Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 76

MWANANGU TIMOTHEO

By Brother Paulo Evarist Koba 1


MWANANGU TIMOTHEO

MWANANGU
TIMOTHEO

By Brother Paulo Evarist Koba 2


MWANANGU TIMOTHEO

YALIYOMO

YALIYOMO……………………………….………………...…..….3
TABARUKU……………………….. ……………………….………4
LENGO LA KITABU………………………....….….…...…...…5
MFAHAMU TIMOTHEO.....................................……7
KWANINI UWE MWANA KAMA TIMOTHEO ?.......28
GHARAMA YA KULELEWA KIROHO….……………..….42
HEKIMA YA KUISHI NA MTUMISHI WA MUNGU...47
NAMNA YA KUPATA UPAKO……………………….....….61
KUHUSU MWANDISHI……………………..…………........72

By Brother Paulo Evarist Koba 3


MWANANGU TIMOTHEO

TABARUKU

NI SHAUKU YA MOYO WANGU KUKISAIDIA KIZAZI


CHANGU KWA HABARI YA UFALME WA MUNGU NA
KUWEKA NJAA NA KIU YA KUMJUA MUNGU PIA
KUINUA WATU WALIO TAYARI KWA AJILI YA
MUNGU AMBAO HAWAJAJIKINAI YAANI ASKARI
WAAMINIFU HIVYO NI MATUMAINI YANGU KUPITIA
MAARIFA HAYA KUNA JESHI KUBWA LITAINUKA NA
KUFANYA KANISA KUTAWALA NA KUMILIKI KATIKA
TAIFA NA MATAIFA KUPITIA VITABU HIVI VYA KI-
ELECTRONIKI AMBAVYO NI BURE KABISA KWA KILA
ATAKAYE.

TANZANIA, WEWE NI JIKO LA KUPIKIA MAISHA


HALISI YA WOKOVU.

By Brother Paulo Evarist Koba 4


MWANANGU TIMOTHEO

Lengo la kitabu hiki ni

Lengo la kitabu ni kusaidia watoto wengi wa Kiroho


waweze kutulia na kulelewa Vizuri kwa baba zao wa
kiroho ili waweze Kuwa watoto Bora na waweze
kurithi Neema za Baba zao.

By Brother Paulo Evarist Koba 5


MWANANGU TIMOTHEO

“Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga


kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa
katikati yetu, Kama walivyotuhadithia na
kufundisha wale waliokuwa mashahidi ambao ni
wazee wetu wa imani wenye kuyaona, na
watumishi wa lile neno tokea mwanzo, Nimeona
vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi
wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia
kwa taratibu, ewe ndugu yangu mpendwa Katika
Bwana, Upate kujua hakika ya mambo yale
yalivyotokea na uliyofundishwa.”

By Brother Paulo Evarist Koba 6


MWANANGU TIMOTHEO

SURA YA KWANZA

MFAHAMU TIMOTHEO

Katika kitabu hiki, Cha MWANANGU TIMOTHEO,


ninawasilisha mmoja wa wana wa Mtume Paulo,
anayeitwa Timotheo. Nimekipa kitabu hiki jina hili ili
kukutia moyo na kukuchochea kuishi kama Mwana
halisi na upendwaye Kwa baba Yako wa Kiroho Kwa
kufuata aina ya hekima na utii aliokuwa nao
Timotheo.

Mfano wa picha ya Timotheo na Mtume Paulo.

By Brother Paulo Evarist Koba 7


MWANANGU TIMOTHEO

Paulo na Timotheo walikua na Uhusiano wa pekee,


kiasi kwamba Paulo alimwamini na kumtenga kama
“mwana mpendwa” na Kitabu hiki ni ushuhuda wa
uwana halisi wa Timotheo hivyo basi lengo la kitabu
hiki ni, Kufunua Uwana wa Kweli. Uwana wa kweli
ni fumbo hilo na ni Lazima lifunuliwe. Ni imani
yangu kwamba unaposoma kitabu hiki, utakuwa
unatiwa moyo kufuata namna ya uwana ambayo
Paulo na Timotheo Walikua nayo.

Mungu katika hekima yake isiyo na kikomo aliamua


kwamba ataitawala dunia kupitia wale ambao Ni
kama Yeye, wanawe na binti zake. Kwa sababu ya
upendo wake mkuu, alijifanya mwenyewe kuwa
mwanadamu Ili aweze kutupata wanadamu Kwa
kuwa ni Sheria ya kiungu kuwa bila Mwili huwezi
ukafanya KAZI dunia kama Kitabu Cha (Mwanzo
1:26) kinavyoonesha na tangu wakati huo yote
Aliyotaka kufanya katika ulimwengu wa dunia,
Anafanya Kupitia mwanadamu. Ni kwa sababu hizo,
alipotaka kumkomboa mwanadamu, alimtuma
Mwanawe kama mwanaume. Fahamu hili; Mungu
hafanyi chochote katika ulimwengu bila ya Mtu.
Angalia Maandiko haya katika kitabu cha Ezekiel

By Brother Paulo Evarist Koba 8


MWANANGU TIMOTHEO

Ezekieli 22:30-31

[30]Nami nikatafuta mtu miongoni mwao,


atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele
zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije
nikaiharibu, lakini sikuona mtu. [31]Kwa sababu
hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao;
nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami
nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao,
asema Bwana MUNGU.

Angalia hilo, mapenzi ya Mungu yalikuwa ni


kuwahurumia watu lakini kwa sababu Yeye
Hakuweza kupata mtu wa kushirikiana naye katika
utekelezaji wa mpango Wake, Hakuwa na Chaguo,
lakini kutuma hukumu. Sasa kama Mungu hafanyi
lolote bila mwanadamu kwanini Kwamba waumini
wanafikiri kwamba kwa ajili ya mafanikio maishani
wanachohitaji ni Mungu tu? Sijali jinsi gani Hali yako
ni mbaya, lakini jua hili, Mungu hatashuka kutoka
mbinguni kuja Kukukomboa kutoka kwayo, ikiwa
hajawahi kushuka wakati mwanawe mpendwa Yesu
alipolia Kwake kutoka msalabani, ni nini
kinakufanya ufikiri atashuka kwako kwa sababu

By Brother Paulo Evarist Koba 9


MWANANGU TIMOTHEO

Unapitia changamoto? Sikia Ukimtaka Mungu,


tafuta Mtumishi ambaye Anambeba Mungu na
kisha kunyenyekea chini ya mtu huyo na Mungu
atatokea kwako yaani kama haujawahi
kunyenyekea Kwa MTU ambaye ni mwakilishi wa
Mungu basi wewe ni mnafki kusema utanyenyekea
Kwa MUNGU.

Tangu vizazi Mungu huchagua Mtu kumuweka Kwa


ajili ya kumsaidia na kumlea mtu ambaye hasa
amebeba Kusudi lake HIVYO MTU yeyote
atakayefaulu kwanza kunyenyekea na kutulia chini
ya MTU HUYO basi MUNGU ndo atamtumia hata
Elisha alipofaulu chini ya Elia ndo akainuliwa Kuwa
nabii mkubwa sana katika biblia mda
hautotoshabkuelezea habari za kina
Samweli,Daudi,Musa,Henoko,Methusela,Nuhu,Mitu
me watu waliokubali kulelewa na Baba zao wa
Kiroho na hatimaye Kuwa watu wakubwa
tunaowafanya Kuwa Mfano wa kuigwa.

Mtumishi wa Mungu najua utakua umewahi kusikia


kuhusu Kitabu Cha Timotheo kinachoonesha jinsi

By Brother Paulo Evarist Koba 10


MWANANGU TIMOTHEO

inavyotakiwa kuwa mahusiano baina ya Baba na


Mtoto wake wa kiroho.

Kutokana na vijana WENGI hasa wa kizazi chetu


kushindwa kufuata utaratibu huu wa Kuwa chini ya
Baba wa kiroho hivyo basi tumeibua
watoto(hawana sifa kuwa watumishi wa Mungu
aliye hai) ambao wana makosa mengi Sana hivyo
basi kupitia Kitabu hiki watasaidikika na kukaa sawa
na Baba zao wa kiroho na wengineo.

Huduma yoyote Ile Ili iwe na matokeo ni lazima


huyo aliyebeba hiyo Huduma awe na nidhamu
madhubuti Kwa waliomtangulia.

