahari ya shamu
sikia endelea na “laba laba laba laba laba laba laba
laba laba” mpaka bahari ya shamu yako ipasuke
hivyo Wengine hawawezi kukuelewa hivyo endelea
tu mbele

1 Wakorintho 2:14-15
[14]Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei
mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni
upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa
yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
[15]Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala
yeye hatambuliwi na mtu.

USIMZIMISHE ROHO tena umeshafahamu hiyo


endelea Sana mbele
Nini kinakupata ukinena kwa lugha.

• Unaongea mambo ya siri ambayo wewe


hauyafahamu.

Mfano kama hapo juu nilivyokuonesha jinsi


nilivyookolewa dhidi ya mauti Kupitia kunena kwa
lugha.

• Kunena kwa lugha kunaleta Hekima ( akili)

Unaenda kufanya usahili kwa ajili ya Kazi nena kwa


lugha kabla ya kuingia, unaenda kuongea na Binti
umuoe nena kwa lugha kwa muda fulani
hautakataliwa kizembe zembe, unataka umfanyie
mtu ushauri nena kwa lugha utaona Hekima kubwa
inakuja na kukuongoza katika Maisha Yako.

Ayubu 32:8
[8]Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi
za Mwenyezi huwapa akili.

• Kunena kwa lugha kunahuisha Maisha Yako ya


kiroho

Ukinena kwa lugha unahuisha antenna zako za


kiroho na kufungua masikio na ufahamu wako wa
rohoni na kuhuisha Maisha ya Maombi tena.
Yuda 1:20
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu
iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho
Mtakatifu,
2)KUCHEKA KATIKA ROHO
Hii ni ishara ya kushinda katika mapito Yako au pia
ni ishara ya kuinuliwa kiroho.

Hii hali ilitokea sana wakati wa huduma ya mtumishi


wa Mungu kenneth e hagin watu Walikua
wanacheka mnoo na Hii ni ishara ya kumshinda adui
Yako

Zaburi 59:8
[8]Na Wewe, BWANA, utawacheka, Utawadhihaki
mataifa yote.

Mithali 1:26
[26] Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,
Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;

Hapo juu ni Mungu anatumia vinywa vitu Ili


atazangaze mshindi wa ushindi
Isaya 35:10
[10]Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi,
watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele
itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko
na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
Hivyo ukisikia rohoni hali ya kucheka we cheka nae
tu mruhusu Roho Mtakatifu kuna Mahali
anakushindia tatizo fulani unalopitia, haleluya YESU
mzuri

3)KUIMBA KATIKA ROHO


Mathayo 26:30
[30] Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje
kwenda mlima wa Mizeituni. Yesu asema kuwa
Petro Atamkana

Waefeso 5:19
[19]Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za
rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana
mioyoni mwenu;

Wakolosai 3:16
[16]Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu
katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana
kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku
mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

4)KUCHEZA KATIKA ROHO


Hii unakuta mtu amezama kabisa rohoni lakini
anasikia kuendelea kuomba huku akiwa anacheza
kabisa kimwili na Hii ni ishara kuwa kuna ushindi au
mpenyo katika Maisha Yako.

Malaki 4:2
[2]Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la
haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake;
nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama
wa mazizini.

Kwa sababu kizazi chetu hakijui hivyo watu


hupuuzia hali kumbe Roho Mtakatifu Huwa
anatangaza kuinuliwa au ushindi katika nyanja
Mbalimbali za Maisha ya mtu huyo.
5)KULIA KATIKA ROHO
Hiki ni kiwango ambacho mtu hufikia kinywa chako
hakiwezi kustahimili uzito wa unachokiongea na hii
hutokea rohoni pale ambapo Roho Mtakatifu ana
jambo lake zito juu Yako ambalo Kikawaida
kutamkika ni ngumu.

Yohana 11:35
Yesu akalia machozi.