Nanukuu “Ninaamini kwamba moja ya hitaji kuu


katika kizazi chetu, leo, ni hitaji la Baba wa kiroho.
Hasa, Baba wa kiroho ambaye amechaguliwa kwa
mapenzi ya Mungu katika maisha ya mwana na
binti. Baba wa kiroho hubeba moyo wa Baba wa
Mbinguni ndani yake. Anawapenda na kuwajali
watoto wake wa kiroho, kupitia wonyesho wa
mbinguni wa upendo na utunzaji wa Mungu.
Anawazaa kiroho, hutoa ushauri, kifuniko cha

By Brother Paulo Evarist Koba 11


MWANANGU TIMOTHEO

kiroho, mwongozo, uzazi wa kiroho na uangalizi. Pia


anatoa mfumo wa uwajibikaji. Anasaidia kuunda
ndani yao tabia ya kimungu na kuwafinyanga ili
waakisi sura ya Kristo.”

Tuone biblia inasemaje kuhusu mahusiano baina ya


baba wa Kiroho na mtoto wake wa kiroho

1 Wakorintho 4:17

[17]Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu,


aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika
Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika
Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika
kila kanisa.

Niwajibu wa Kila Mwana kutii na kunyenyekea na


kukubali kulelewa na Baba yake wa Kiroho Mpaka
pale atakapopevuka KIHUDUMA na Kuwa tayari na
kupakwa mafuta na Mungu mwenyewe Kwa ajili ya
Kusudi alilolibeba pia tunajifunza Kwa Mfalme sauli
ambaye alikubali kukaa chini ya baba yake mpaka
pale alipokua ametumwa kutafuta punda na
kukutana na Nabii Samwel ambaye alimpaka mafuta
kama ishara ya kuwekwa wakfu na Roho Mtakatifu
By Brother Paulo Evarist Koba 12
MWANANGU TIMOTHEO

Kwa ajili ya kutumiwa na Bwana Yesu na Kwa ajili ya


Huduma.
1 Samweli 9:19-21
[19]Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi
mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka
mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami
leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami
nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako.
[20]Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu,
usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na
yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa
nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako?
[21]Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si
Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila
zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko
jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi,
kuniambia hivyo?
Hapo Juu kutoka katika hayo maandiko tunaona
namna ambavyo sauli anakutana na Upako wa
Kifalme lakini baada ya utumishi Mwema Kwa Baba
yake hivyo ikiwa unataka utumiwe Kwa viwango

By Brother Paulo Evarist Koba 13


MWANANGU TIMOTHEO

vikubwa kabla ya kufunga Sana na kwenda kwenye


makambi mengii ya Maombi basi heshimu
waliokutangulia katika Imani maana usipofanya
hivyo ukengeufu upo mlangoni mwako nao HAKIKA
yake utakua mtumwa kwake.

TAFAKARI, MTAZAMO NA MAWAZO YANGU JUU


YA TIMOTHEO NA MTUME PAULO
TIMOTHEO anatembea taratibu katika barabara
inayotoka nyumbani kwao, macho yake yakitazamia
kwa hamu mambo yaliyokuwa mbele yake.
Waandamani wenzake wanaongoza njia
wanapopita katika mashamba ambayo Timotheo
anayafahamu vizuri sana. Kadiri wanavyotembea
ndivyo wanavyozidi kuliacha jiji la Listra lililokuwa
juu ya kilima. Timotheo anatabasamu
anapokumbuka jinsi mama na nyanya yake
wanavyojivunia maendeleo yake ingawa
wanahuzunika kumwona akiondoka. Je, ageuke na
kuwapungia mkono kwa mara ya mwisho?
Mara kwa mara, mtume Paulo angemtazama
Timotheo na kutabasamu. Ingawa alijua kwamba
By Brother Paulo Evarist Koba 14
MWANANGU TIMOTHEO

Timotheo alikuwa mwenye haya kwa kiasi fulani,


alifurahishwa na shauku ya kijana huyo. Timotheo
alikuwa kijana sana, labda mwishoni mwa utineja au
umri wa miaka ishirini na kitu, na alimpenda na
kumheshimu sana Paulo. Sasa Timotheo alikuwa
akisafiri mamia ya kilometa kutoka nyumbani
pamoja na mwanamume mwenye bidii na
mwaminifu. Wangesafiri kwa miguu na meli, na
wangekabili hatari nyingi njiani. Kwa kweli,
Timotheo hakujua ikiwa angerudi nyumbani.
Kwa nini kijana huyo alichagua maisha ya aina hiyo?
Angepata baraka gani kwa sababu ya kujidhabihu
kiasi hicho? Tunajifunza nini kutokana na imani ya
Timotheo?
“TANGU UTOTO MCHANGA”
Hebu turudi nyuma miaka miwili au mitatu katika jiji
la Listra ambalo Timotheo aliishi. Ulikuwa mji
mdogo wa mashambani katika bonde lenye maji
mengi. Huenda watu wa eneo hilo walizungumza
lugha yao ya Kilikaonia ingawa walijua pia Kigiriki.
Siku moja, mji huo wenye utulivu ulivurugika.
Wakristo wawili wamishonari, mtume Paulo na

By Brother Paulo Evarist Koba 15


MWANANGU TIMOTHEO

Barnaba waliwasili kutoka jiji kubwa la karibu


lililoitwa Ikoniamu. Walipokuwa wakihubiri
hadharani, Paulo alimwona mwanamume mlemavu
aliyeonyesha imani ya kweli. Hivyo, Paulo alifanya
muujiza na kumponya mwanamume huyo!—
Matendo 14:5-10.
Inaonekana kwamba watu wengi katika jiji la Listra
waliamini hekaya zilizodai kwamba zamani kulikuwa
na miungu iliyojifanya kuwa wanadamu na
kutembelea eneo hilo. Hivyo, watu walidhani
kimakosa kwamba Paulo alikuwa Herme na Barnaba
alikuwa Zeu! Ilikuwa vigumu kwa Wakristo hao
wanyenyekevu kuwazuia watu wasiwatolee
dhabihu.—Matendo 14:11-18.
Hata hivyo, kwa wakazi wachache wa Listra, pindi
hiyo haikuwa ziara ya miungu ya kipagani
inayotajwa katika hekaya bali watumishi wa Mungu
aliye hai Kwa mfano, ni wazi kwamba Eunike,
mwanamke Myahudi aliyeolewa na mwanamume
Mgiriki asiye mwamini, pamoja na mama yake, Loisi,
waliwasikiliza Paulo na Barnaba kwa shauku na
shangwe kubwa na Hatimaye walikuwa wakisikia
habari ambazo kila Myahudi mwaminifu alizisubiri
By Brother Paulo Evarist Koba 16
MWANANGU TIMOTHEO

kwa hamu. Habari hizo zilisema kwamba Masihi


alikuja na alitimiza unabii mwingi kumhusu
ulioandikwa katika Maandiko!
Fikiria jinsi ziara ya Paulo ilivyomsaidia Timotheo.
“Tangu utoto mchanga,” Timotheo alizoezwa
kupenda maandishi matakatifu ya Maandiko ya
Kiebrania. (2 Timotheo 3:15) Kama mama na nyanya
yake, Timotheo aliona wazi kwamba Paulo na
Barnaba walisema kweli kumhusu Masihi. Mfikirie
mwanamume kilema aliyeponywa na Paulo. Huenda
tangu alipokuwa mvulana, Timotheo alimwona
mara nyingi mwanamume huyo katika mitaa ya
Listra. Sasa, Timotheo anamwona mwanamume
huyo akitembea kwa mara ya kwanza! Haishangazi
kwamba Eunike, Loisi, na Timotheo wakawa
Wakristo. Leo, wazazi, babu na nyanya, wanaweza
kujifunza mengi kutoka kwa Loisi na Eunike. Je,
mnaweza kuwawekea mfano mzuri vijana?
“KUPITIA DHIKI NYINGI”
Ni wazi kwamba Wakristo katika jiji la Listra
walisisimuka sana walipojifunza kuhusu tumaini la
wafuasi wa Kristo. Hata hivyo, walijua pia kwamba

By Brother Paulo Evarist Koba 17


MWANANGU TIMOTHEO

wangehitaji kujidhabihu ili kuwa wafuasi wa Kristo.


Wayahudi wapinzani wenye msimamo mkali kutoka
Ikoniamu na Antiokia waliingia jijini na
kuwachochea watu wasiwasikilize Paulo na
Barnaba. Muda mfupi baadaye, umati wenye hasira
kali ulimfuata Paulo na kumpiga kwa mawe.
Walimpiga mpaka alipoanguka chini. Kisha
wakamkokota mpaka nje ya jiji wakidhani kwamba
alikuwa amekufa.—Matendo 14:19.

Hata hivyo, wanafunzi katika mji huo wa Listra


walienda na kumzunguka Paulo. Walifurahi sana
Paulo aliposimama na kurudi tena Listra kwa ujasiri!
Siku iliyofuata, Paulo na Barnaba walienda Derbe ili
waendelee na kazi ya kuhubiri. Baada ya kupata
wanafunzi wapya huko, walirudi tena Listra kwa
ujasiri licha ya hatari ambayo huenda ingewakabili.
Walifanya hivyo kwa kusudi gani? Simulizi hilo
linasema kwamba ‘walizitia nguvu nafsi za
wanafunzi, wakiwatia moyo kubaki katika imani.’
Wazia kijana Timotheo akisikiliza na kuwatazama
Paulo na Barnaba walipowafundisha Wakristo hao
kwamba tumaini lao tukufu la wakati ujao ni lenye
By Brother Paulo Evarist Koba 18
MWANANGU TIMOTHEO

thamani sana kuliko mateso wanayokabili.


Walisema: “Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu
kupitia dhiki nyingi.”—Matendo 14:20-22.
Timotheo alikubali kwa moyo wote mafundisho ya
mtume Paulo
Timotheo alimwona Paulo akiishi kulingana na
maneno hayo, akikabili dhiki kwa ujasiri ili
awahubirie wengine habari njema. Kwa hiyo,
Timotheo alijua kwamba ikiwa angefuata mfano wa
Paulo, angepingwa na watu wa Listra na huenda
hata baba yake mwenyewe angempinga. Lakini
Timotheo hakutaka kuruhusu mambo hayo yaathiri
uamuzi wake wa kumtumikia Mungu. Leo, kuna
vijana wengi walio kama Timotheo. Kwa hekima,
wanatafuta marafiki walio na imani yenye nguvu
ambao watawatia moyo na kuwaimarisha. Na
hawaruhusu upinzani uwazuie kumtumikia Mungu
wa kweli!

“ALISHUHUDIWA VEMA NA AKINA NDUGU”

By Brother Paulo Evarist Koba 19


MWANANGU TIMOTHEO

Kama ilivyotajwa mwanzoni, huenda Paulo


alitembelea tena miaka miwili au mitatu hivi
baadaye. Hebu wazia msisimko uliokuwa nyumbani
kwa akina Timotheo wakati Paulo alipowasili akiwa
pamoja na Sila. Kwa hakika, ulikuwa wakati wenye
shangwe kwa Paulo. Alijionea mwenyewe matokeo
ya mbegu za kweli alizopanda Listra. Loisi na binti
yake, Eunike, walikuwa wanawake Wakristo
washikamanifu wenye ‘imani isiyo na unafiki’
ambayo ilimvutia Paulo. (2 Timotheo 1:5) Vipi
kuhusu kijana Timotheo?

Paulo aliona kwamba tangu alipowatembelea


wakati uliopita, kijana huyo alikuwa amekomaa
kiroho. Timotheo “alishuhudiwa vema na akina
ndugu,” huko Listra na pia Ikoniamu, kilometa 32
hivi upande wa kaskazini-mashariki.
(Matendo 16:2) Aliwezaje kupata sifa nzuri?
“Maandishi matakatifu” ambayo Timotheo
alifundishwa “tangu utoto mchanga” na mama na
nyanya yake yalitia ndani shauri zuri kwa ajili ya
vijana. (2 Timotheo 3:15) Kwa mfano, fikiria shauri
By Brother Paulo Evarist Koba 20
MWANANGU TIMOTHEO

hili: “Mkumbuke, sasa, Muumba wako Mkuu katika


siku za ujana wako.” (Mhubiri 12:1) Timotheo
alielewa vizuri zaidi maneno hayo baada ya kuwa
Mkristo. Alitambua kwamba njia bora zaidi ya
kumkumbuka Muumba wake Mkuu ilitia ndani
kuhubiri habari njema kuhusu Mwana wa Mungu,
Kristo. Hatua kwa hatua, Timotheo aliacha kuona
haya ambayo ilimzuia kuwa na ujasiri wa
kuwahubiria wengine habari njema kuhusu Yesu
Kristo.

Wanaume walioongoza makutaniko waliona


maendeleo ya Timotheo. Hapana shaka walivutiwa
na jinsi kijana huyo alivyowajenga na kuwachochea
wengine. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Timotheo
alipata kibali cha Yehova. Mungu aliongoza unabii
fulani utolewe kumhusu Timotheo—huenda ulihusu
utumishi ambao siku moja angetimiza katika
makutaniko. Paulo alipowatembelea, aliona kuwa
Timotheo angekuwa mwandamani mzuri katika
safari za umishonari. Ndugu wa Listra walikubaliana
na jambo hilo. Walimwekea mikono kijana huyo,
kuonyesha kwamba alikuwa amewekwa rasmi
By Brother Paulo Evarist Koba 21
MWANANGU TIMOTHEO

kumtumikia Yehova Mungu katika utumishi wa


pekee.—1 Timotheo 1:18; 4:14.

Tunaweza wazia jinsi Timotheo alivyostaajabu na


kuhisi hastahili kutokana na kuaminiwa na
kukabidhiwa jukumu hilo kubwa. Alikuwa tayari
kutimiza mgawo huo, Hata hivyo, baba yake asiye
mwamini alihisije aliposikia kwamba mwana wake
alipenda kutumikia kama mhudumu Mkristo
anayesafiri? Inaelekea kwamba alikuwa na malengo
tofauti kuhusu wakati ujao wa mtoto wake. Vipi
kuhusu mama na nyanya ya Timotheo? Je,
walijivunia maendeleo ya kijana huyo huku
wakificha wasiwasi wao kuhusu usalama wake? Ni
kawaida kuwa na hisia hizo.

Tuna uhakika kuwa Timotheo aliondoka. Asubuhi


iliyotajwa mwanzoni mwa makala hii, ilikuwa
mwanzo wa maisha ya kusafiri na mtume Paulo.
Alipokuwa akiiacha nyuma Listra, kila hatua
aliyopiga alipotembea ilimaanisha hatua nyingine
kuelekea njia asiyoijua mbali na nyumbani. Baada ya
By Brother Paulo Evarist Koba 22
MWANANGU TIMOTHEO

kutembea kwa siku nzima, wanaume hao watatu


walifika Ikoniamu. Timotheo alianza kuona jinsi
Paulo na Sila walivyotoa miongozo ya karibuni zaidi
kutoka baraza linaloongoza lililokuwa Yerusalemu
na walivyojitahidi kujenga imani ya waamini katika
Ikoniamu. (Matendo 16:4, 5) Lakini, huo ulikuwa
mwanzo tu.

Baada ya kutembelea makutaniko katika Galatia,


wamishonari hao waliziacha barabara pana
zilizotengenezwa na Waroma na kutembea mamia
ya kilometa kupitia maeneo yaliyoinuka ya Frigia
wakielekea kaskazini na kisha magharibi. Wakifuata
mwongozo wa roho takatifu ya Mungu, walienda
Troa na kupanda meli kuelekea Makedonia.
(Matendo 16:6-12) Kufikia wakati huo, Paulo aliona
jinsi ambavyo Timotheo aliwasaidia sana. Paulo
aliweza kuwaacha Timotheo na Sila katika mji wa
Beroya. (Matendo 17:14) Hata alimtuma kijana
huyo akiwa peke yake kwenda Thesalonike. Akiwa
huko, Timotheo alitumia mambo aliyoona kutoka
kwa akina Paulo na Sila, na aliwatia moyo Wakristo

By Brother Paulo Evarist Koba 23


MWANANGU TIMOTHEO

waaminifu katika Thesalonike.—1 Wathesalonike


3:1-3.
Baadaye, Paulo aliandika hivi kuhusu Timotheo:
“Sina mtu mwingine yeyote aliye na mwelekeo
kama wake atakayejali kwa unyoofu mambo yenu.”
(Wafilipi 2:20) Hakupata sifa hiyo nzuri kimuujiza.
Timotheo alipata sifa nzuri kupitia jitihada,
unyenyekevu, na kuvumilia kwa uaminifu hali
ngumu. Huo ni mfano mzuri sana kwa vijana leo!
Kumbuka kwamba jitihada zako ndizo
zitakazokufanya upate sifa nzuri. Ukiwa kijana, una
fursa ya pekee ya kupata sifa nzuri kwa
kumtanguliza Mungu kwanza maishani mwako na
kwa kuwaheshimu na kuwaonyesha fadhili wengine.