Waebrania 5:7
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule,
awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti,
maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi,
akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

Luka 19:41
Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
Nini hutokea pale watu wakilia ni kutembea katika
viwango vikubwa vya kimiujiza ,pia kutembea katika
kibali na kuinuliwa kiungu katika Maisha yetu

6)KUUGUA ROHONI
Hii ni dalili inayoonesha kuwa kwa akili Yako
umeshindwa kuombea jambo kiusahihi na jambo la
lazima ndo Roho Mtakatifu anaingia Kati kuugua
rohoni mwako na hali hii huwa inaambatana na
suala la kukosa amani hii ni dalili kuwa jambo sio
jema ila linahitaji muombaji sana pia huwa anakupa
kuugua kwa ajili ya watakatifu wengine ili wasipotee
katika Jina la Yesu.
Warumi 8:26-27
[26]Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,
kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa.
[27]Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho
ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama
apendavyo Mungu.

Sasa mkristo ikimtokea hiyo hali wengine wetu


hujizuia na hata kuwatafuta watu watuchangamshe
Ili hii hali iondoke na kweli hufanikiwa kuiondoa hii
hali ila tukio lile lililopangwa hutokea kweli na
kuleta majuto makuu.

7)KUTETEMEKA
Hii ni hali inayoashiria ni uwepo wa Mungu wa
kiwango cha juu sana eneo hilo

1 Wafalme 19:11-12
[11]Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za
BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi
wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja
miamba mbele za BWANA; lakini BWANA
hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo,
tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika
lile tetemeko la nchi;
[12]Na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto;
lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada
ya moto sauti ndogo, ya utulivu.

8)KUPIGA KELELE
Hii ni alama mojawapo inayowakilisha ushindi

Warumi 8:26
[26]Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,
kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa.

Mwingine hii kuugua kusikoweza kutamkwa sasa


Wengine humaanisha piga kelele kusikoweza
kutamkwa kwa kadiri Roho Mtakatifu anavyomjalia
mtu wa Mungu kuvuka kwa kupiga kelele
Zaburi 66:1-3,5-6
[1]Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
[2]Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake.
[3]Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama
nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako
watakuja kunyenyekea mbele zako.
[5]Njoni yatazameni matendo ya Mungu; Hutisha
kwa mambo awatendayo wanadamu;
[6]Aligeuza bahari ikawa nchi kavu; Katika mto
walivuka kwa miguu; Huko ndiko mlikomfurahia.

Kelele ni ishara ya ushindi na ishara ya matendo


makuu ya Mungu katika Maisha Yako

Yoshua 6:2,4-5
[2]BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia
Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na
mashujaa wake.
[4]Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba
za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo
sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara
saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao.
[5]Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za
kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia
sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa
sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale
pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea
mbele kukabili.

Kelele ni mbinu kabisa ambayo inafahamika na


mbingu ili kumsaidia mwanadamu kushinda na
kumiliki oh haleluya

Yoshua 6:10
[10]Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige
kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote
lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile
nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo
mtakapopiga kelele.

Hivyo ukisikia kwenye Maombi kupiga kelele piga


kelele sana tu au mtumishi au mchungaji
anaposema piga kelele basi piga kelele sana kuna
ushindi wako hapo.

Yoshua 6:16,20
[16]Hata mara ya saba makuhani walipozipiga
tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele;
kwa maana BWANA amewapeni mji huu.
[20]Basi watu wakapiga kelele, na makuhani
wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu
waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga
kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji
ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu,
wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili
mbele; wakautwaa huo mji.
Mi Sijui unapitia nini ila ninachokijua kelele inaweza
kukutoa hapo ulipo najua kibinadamu hakuna
anayependa kelele kwa sababu Kikawaida hazina
Maana ila kwenye ulimwengu wa roho ina Maana
kubwa Sana kwa sababu roho zinajua Maana ya
kelele na zinapambanuliwa na kujulikana zina
Maana gani ashukuriwe huyu Mungu kwa kuwa
yeye anachuja na kuelewa kelele