“FANYA KABISA YOTE UNAYOWEZA ILI UJE


KWANGU”
Timotheo alijitoa katika huduma ya Kikristo akiwa
na umri mdogo na Kwa zaidi ya miaka 14 hivi,
Timotheo alitumia muda mrefu akifanya kazi na
Baba yake wa kiroho mtume Paulo. Alikabili hatari
nyingi na alifurahia mambo mengi katika kazi hiyo.
By Brother Paulo Evarist Koba 24
MWANANGU TIMOTHEO

(2 Wakorintho 11:24-27) Hata aliwahi kufungwa


gerezani kwa sababu ya imani yake. (Waebrania
13:23) Kama Paulo, aliwapenda na kuwahangaikia
sana ndugu na dada zake Wakristo. Ndiyo sababu
Paulo alimwandikia hivi: ‘Ninayakumbuka machozi
yako.’ (2 Timotheo 1:4) Sawa na Paulo, inaelekea
kwamba Timotheo alijifunza ‘kulia pamoja na watu
wanaolia,’ akijitahidi kuelewa hisia zao ili aweze
kuwatia moyo na kuwafariji. (Warumi 12:15) Kila
mmoja wetu na ajitahidi kufanya hivyo!

Haishangazi kwamba baada ya muda, Timotheo


alifanikiwa sana akiwa mwangalizi Mkristo. Pamoja
na kumkabidhi jukumu la kuyatembelea makutaniko
ili kuyaimarisha na kuyatia moyo, Paulo alimpa pia
daraka la kuwaweka rasmi wanaume wanaostahili
kutumika wakiwa wazee na watumishi wa huduma
katika makutaniko.—1 Timotheo 5:22.

Paulo alimpenda sana Timotheo, na alimpa maagizo


na ushauri unaofaa kama vile baba anavyofanya
kwa kijana wake. Alimhimiza Timotheo athamini
By Brother Paulo Evarist Koba 25
MWANANGU TIMOTHEO

zawadi za kiroho alizokuwa nazo na aendelee kukua


na kufanya maendeleo. (1 Timotheo 4:15, 16)
Alimtia moyo Timotheo asiruhusu kamwe ujana
wake—na huenda haya aliyokuwa nayo—imzuie
kutetea lililo sawa ilipohitajika kufanya hivyo. (1
Timotheo 1:3; 4:6, 7, 11, 12) Pia, Paulo alimshauri
jinsi ya kushughulikia ugonjwa wa tumbo ambao
huenda ulimpata mara kwa mara kijana huyo.—1
Timotheo 5:23.
Wakati ulifika ambao Paulo alijua kuwa mwisho wa
maisha yake ulikuwa karibu; inaonekana muda
mfupi baadaye angeuawa kwa kunyongwa.
Alimtumia Timotheo barua yake ya mwisho
iliyoongozwa na roho. Ilitia ndani maneno haya
yenye kugusa moyo: “Fanya kabisa yote unayoweza
ili uje kwangu upesi.” (2 Timotheo 4:9) Paulo
alimpenda sana Timotheo; alimwita “mtoto wangu
mpendwa na mwaminifu katika Bwana.” (1
Wakorintho 4:17) Haishangazi kwamba alitaka
Timotheo, rafiki yake, awe naye alipokaribia
kuuawa! Inafaa kila mmoja ajiulize, ‘Je, watu
hunifuata ili wapate faraja wanapokabili matatizo?’

By Brother Paulo Evarist Koba 26


MWANANGU TIMOTHEO

Je, Timotheo aliweza kufika kwa Paulo kabla


hajauawa? Hatujui. Tunajua kuwa sikuzote alifanya
yote awezayo kumfariji na kumwimarisha Paulo na
wengine wengi. Timotheo aliishi kupatana na
maana ya jina lake, yaani, “Mtu Anayemheshimu
Mungu.” Ametuachia mfano mzuri sana wa imani
tunaoweza kuiga iwe sisi ni vijana au wazee.

By Brother Paulo Evarist Koba 27


MWANANGU TIMOTHEO

SURA YA PILI
KWANINI UWE MWANA KAMA TIMOTHEO?
Kupitia kuwa mwana Timotheo anapata vitu
vilivyomsaidia kufikia na kulitimiza kusudi lake Hapa
Duniani kama tujuavyo kuwa huyu Timotheo ndiye
baadae alikuja kuwa Askofu Mkuu wa KANISA LA
EFESO,hivyo basi tunashawishika kabisa kuwa
Timotheo alipata vitu sahihi wakati akiwa chini ya
mtume Paulo na vifuatavyo ni baadhi ya vitu
alivyovipata huyu Timotheo;
1. Timotheo alipewa kanuni za kufanikiwa katika
Huduma na maisha kiujumla na Mtu
aliyemtangulia ambaye ni Mtume Paulo.
Wazee au WATU Waliokutangulia wao wanaona
mambo ya Leo yajayo lakini pia
kinachowaongezea thamani zaidi wao
wamejifunza kutokana na mambo yaliyopita
hivyo wao Wanamuono wa mambo
yaliyopita,yasasa na yajayo tofauti na vijana sisi
tunaona Sasa na tunapoelekea mtumishi mmoja
akasema mzee mmoja ni sawa na maktaba
nyingi zilizobeba maarifa hivyo Wao wanajua
By Brother Paulo Evarist Koba 28
MWANANGU TIMOTHEO

mtu akifanya jambo Fulani basi ataishia sehemu


Fulani wao wanajua Maana maisha ni kanuni na
mtu akifanya jambo Fulani basi matokeo yake
yanajulikana

1 Timotheo 4:6,13,15
[6]Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe
utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na
mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho
mazuri yale uliyoyafuata.
[13]Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika
kusoma na kuonya na kufundisha.
[15]Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili
kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.

1 Timotheo 6:11
[11]Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie
mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani,
upendo, saburi, upole.

By Brother Paulo Evarist Koba 29


MWANANGU TIMOTHEO

Kwa mfano hapo anamsihi na kumpa kanuni


zitakazomsaidia kufanikiwa katika Huduma
aliyopewa na mfano wa mambo ambayo
aliambiwa Ili afanikiwe ni kuachana na hadithi
za kizee zisizokua za dini,kupenda fedha na
kadhalika

2.Anapewa utaratibu na Namna ya uendeshwaji wa


KANISA/HUDUMA Kutoka Kwa Mtume Paulo.

1 Timotheo 3:1-13
[1]Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya
askofu,atamani kazi njema. [2]Basi imempasa
askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke
mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu,
mkaribishaji, ajuaye kufundisha; [3]si mtu wa
kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si
mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda
fedha; [4]mwenye kuisimamia nyumba yake vema,
ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; [5](yaani,
mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe,
atalitunzaje Kanisa la Mungu?) [6]Wala asiwe mtu

By Brother Paulo Evarist Koba 30


MWANANGU TIMOTHEO

aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka


katika hukumu ya Ibilisi. [7]Tena imempasa
kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke
katika lawama na mtego wa Ibilisi. [8]Vivyo hivyo
mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli
mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu
wanaotamani fedha ya aibu; [9]wakiishika siri ya
imani katika dhamiri safi. [10]Hawa pia na
wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya
shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.
[11]Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si
wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika
mambo yote. [12]Mashemasi na wawe waume wa
mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na
nyumba zao. [13]Kwa maana watendao vema kazi
ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi
katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

1 Timotheo 5:1-6
[1]Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na
vijana kama ndugu; [2]wanawake wazee kama
mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike;
katika usafi wote. [3]Uwaheshimu wajane walio

By Brother Paulo Evarist Koba 31


MWANANGU TIMOTHEO

wajane kweli kweli. [4]Lakini mjane akiwa ana


watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda
yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na
kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika
mbele za Mungu. [5]Basi yeye aliye mjane kweli
kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea
Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi
na sala mchana na usiku. [6]Bali, yeye asiyejizuia
nafsi yake amekufa ingawa yu hai.
Hapo juu tunaona utaratibu mzima wa Namna ya
uendeshwaji wa KANISA/HUDUMA Kibiblia Sasa
haya mambo Timotheo asingeyapata popote kule
ila Kwa BABA yake wa kiroho la sivyo Timotheo
ambaye hapo baadae Alikua Askofu Mkuu wa
KANISA LA EFESO angekua na mfumo mbaya wa
uendeshwaji wa KANISA/HUDUMA katika Jiji la
EFESO.
3.Anapewa Mafundisho sahihi ambayo inabidi na
Yeye arithishe kizazi kingine.
Kama tujuavyo kuwa mafundisho (doctrine) watu
hurithishwa kutoka Kwa kizazi kilichowatangulia
kama ambavyo biblia ilishatoa utaratibu wake na Ili

By Brother Paulo Evarist Koba 32


MWANANGU TIMOTHEO

mtumishi yeyote yule awe na usahihi katika


mafundisho yake ni Lazima awe amerithishwa
mafundisho sahihi na yenye uhakika Kibiblia hivyo
basi Timotheo naw alirithishwa mafundisho yenye
usahihi yaliyomsaidia kuwa Mtumishi Mwema
katika KAZI za KRISTO

1 Timotheo 4:11,16
[11]Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.
[16]Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu
katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo
utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

1 Timotheo 6:2
[2]Na wale walio na bwana waaminio
wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; bali afadhali
wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya
kazi yao wamekuwa wenye imani na kupendwa.
Mambo hayo uyafundishe na kuonya.