9)MGUSO WA MOTO KWENYE SEHEMU ZA MWILI


Hii ni ishara ya madhihirisho ya uwepo wa malaika
kwenye eneo ulilopo
Sikia hata kipindi hiki utendaji Kazi wa Malaika bado
upo na ni halisi Sana kuliko hata kipindi cha agano la
kale

Waebrania 1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa
kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Ufunuo 19:10
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili
nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi
ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda
wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda
wa Yesu ndio roho ya unabii.

Ufunuo 22:8-9
[8]Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona
mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona
nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika
yule mwenye kunionyesha hayo.
[9]Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni
mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale
wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie
Mungu.

Malaika ni wajumbe na watendakazi wetu hivyo


ukiokoka tu unakaribisha shughuli za malaika
kwenye maisha Yako oh haleluya Utukufu kwa
Mungu tumpendae hatupo wenyewe ijapokua
hatuoni kwa macho lakini haimaanishi kuwa
hawapo kwenye Mazingira yetu

2 Wafalme 6:15-17
[15]Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule
mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje,
kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari,
wameuzingira mji ule. Mtumishi wake
akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?
[16]Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi
ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
[17]Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi,
mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA
akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona;
na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na
magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.

Matendo 12:7
Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye,
nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro
ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi.
Minyororo yake ikamwanguka mikononi.

Maombolezo 1:12-13
[12]Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia,
Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yo yote
mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi,
Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya
hasira yake iwakayo.
[13] Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu,
Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu,
Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa
pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.

Moto huu huwakilisha vitu vifuatavyo


• Uwepo wa malaika wa Uponyaji.
Yohana 5:4
Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka,
akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye
aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa,
akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]

Kuna watu huniuliza kaka Paulo Mbona unasema


kuna malaika Mahali hapa je unamuonaje kama
yupo huwaga nawaambia kiukweli simuoni ila kuna
hali fulani ya moto nikiisikiaga huwa najua malaika
wa Uponyaji yupo hapa huyu ndo kwenye biblia
wanamuita “uweza wa kuponya”

• Maandalizi juu ya Kusudi ulilolibeba.


Isaya 6:6-7
[6]Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka
akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi
mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo
toka juu ya madhabahu;
[7]akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo,
akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako,
na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako
imefunikwa.
Kutoka 3:2
Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa
moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na
kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti
hakikuteketea.

• Udhihirisho wa Malaika wa Mungu ambaye


hushughulikia Kusudi ulilolibeba.

Mwanzo24:40
Akaniambia, BWANA, ambaye naenenda machoni
pake, atapeleka malaika wake pamoja nawe,
atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu
mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya
babangu.

Hii unakuta mtumishi anapitia mazingira ambayo


hayamuoneshi kama atakua vile Mungu
alimwambia kuwa hivyo malaika hujidhihirisha
namna hii kama ishara ya kuwa utafika kule Mungu
anapotaka ufike ikiwa utatembea katika njia za
MUNGU

• Ni ishara ya ulinzi wa Mungu juu Yako


Kutoka 23:20
[20]Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele
yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali
pale nilipokutengezea.

10) KUSHANGILIA KATIKA ROHO


Ni hali ya kusikia furaha juu ya jambo fulani na
kuonesha waziwazi

Pia mitandaoni wameweka Maana nzuri kidogo ya


kushangilia.
Neno “shangilia” lilitumiwa sana na Wakristo wa
mapema. Ilikuwa wito wa furaha na mara nyingi
hutumika kama salamu . Wakati fulani, Yesu
angeingia chumbani na kuwaita watu mara moja
kwenye shangwe badala ya kutumia kiwango
“jambo.” Furaha ni zaidi ya furaha tu.” Yesu hakuwa
akiwaita watu kucheza na kucheka au kujiburudisha
bali kufurahi toka ndani.

Furaha hii hailetwi na mpenzi au sababu nyingine


yoyote ile ila ni ROHO MTAKATIFU ndio Maana
Daudi alisema usiniondolee Roho wako Mtakatifu
kisha nirejeshee furaha ya wokovu sikia furaha hii
chanzo chake ni ROHO MTAKATIFU ndio kuna siku
unasikia furaha sana tangu ulipoamka asubuhi pia
unaweza kuta katikati ya Maombi unasikia hii
furaha na kushangilia hii ni Mungu mwenyewe

1 Petro 1:8
[8]Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona;
ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na
kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye
utukufu,

Petro anaiita furaha isiyoneneka wazungu wanaiita


“joy unspeakable” na sifa ya hii furaha ni kuwa
imejaa utukufu oh haleluya.

Mitume na baadhi ya watu wa Kanisa la kwanza


waliita furaha ya Roho Mtakatifu.

1 wathesalonike 1:6
Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha
kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na
furaha ya Roho Mtakatifu.

Warumi 14:17
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali
ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Matendo ya mitume 13:52
Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
Mtume Paulo pia anaiita “furaha yote”
Warumi 15:13
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha
yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana
kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Zaburi 118:24
[24]Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia
na kuifurahia.

Na Hii ndo ilimtokea Daudi wakati wa Siku ambayo


anaenda kumuua goliati alisikia furaha
iliyoambatana na maneno ya ushindi na ukiri na
mimi namwambia hali hii ikikutokea ruhusu lakini
isindikize na maneno ya ushindi, kuweza na
kutawala kama Daudi hebu tuangalia zaburi 144
yote Maana ndiyo maneno aliyoyatamka wakati
anaenda kumuua goliati.

Zaburi 144:1-15
[1]Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,
Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu
kupigana.
[2]Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na
mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia,
Huwatiisha watu wangu chini yangu.
[3]Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue? Na
binadamu hata umwangalie?
[4]Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni
kama kivuli kipitacho.
[5]BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke,
Uiguse milima nayo itatoka moshi.
[6]Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale
yako, uwafadhaishe.
[7]Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,
Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
[8]Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao
wa kuume ni mkono wa uongo.
[9]Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa
kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
[10]Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi,
mtumishi wake, na upanga wa uovu.
[11]Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni.
Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa
kuume ni mkono wa uongo.
[12]Wana wetu na wawe kama miche Waliokua
ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni
Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
[13]Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote.
Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu
mashambani mwetu.
[14]Ng’ombe zetu na wachukue mizigo, Kusiwe na
kushambuliwa. Wala kusiwe na kuhamishwa, Wala
malalamiko katika njia zetu.
[15]Heri watu wenye hali hiyo, Heri watu wenye
BWANA kuwa Mungu wao.

Ukisikia hali hii basi usiache na usiruhusu Shetani


akutoe hivyo kataa taarifa mbaya ukiweza kaa peke
Yako pia unaweza kuhatamia hii hali kwa kunena
kwa lugha au kukiri maandiko yenye ushindi

11) MGUSO WENYE HOFU YA GIZA


Hii ni ishara kuwa kuna uwepo wa giza au kuna
mipango ya giza imepangwa kwa ajili Yako na ipo
karibu kutimia

Ayubu 4:12-16
[12]Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu
likasikia manong’ono yake.
[13]Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya
usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo
wanadamu.
[14]Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha
mifupa yangu yote.
[15]Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na
nywele za mwili wangu zilisimama.
[16]Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua
sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu;
Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,

Ukisikia hali hii usijifanye mjuaji hata ukatafuta muvi


au tamthilia kutazama ili upate amani ya moyo sikia
hii ni dalili yenye kuashiria kuna ubaya hivyo kemea
sana kila mpango wa giza uwe unaujua au Hata
kama hauujui na ukipata Muda nena sana kwa lugha