By Brother Paulo Evarist Koba 33


MWANANGU TIMOTHEO

2 Timotheo 2:2,14-15
[2]Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya
mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu
watakaofaa kuwafundisha na wengine.
[14]Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya
machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya
maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu
wasikiao.
[15]Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na
Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari,
ukitumia kwa halali neno la kweli.

2 Timotheo 3:10,14
[10]Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na
mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani,
na uvumilivu,
[14]Bali wewe ukae katika mambo yale
uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua
ni akina nani ambao ulijifunza kwao;

By Brother Paulo Evarist Koba 34


MWANANGU TIMOTHEO

BAADHI YA MASWALI AMBAYO YATAKUSAIDIA


Ntampataje na kumjua baba yangu wa kiroho?

NI KWA KUANGALIA MAMBO YOTE MATANO


YAFUATAYO

i) Awe mtu wa rohoni na si mtu wa mwilini

ii) Kiroho chake kiwe juu ya chako

iii)tabia, mwenendo na maadili) yasiwe na maswali.

iv) Awe mtu aliye na vitu ulivyobeba au aliyeweza


kulea watu wenye vitu vya aina yako.

v)Awe mtu ambaye anaruhusu watu wamfuate


kama yeye anavyomfuata Kristo, wakiona anapotea
wamuache wabaki na Yesu!

MSHIRIKISHE MUNGU KWA MAOMBI, MPAKA UWE


NA AMANI NA UHAKIKA KABLA YA KUMFUATA MTU
KUMUOMBA AWE BABA YAKO WA KIROHO.

Nani anamfuata mwenzake kujitambulisha, baba


au mtoto?

By Brother Paulo Evarist Koba 35


MWANANGU TIMOTHEO

YEYOTE KATI YAO ANAWEZA.

-Eliya alimfuata Elisha,

-Yesu aliwafuata Zakayo, Mathayo, Petro na


wengine wengi ambao walimfuata baada ya yeye
kuwaambia NIFUATE!

-Wanafunzi wa Yohana walimfuata Yesu, wakaenda


kwake na hawa kurudi tena kwa Yohana. Bali
walianza kuwaleta wenzao kwa baba yao mpya,
Yesu!

HIVYO, KUNA WAKATI BABA HUMFUATA MTOTO


NA KUNA WAKATI MTOTO HUMFUATA BABA!

NAKUSHAURI UMFUATE BABA, USISUBIRI


AKUFUATE!

Je ni lazima baba wa kiroho awe mchungaji au


anachunga kanisa?

By Brother Paulo Evarist Koba 36


MWANANGU TIMOTHEO

Yesu hakuwa na jengo wala dhehebu analolichunga


lakini alikuwa na watoto wa kiroho anaowalea na
kuwaandaa!

Musa hakuwa na jengo na dhehebu lakini aliwalea


akina Joshua na Kalebu na wale 70 waliokuwa chini
yake.

UBABA NI MAJUKUMU, SI CHEO.

UBABA SI HUDUMA BALI NI UWAJIBIKAJI.

Nikiwa Mwalimu wa Neno la Mungu, tayari nilikuwa


na watoto wa kiroho zaidi ya 70, niliokuwa
nafuatilia maendeleo yao ya kiroho, uchumi,
mahusiano, familia na malezi, makusudi
waliyobeba, maono, ndoto na malengo yao, na
kuwa simamia, kuwakazania, na kuhakikisha
wanayafikia na kuyaishi!

Mtu yeyote aliye na sifa za ubaba, nilizotaja kwenye


sura zilizotangulia, na ANAWAJIBIKA, hata kama
hachungi, huyo ni baba sahihi, kaa naye

By Brother Paulo Evarist Koba 37


MWANANGU TIMOTHEO

Je ninaweza kubadili baba wa kiroho? Kama ndiyo,


kwa sababu zipi?

NDIYO, UNAWEZA KUBADILI BABA WA KIROHO.

Sababu za kubadili baba wa kiroho;

1. Ukigundua hana ulivyo navyo au hawezi kuvilea


ulivyobeba, na hajawahi kulea mtu au watu wa aina
yako!

Kwa Usalama wako, tafuta utakakolelewa vizuri.

2. Akiwa na matatizo ya kitabia, maadili na


mwenendo (character)!

Mfano ameshindwa kukaa kwenye ndoa yake,


ameiacha imani, amejiunga na imani potofu,
ameacha kumfuata Yesu, ameanza kuibia na
kutapeli watu kwa jina la Yesu, ameanza masuala
machafu kama uzinzi na zinaa, na mengine ya
namna hii!

By Brother Paulo Evarist Koba 38


MWANANGU TIMOTHEO

3. Pale unapokuwa na Yohana Mbatizaji, kumbe


uliwekwa kwake kwa muda, akulee ila akija Yesu,
ndiye haswa unayepaswa kuambatana naye!

Rejea: Habari za wanafunzi wa Yohana waliomuacha


na kumfuata Yesu na kuwa wanafunzi wake (Yohana
1)!

NB: UKIFANYA BIASHARA YA KUHAMA HAMA


KUTOKA BABA HUYU HADI YULE NJE YA SIFA HIZI,
WEWE UNAKUWA NA MATATIZO, NA HUJUI HATA
MAANA YA UBABA WA KIROHO.

Nini ni majukumu ya baba wa kiroho?

i) Kuongoza kwa mfano (leading by doing), baba


yeyote lazima awe kioo na walioko nyuma yake
wajifunze kwake kwa matendo na si notice!

ii) Awe kioo cha kitabia (character image) kwa


watoto wake.

By Brother Paulo Evarist Koba 39


MWANANGU TIMOTHEO

iii) Awe mtu anayewaunganisha watu na Bwana


Yesu na si kuchukua utukufu na mahali pa Yesu!

iv) Awe mshauri anayefuata baada ya Roho


Mtakatifu kwa watoto wake.

v) Kuwatambulisha wanawe kwa walimu bora na


makini waliomo ndani ya Kristo, badala ya
kuwaaminisha kwamba yeye pekee ndiye ana kitu
cha kuwafaa.

vi) Usimamizi na uangalizi (overseer and


supervisor): Lazima awe msimamizi na mwangalizi
wa vipawa, huduma, karama, wito na makusudi
waliyobeba watoto wake!

Lakini pia lazima awe msimamizi wa hali zao


kiuchumi, ndoa, familia, malezi nakadhalika!

Je naweza kuwa na baba wa kiroho zaidi ya


mmoja?

By Brother Paulo Evarist Koba 40


MWANANGU TIMOTHEO

Hapana haiwezekani, baba ni mmoja tu, ila ruksa


kuwa na walimu maelfu maelfu wa kujifunza kwao
ila walio na tabia na ushuhuda wa kristo!

“Kwa kuwa ijapokuwa MNA WAALIMU KUMI ELFU


KATIKA KRISTO, walakini HAMNA BABA WENGI.
MAANA MIMI NDIMI NILIYEWAZAA KATIKA KRISTO
YESU KWA NJIA YA INJILI. BASI NAWASIHI
MNIFUATE MIMI…”

(1Wakorintho 4:15-16).

By Brother Paulo Evarist Koba 41


MWANANGU TIMOTHEO

SURA YA TATU

GHARAMA YA KULELEWA KIROHO.

Naitwa Paulo Evarist Koba, ninatokea makanisa ya


Gilgal Revival Church ambayo makao makuu yake ni
Gongo la mboto Ulongoni na ninalelewa na Baba
yangu wa Kiroho Bishop Paul Israel Shaban.

Huko Nyuma nilikua mtoto mwenye mambo mengi


sana yaani naenda kufanya huduma na Yeye hajui,
au najiamlia tu kwenda Ibada au lah utasikia naingia
Maombi lakini nilipoamua kutulia nikasema
sitaenda kufanya huduma bila taarifa kwa mzee
wangu Bishop Paul Israel Shaban ndipo nilipoona
gharama ya kukaa chini ya Mtumishi wa Mungu
akulee.