12) MACHALE YA KIROHO


Utasikia mtu akisema nilihisi tu kuwa ile gari itapata
ajali na Kweli ilipata ajali hii hali ukiisikia basi ifanyie
kazi kwa haraka sana.
Mwengine kuna mtu siku ya kwanza tu ukakosa
amani nae na ukaona asiwe rafiki yako lakini kwa
sababu ulitaka uonekane sio mtu mbaya basi
ukamkubali na kumpokea kuwa rafiki yako aisee leo
hii Maisha Yako ya ibada yapo chini sana, Maisha
Yako ya kiroho yameporomoka huna hamu ya ibada
wala hamu ya kusoma Neno wala vitabu.
Wengine mkaka fulani alivyokufuata kuwa
anakupenda ukasita na hata ukakosa amani ya
moyo na hata ukimpima kwenye Neno huyo mkaka
unaona amepwaya lakini wewe kwa sababu ni
mama huruma ukamuhurumia na leo unaona
matokeo yake ndo unasikia mtu anasema ndo
maana nilisikia kumkataa mie.

Hizo zote hapo juu ni Mifano ya machale ya kiroho


lakini Haya mambo hayakuanzia kwetu ila yalianza
toka agano la kale na agano la kale walitumia vitu
vinaitwa “urimu na thumimu”

Kutoka 28:30
Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko
cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo
wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya
BWANA; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana
wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya BWANA
daima. Mavazi mengine ya Ukuhani

Urimu na thumimu
Katika Agano la kale Mungu alikuwa akitumia njia
kuu tatu aidha kuwasilisha ujumbe au leta majibu
au kuthibitisha jambo..Njia ya kwanza ni manabii,
njia ya pili ni ndoto, na njia ya tatu ni Urimu na
thumimu.
Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha 1Samweli 28:4
pale ambapo Mfalme Sauli alipokwenda kuuliza kwa
Bwana kuhusu vita iliyokuwa inamkabili mbele yake
dhidi ya wafilisti, Kama watashinda au La, lakini
Bwana hakumjibu kwa njia yoyote kati ya hizo tatu..
1Samweli 28:4 “Nao Wafilisti wakakusanyika,
wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli
akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema
katika Gilboa.
5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo
Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana.
6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana
hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala
kwa manabii”.

URIMU NA THUMIMU maana yake ni nini?


Urimu maana yake ni “Mianga” Na Thumimu
“mikamilifu”..Haya Ni mawe 12 ya aina tofauti
tofauti yaliyokuwa yamegundishwa katika ki-mfuko
kidogo kilichokuwa kinakaa katika kifua cha kuhani
mkuu. Hivyo ikiwa kuna jambo watu wanahitaji
kupata uhakika kutoka kwa Bwana basi Mawe haya
yalikuwa yanatoa mwanga Fulani unaoakisiana,
kuthibitisha jambo hilo, Na hivyo kama jambo hilo
sio sawa basi hayakutoa mwanga wowote. Urimu na
Thimumu ilikuwa inatoa jibu la mwisho japo si mara
zote ilikuwa inatumika.

Kwa mara ya kwanza urimu na thumimu


inaonekana katika kitabu cha
Kutoka 28:29-30
29 Na Haruni atayachukua majina ya wana wa
Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu
ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali
patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya Bwana
daima.
30 Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile
kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu
ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele
ya Bwana; na Haruni atachukua hukumu ya hao
wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Bwana
daima.
Walawi 8:6
Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe,
akawaosha kwa maji.
7 Kisha akamvika Haruni ile kanzu, na kumfunga
mshipi, na kumvika joho, na kumvika naivera, na
kumfunga huo mshipi wa kazi ya mstadi wa naivera
na kumfunga naivera kwa huo mshipi.
8 Kisha akamtia kile kifuko cha kifuani; akatia hizo
Urimu na Thumimu katika hicho kifuko cha kifuani.
9 Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu
ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande
cha dhahabu, hiyo taji takatifu; kama Bwana
alivyomwagiza Musa.