Kuna mialiko mingi tu alinizuia kwenda kabisa na


mwanzoni aisee nilikua nakwazika mnoo lakini Yeye
akishasema jambo harudii tena sasa kuna siku
nilienda kibaha kwenye makongamano ya CASFETA
na nililala huko sasa cha ajabu akiwa hajanipanga
muda mrefu kuhubiri kwenye Ibada za asubuhi
akanitumia meseji Saa kumi na moja na dakika 29
By Brother Paulo Evarist Koba 42
MWANANGU TIMOTHEO

ongoza Ibada na ufundishe aisee alafu nilikua nipo


kibaha aisee nikamtumia meseji mwenyewe niliona
ni unyenyekevu mnooo nikamwambia baba
samahani nipo kibaha akakaa kimya ilipofika Saa
mbili akatuma meseji niwakute kanisani Saa Nne
kamili aisee tukachukua pikipiki watu watatu
mshikaki tulikua tunamwambia dereva aisee ongeza
tu mwendo hatuwezi pata ajali tukafika Mahali
mvua ikanyesha lakini tukamwambia bodaboda we
twende tu acha tuloe ila tufike kwa wakati hatimaye
tukafika tukiwa tumeloa kasoro dakika kadhaa
akatusamehe.

Kuna mialiko wewe mwenyewe unatamani kwenda


lakini Baba akisema usiende inakupasa utulie na
usiende na wala usiwe na kinyongo najua wengine
mtasema ni utumwa huu sasa yaani kuacha kwenda
kuhubiri na kubaki kanisani tu bila kuhubiri utasema
ukienda kuhubiri ufalme utatanuka hahah
umechengwa sana, hata sasa siendi kuhubiri
makanisani kama yeye hajui yaani huwa wanaongea
nae na akikubali ndo ninaenda akisema hapana ujue
siji.

By Brother Paulo Evarist Koba 43


MWANANGU TIMOTHEO

Kuna kipindi nina mifungo yangu binafsi alafu


anatuita vijana wake binafsi utasikia nunua soda
hapo mnywe au ukimtembelea kwake unasikia koba
chukua chakula ule hapo yaani hakuna mfungo
unaoendelea hapo ni unakula bila maneno,
anaweza kukuonya wakati wowote na Sehemu
yoyote ile bila maswali unaitikia ndio bila kinyongo.

Sasa wewe endelea kuwa mjuaji sana kwa Baba


Yako na Kusema umekua Kiroho na wengine hamna
Baba kabisa alafu unataka uwe mbali na Salama
Sawa haina shida tutakuona, wengine wachungaji
wenu hawawezi kuwaonya kwa sababu ni wajuaji
sana.

Leo hii Kupitia kukaa chini ya Baba wa Kiroho Bishop


Paul Israel Shaban nimeona kesho yangu
itakavyokua yaani nina uhakika wa kuwa na
matokeo ya kushikika kabisa.

Kabla ya kuwa Mtumishi wa Mungu unatakiwa uwe


Mtumishi wa Mtumishi wa Mungu kwanza.

By Brother Paulo Evarist Koba 44


MWANANGU TIMOTHEO

Yoshua 1:1
[1]Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa
BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa
Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,

Mtoto wa kiroho akiwa chini ya Baba huwa maono


yake yanakaa pembeni na kufanya maono ya Baba
yake tu.

Yohana 5:19,30
[19]Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile
ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote
ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile
vile.

[30]Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama


nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu
ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu
mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

By Brother Paulo Evarist Koba 45


MWANANGU TIMOTHEO

Ulimwengu wa kiroho na Watu hawashangai upako


ila watakuuliza ni nani baba yako

1 Samuel 17:55-56,58
[55]Basi Sauli, hapo alipomwona Daudi akitoka ili
kumwendea yule Mfilisti, alimwambia Abneri,
jemadari wa jeshi, Je! Abneri, kijana huyu ni mwana
wa nani? Abneri akamjibu, Ee mfalme, kama
iishivyo roho yako, mimi siwezi kusema.

[56]Basi mfalme akasema, Ulizaf wewe, kijana huyu


ni mwana wa nani.

[58]Basi Sauli akamwuliza, Wewe, kijana, u mwana


wa nani? Naye Daudi akamjibu, Mimi ni mwana wa
mtumishi wako, Yese, mtu wa Bethlehemu.

Unataka uwe na matokeo ya kushikika na Dunia


nzima imuone YESU Kupitia wewe basi unahitaji
Baba wa Kiroho la sivyo hutofika mbali hivyo acha
ujuaji kakae chini ya Baba wa Kiroho na kama hauna
Baba na unataka nitafute nitakuelekeza.

By Brother Paulo Evarist Koba 46


MWANANGU TIMOTHEO

SURA YA NNE

HEKIMA YA KUISHI NA MTUMISHI WA MUNGU


ALIYEKUZIDI.

Mtumishi wa Mungu ni mtu yeyote yule


anayemtumikia Mungu, Kwenye kizazi chetu tuna
tatizo kubwa hasa kwa watumishi vijana juu ya
namna ya kuishi na Mtumishi wa Mungu hasa
mwenye matokeo kuliko wewe au yule ambaye
Mungu alimuweka kukusaidia na aliwahi kukuvusha
Mahali fulani na kuwa hivyo ulivyo au hata kama
unamzidi matokeo lakini amekutangulia katika
kumtumikia MUNGU kuna namna ya kuishi nao kwa
sababu ijapokua wote tumeokolewa Sawa lakini
hatuko Sawa Kwenye ufalme wa Mungu kutokana
na jinsi watu walivyotembea na Mungu, mfano Elia
alifunga mvua na kulikua hamna namna nyingine
yoyote ile ya mvua kunyesha mpaka Elia mwenyewe
aombe tena yaani inamaana hata wangetokea watu
na kufunga saba kavu lakini mvua isingenyesha.

YESU mwenyewe alikua na upako kuliko Yohana


mbatizaji lakini alijishusha kwa Yohana mbatizaji na

By Brother Paulo Evarist Koba 47


MWANANGU TIMOTHEO

tena anasema inatupasa kutimiza haki yote na hapo


hakumaanisha tu ubatizo bali alimaanisha kuwa na
kuwaheshimu waliokutangulia.

Mathayo 3:15
[15]Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa
kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.

Hivyo kuna haja ya kuwaheshimu na kujua namna


gani hata ya kuwasiliana nao hata kama unaona
miujiza mingi inatokea kwako, Karama za Roho
Mtakatifu zinafanya Kazi hata kama umeandika
vitabu na yeye hajawahi kuandika sikia muheshimu.

Hata kama umekua maarufu kuliko yeye endelea


kumuheshimu maana wengine wanapokua maarufu
huwa Wana wadharau na hata wanahama kwao
tena kwa kejeli na kebehi nyingi sivyo hivyo
mtumishi mwenzangu kijana na kama Ukifanya
hivyo hata kama Mungu aliwahi kukuambia kitu
kuhusu wewe hakitotimia na utakua kama Gehazi
tu.
By Brother Paulo Evarist Koba 48
MWANANGU TIMOTHEO

Ukiona unaanza kutumiwa kama yeye


usijilinganishe nae muheshimu vilevile kama zamani
wala usihitaji kumshusha thamani kama ulikua
unamuita kaka endelea kumwita Hivyo hivyo kama
ulikua unamuita jina fulani kuonesha heshima Yako
kwake endelea.

Mithali 23:10a
[10]Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani;

Hekima hii nimejifunza namna ya kuishi na


Mtumishi wa Mungu.

Eneo la Mawasiliano.

Sikia kupata namba yake haimaanishi sasa ndo


umtumie kila kitu yaani utasikia meseji inaingia
“kamanda acha uvivu wewe hebu amka Saa nane
uombe”

By Brother Paulo Evarist Koba 49


MWANANGU TIMOTHEO

Au utasikia meseji “Mtumishi moto Upo?” Au


Wengine wanakutumia yale mameseji ya
kusambaza utasikia usiposambaza utakufa aisee
mimi Huwa sijibu Kabisa au mwengine anakupigia
akupigishe tu stori za ajabu tu.

Pia unakuta mtu anakutafuta anakuuliza kitu na


unamjibu vizuri tu na mnakubaliana atafanya hivyo
alafu anatoka hapo anamuuliza mtu mwengine tena
kitu hiko hiko na akipata anamuuliza mwengine
tena utasikia anamwambia yule mwengine kuwa
nilimuuliza kaka Paulo kanijibu hivi na hivi je ipo
Sawa hiyo, yaani nikionaga tu hivyo mtu huyo
akirudi tena kwangu huwaga sinaga majibu mengine
nitamwambia sijui.

Usitumie meseji kama unavyomtumia mtu


mwengine ukiweza andika meseji moja tu yenye kila
kitu mfano

“Baba Bwana YESU Asifiwe, shikamoo ni mimi Paul,


ninaendelea salama natumaini hata wewe pia,
Mahusiano yangu yapo vizuri,huduma yangu
inaendelea salama sana na natumaini kwa ruksa

By Brother Paulo Evarist Koba 50


MWANANGU TIMOTHEO

yako nitafanya jambo fulani na fulani nina


changamoto fulani fulani ahsante sana baba”

Meseji moja yenye adabu.

Mwingine unampigia simu usiku sana na unajua


ameoa aisee wewe.

Namna ya kukutana nae au kuongea nae.

Ukikutana nae usiwe mjuaji sana yaani usiongee


ongee hovyo tulia msikilize sana kuliko kujibu hata
kama Yesu alikutokea jana yake we kaa kimya na
usikilize siku moja tulikua na Mchungaji Peter
mahenge sasa kuna jamaa yaani kila mchungaji
Peter Mahenge akiongea yeye lazima atie neno lake
utasikia hapo na mimi niliwahi kuona Maono au
niliwahi kutumiwa na MUNGU ujue nikasema huyu
jamaa ajui anachokifanya kabisa.

By Brother Paulo Evarist Koba 51


MWANANGU TIMOTHEO

Alafu pia anamuita mchungaji Peter mahenge yaani


utasikia “mtumishi eeh” yaani ni hatari sikia sasa
ukikutana nae kuna majina ni mazuri hata kama Sio
mchungaji wako yaani sio Baba Yako wa kiroho ila
kwa sababu amekuzidi we mwite tu Baba yule
ambaye kichwa chake kimekaa vizuri sio hawa
wanaotafuta kuitwa Baba kwa lazima ambao
asilimia kubwa ni vijana na hawana matokeo kabisa
ila wale ambao kwa mwenendo wao
wamethibitisha kuwa wametembea na Mungu
Nakushauri tumia neno Baba au Mama kwa
watumishi wa kike itakusaidia Sana.

Kama Mungu amekubariki usiende mikono mitupu


maana hata waswahili husema mikono mitupu
hailambwi hivyo nenda na sadaka Yako akimaliza
kuongea mpatie na hata kama yuko mbali na
unabarikiwa na huduma yake mwombe namba yake
Mtumie sadaka Yako sikia mimi mwenyewe Huwa
nafanya hivyo hata kama nikiwa na buku tu naitoa
kama ilivyo

By Brother Paulo Evarist Koba 52


MWANANGU TIMOTHEO

1 Samwel 9:7-8
[7]Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini
angalia, kama tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu
gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu,
wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu;
tuna nini sisi?

[8]Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama,


mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha;
nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie
njia yetu.

Hiyo ni sadaka Yako kwake na wala haumsaidii kitu


kwa sababu mtumishi wa Mungu ni fursa ya
kubarikiwa kwako wewe na wewe sio fursa kwa
mtumishi wa Mungu ukielewa hili hutolingalinga
hovyo.

Akikukaribisha kula chakula basi kula kihekima usile


kama unataka kufa yaani ufakamia kila kitu aisee
usipakue zaidi ya alichopakua yeye hata kama una

By Brother Paulo Evarist Koba 53


MWANANGU TIMOTHEO

njaa kubwa na usimalize hiko chakula kula


kistaarabu ila ukiwa kwako kula mpaka uzimie.

Mfano kuna kijana ni Mtumishi mzuri sana ila


kwenye eneo la kula bado hajastaarabika kabisa
anajaza sahani mpaka inajaa kweli alafu sasa mjuaji
huyo yaani anaongea tu hata kama ndo mmealikwa
utasikia pale madhabahuni Fanya hivi na hivi au
anamwambia mpaka mchungaji mwenyeji utasikia
mtumishi wa Mungu sijawaelewa praise wako
kabisa wako hovyo sana aisee hutoitwa tena na
unajiharibia sifa Yako.

ISHARA HUYU MTUMISHI KIJANA AMEANZA


KUASI.
📍Kuona makosa ya Mchungaji wako (kuwa
mkosoaji wa hovyohovyo)
Hesabu 12:1
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa
sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa
amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke
Mkushi.
By Brother Paulo Evarist Koba 54
MWANANGU TIMOTHEO

Utasikia Mbona Mchungaji amechelewa Ibada leo


au utasikia Mbona mama Mchungaji amekosa Ibada
leo au umeona mama Mchungaji alivyosuka na
wengine hufika mbali husema sijapenda Mchungaji
anavyohubiri au Wengine utasikia siku hizi
Mchungaji anafundisha Muda mrefu sana hajui
kama tunachoka eeh.

Ukiona hali Hii juu ujue huyo mtumishi kijana


ameingiwa na roho ya uasi.
📍Mtumishi asiyeandika notsi wakati Mchungaji
kiongozi au Baba yako wa kiroho akifundisha.

Huyu anaashiria hana cha Kujifunza kwako Hivyo


hawezi kuandika na anajiona yuko Sawa na wewe
ndio maana mimi huwa haandiki Hii ni ishara kubwa
kwa mtu aliyeingiwa na roho ya uasi, wengine
husema Mbona Mchungaji haubiri kama Mchungaji
fulani au husema naweza kufanya kama Mchungaji
wangu tu hali hii ni mbaya mnoo.

By Brother Paulo Evarist Koba 55


MWANANGU TIMOTHEO

Nimekua nikialikwa kwenye makanisa makubwa na


madogo nimekutana na watu wa namna hii wengi
hawaandiki notsi na ni wazee wa Kanisa kabisa sikia
watu hawa usipowashughulikia wataleta uharibifu
mkubwa.

📍Mtumishi anayeona Maono ya Mchungaji wake ni


madogo na ya kijinga.
Kuna vijana huona wachungaji wao hawana Maono
na hata huwadharau kabisa watu wa hivi asilimia
kubwa Wana dalili kubwa ya uasi.
Utawasikia wakisema pale ningekua mimi
ningefanya hivi na vile aisee mtu wa hivi ni hatari
sana kwenye kazi ya MUNGU.

2 Samwel 15:4
[4]Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa
kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye
neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake!

By Brother Paulo Evarist Koba 56


MWANANGU TIMOTHEO

Watumishi wanaojiweka kutatua matatizo ya


washirika Bila ruhusa ya Mchungaji.
Husema haina haja ya kwenda Mchungaji ninaweza
kulitatua hili jambo hivyo hutengeneza vikundi
vidogo vidogo ambavyo humsikiliza yeye tu.

2 Samwel 15:2-3
[2]Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema,
na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa,
mtu ye yote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina
budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu
humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u
mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumwa wako ni
mtu wa kabila fulani ya Israeli.
[3]Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno
yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu
aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza.

Kujiamulia mambo mwenyewe Bila utaratibu yaani


hatoi Taarifa na wala haombi ruhusa.

By Brother Paulo Evarist Koba 57


MWANANGU TIMOTHEO

Utasikia leo kazindua vitabu Mahali fulani na


Mchungaji wake hajui au utasikia kaandaa Ibada au
mikutano ya injili Bila ruhusa na bado yupo chini ya
kanisa la Mchungaji wake ni mshirika na wala
Mchungaji wake hajui hii ni mbaya zaidi.

2 Samuel 18:5,14
[5]Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai,
akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa
upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia,
mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za
Absalomu.
[14]Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na
kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu
mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni,
alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.

Yoabu alikua anajiamulia mambo mwenyewe yaani


Mtume,nabii,Mwinjilisti,mwalimu na Mchungaji

By Brother Paulo Evarist Koba 58


MWANANGU TIMOTHEO

msaidizi yoabu alikua anajiamulia mambo


mwenyewe Bila kufuata utaratibu uliowekwa.

Mimi nimewahi kutumiwa na Yesu kwa vitu kadha


wa kadha kama vile mijiuza watu wenye kansa
wamepona, mtu asiyepalalaizi anatembea, wenye
ukimwi niliacha kuhesabu nilivyoingia chuoni
mwaka 2018 huko na mara ya mwisho walikua sita
na wengine sina idadi yake na nimekua nikitumiwa
kwa Karama za neno la maarifa, kutafsiri lugha,
kupambanua roho na kadhalika lakini pamoja na
hayo siwezi kwenda kwenye huduma yoyote kama
hao wanaonihitaji hawajaongea na Mchungaji
wangu na lolote atakalosema Mchungaji wangu
ndilo nitakalofanya hata akisema usiende basi ujue
sitaenda hapo kamwe mpaka yeye akiruhusu kuna
watu walikua wananisema sana ohh huduma Yako
inazikwa toka utumike wewe na wengine husema
Mungu hawezi kukuzuia kwenda Mahali huwa
ninawajibu Mchungaji wangu anaona zaidi ya mimi
ninavyoona pia mimi Sio mtumishi wa Mungu mimi

By Brother Paulo Evarist Koba 59


MWANANGU TIMOTHEO

bado nipo kwenye viwango vya kuwa Mtumishi wa


Mtumishi wa Mungu.
Sikia usibabaike na miujiza unayoiona Ukiwa
unatumika hebu fikiria pamoja hapa yaani Yoshua
katumika sana vitani kuua watu Ili israel ivuke lakini
pamoja na hayo yote mbingu ilikua inamtambua
kama ni mtumishi wa Musa tu.