Kumbukumbu la Torati 33:8


Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina
mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta
naye kwenye maji ya Meriba.

Hesabu 27:21
Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye
atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za
BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake
wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja
naye, mkutano wote pia.
Tunaona tena, wakati mfalme Sauli alipopishana na
mwanawe kuhusu kuvunjwa viapo ambavyo
alivyoweka, alitaka Mungu ahukumu katikati yao ni
nani mwenye makosa, Hivyo alitumia Urimu na
Thumimu kuomba uthibitisho huo.

1Samweli 14:41 “Kwa hiyo Sauli akamwambia


Bwana, Mungu wa Israeli, [Kwani usimjibu mtumishi
wako leo? Ikiwa dhambi I ndani yangu, au ndani
yake Yonathani mwanangu, Ee Bwana, Mungu wa
Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi I
katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu ,Basi
Yonathani na Sauli wakatwaliwa,lakini watu
wakapona”.

Kwa sasa hatuna urimu na thumimu ya kimwili ila


tunayo ya rohoni ambayo ndo hii Huwa
inatukosesha amani kwa watu fulani na kutupa
mashaka juu hata ya gari za kupanda au Hata watu
ambao watakuzunguka hivyo sasa Haya ndo
tunayaita machale ya Kiroho.
SURA YA TATU
MATOKEO YA KUTOKUZIZIMISHA DALILI ZA ROHO
MTAKATIFU.
• Kama tujuavyo kuwa yeyote ambaye anatii sauti
ya Mungu basi mtu huyo atastawi sana na kuwa
mtu bora sana

Mwanzo 26:1-2,6,12-13
[1]Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya
kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka
akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko
Gerari.
[2]BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda
Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
[6]Isaka akakaa katika Gerari.
[12]Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata
mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA
akambariki.
[13]Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi,
hata akawa mkuu sana.
• Baraka zitakufuata
Kumbukumbu la Torati 28:1-2
[1]Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu
wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake
yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako,
atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
[2]na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata
usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
• Hautakosea njia au kufeli.
Huwezi ukachumbia au kuchumbiwa alafu
ukaachwa au ukaacha
Zaburi 32:8
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Isaya 30:21
na masikio yako yatasikia neno nyuma yako,
likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda
mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa
kushoto.

Yaani hautotembea kwa kubahatisha kamwe katika


Jina la Yesu.
Naitwa Paulo Evarist Koba nimeokoka na nampenda
sana YESU, Muhitimu wa ngazi ya astashahada pale
kwenye chuo cha ufundi cha DIT.
Niliokoka Mwaka 2014 nikiwa kidato cha tatu huko
shuleni nilipokua nasoma elimu ya sekondari, tangu
hapo Maisha yangu yamebadilika kabisa.
Ninaabudu kanisa la Gilgal Revival Church pia ni
mtoto wa kiroho wa mchungaji Paulo Israel Shaban.
Haya maarifa nimejifunza Kupitia kwa Baba yangu
wa kiroho Askofu Paul Israel Shaban.
Kama umeguswa na huduma hii na una ushuhuda
kuhusu hiki kitabu basi karibu kwa namba za hapo
chini pia kama unataka kutushika mkono kwa
sadaka Yako karibu kwa mawasiliano ya hapo chini
pia kwa ushauri na msaada wa kiroho karibu sana
kupitia Email ifuatayo paulokoba395@gmail.com na
mawasiliano ya 0783428460 au mitandao ya kijamii
nitafute kama Evarist Koba.
Vitabu vinginevyo vilivyoandikwa na mwandishi.

✓USICHOCHEE MAPENZI
✓KIJANA ALIYEOKOKA NDANI YA BABILONI
✓MAHALI PA SIRI PA MUNGU
✓UELEWE ULIMWENGU WA ROHO

You might also like