Yoshua 1:1
[1]Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa
BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa
Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,

Huwezi kuwa Mtumishi wa Mungu kama haujawahi


kuwa Mtumishi wa Mtumishi wa Mungu au huwezi
kufanya Maono ya Mungu kama hujatumikia Maono
ya mtumishi wa Mungu.

By Brother Paulo Evarist Koba 60


MWANANGU TIMOTHEO

SURA YA TANO
NAMNA YA KUPATA UPAKO
Vijana Wengi tumekua tukifunga na kuomba Bila
mafanikio Ili kupata upako utakaotusaidia katika
Maisha ya Kusudi tulilolibeba.

Upako ndio unaozalisha matokeo na bila upako


hamna matokeo katika Maisha yetu na ndio maana
Yesu anasema tusitoke bila kujaa nguvu ya Mungu
ambayo ndiyo inaitwa Upako hivyo basi ni jukumu
letu kuhakikisha huu Upako unakaa juu yetu katika
Maisha yetu ya kila siku

Wengi wetu tumekua tukitamani viwango fulani vya


upako Kutoka kwa mababa wengi wa imani walio na
viwango vikubwa lakini ukiangalia baadhi yao
hatuna Hata mawasiliano nao na unatamani neema
walizonazo.

By Brother Paulo Evarist Koba 61


MWANANGU TIMOTHEO

Upako huja kwa njia kuu mbili nazo ni


1.Kuutafuta Kupitia kufunga,kuomba na usomaji wa
neno endelevu

2.Kupandikizwa kutoka kwa watu walio nao.


Hii ndio njia salama sana katika kuutafuta upako
ijapokua hii njia inahusisha kuomba,kufunga na
usomaji wa neno kama kawaida ila watu waliokuzidi
huja na kukufanya ujae viwango vikubwa zaidi vya
upako

Zifuatazo ni njia zinazotumika kupata upako wa


aina hii.
A.kutumika chini ya wengine waliofanikiwa kuwa na
upako.
Mfano
Elisha na Elia.
Timotheo na Paulo
Tito na Paulo

By Brother Paulo Evarist Koba 62


MWANANGU TIMOTHEO

Yoshua na Musa
Musa na mzee yethro

Ukitumika chini ya mtu uwe na uhakika kuwa kuna


viwango vya upako vinakaa juu Yako lakini utakaa
juu Yako kama utafanya yafuatayo.

Utafatilia maneno ya huyo mtumishi wa Mungu kwa


ukaribu sana.

Maneno ni roho hivyo yamebeba upako hivyo kadiri


unavyomsikiliza na kufatilia kwa makini maneno
yake basi ule upako ulio juu yake unakuja na kwako

Yohana 6:63
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno
hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Ezekiel 2:2

By Brother Paulo Evarist Koba 63


MWANANGU TIMOTHEO

Naye aliposema nami, roho ikaniingia,


ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.
Alipoongea nami roho au upako ukaniingia na
ukanisimamisha yaani ukanifanya niwe kama
aliyeongea

Ukimpenda na kumkubali kama mtumishi wa


Mungu Yaani ukimuheshimu

Mathayo 10:41
Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata
thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki
kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya
mwenye haki.

Thawabu ni pamoja na upako wa mtu huyo na kila


neema aliyoibeba.
B.Kusikiliza audio, kuangalia video, na kusoma
vitabu vyao mpaka uone hiyo neema imekaa kwako.

By Brother Paulo Evarist Koba 64


MWANANGU TIMOTHEO

Hii ni njia ya pale ambapo unakuta mtumishi wa


Mungu Sio mchungaji wako na pia hata yuko mbali
sana na Wewe.

Sikiliza audio zake iwe mchana, asubuhi, jioni hata


usiku na kuna kipindi Nilikua nikilala naweka audio
zinaendelea kupiga kwenye Simu yangu ijapokua
kuna Watu walinisema Kuwa natumia vibaya sana
fedha zangu kwa kununua MB sana lakini leo hii
wao ni mashahidi wa upako na neema zilizo Juu
yangu

Mfano Watu wengi hunishangaa katika eneo la


ushirika na ROHO MTAKATIFU huniuliza imekuaje
huwa nawajibu ni neema tu lakini ndani ya hii
neema nilisoma sana kitabu cha NAKUSALIMU
ROHO MTAKATIFU Zaidi ya mbili yaani nasoma
narudia tena kusoma alafu huku kila siku naangalia
video za benny Hinn aisee mpaka leo eneo ambalo
naona kwenye huduma yangu lina matokeo

By Brother Paulo Evarist Koba 65


MWANANGU TIMOTHEO

makubwa ni kumuhusu rafiki yangu kipenzi ROHO


MTAKATIFU.
Pia Nilikua nasikiliza audio na kuangalia video pia
kusoma sana vitabu vya kenneth e hagin leo huwezi
Kuwa na mashaka Juu ya neema iliyo Juu yangu
Kuwa kuna neema za Kenneth e hagin Juu yangu.

Mimi Sio mshirika wa apostle edu lakini ukiangalia


Maisha yangu ya Maombi utaona kitu kutoka kwa
apostle edu lakini pia Muda hautotosha kuelezea
neema kutoka kwa mtumishi wa Mungu Pastor
Peter mahenge maana hata kuhudumu kunafanana.

Utajuaje kama huo upako umeshakaa Juu Yako?


• Kufanya vitu ambavyo Huwa vinatokea kwa
huyo mtumishi wa Mungu.

Kuongea kama yeye Sio tu kuigiza kuhubiri kama


yeye bali ni kule ambako hauigizi

By Brother Paulo Evarist Koba 66


MWANANGU TIMOTHEO

Mathayo 26:73
Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea,
wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja
wao; kwa sababu hata usemi wako
wakutambulisha.

• Kufanya vitu ambavyo Huwa vinatokea kwa


mtumishi huyo.

2 Wafalme 2:14-15
[14]Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia,
akayapiga maji, akasema, Yuko wapi BWANA,
Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji,
yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
[15]Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko
wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya
inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye,
wakainama kifudifudi mbele yake.

By Brother Paulo Evarist Koba 67


MWANANGU TIMOTHEO

Walipomuona akipasua mto yordani kama elia


alivyokua anafanya basi wakajua kuwa ana upako
wa Elia.

• Kufanana nae aina ya Maisha hata nguo


mnazovaa na hata aina za kunyoa hufanana.

Luka 1:17,80
[17]Naye atatangulia mbele zake katika roho ya
Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba
iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye
haki, na kumwekea Bwana tayari watu
waliotengenezwa.
[80]Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni,
akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa
Israeli.

By Brother Paulo Evarist Koba 68


MWANANGU TIMOTHEO

Mathayo 3:4
[4]Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la
singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni
mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya
mwitu.

Maisha ya Elia yalifanana Kabisa na Maisha ya


Yohana mbatizaji mpaka uvaaji mpaka chakula
wanachokula.

Mfano nilikua napenda kunyoa vipara lakini siku


nilivyokutana na Mtumishi wa Mungu Peter
mahenge nikaanza kuvutiwa kufuga nywele, nikiwa
naenda kuhubiri huwa ninatembea kwa kujitanua
unajua hii niliipata wapi kwa Mchungaji wangu Paul
Israel Shaban.
Kuna Watu fulani walikosoa sana kuwa mimi ni
muongo siwezi kuwa na neema za watu wengi kiasi
hiko kwa sababu nitachanganikiwa niliwajibu ukikua
utaacha kuongea hivyo

By Brother Paulo Evarist Koba 69


MWANANGU TIMOTHEO

Sikia unaweza ukawa na upako wa Watu wengi


wengi lakini huo wote unakuja kuunda aina ya
utumishi utakaoubeba.

Luka 9:18-19
[18]Ikawa alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi
wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je!
Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?
[19]Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini
wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo
wa manabii wa kale amefufuka.
Watu walisema Yesu amefanana na Elia na kina
Yohana mbatizaji na hata manabii wa zamani kwa
sababu waliona madhihirisho ambayo yalikua kwa
hao watu yanapatikana kwa Yesu yaani waliona
neema za watu hao zikiwa kwa Yesu lakini ni kweli
kuwa hizo upako zilikua kwa Yesu lakini hizo upako
kwa pamoja ndo ziliunda utendaji wa Yesu na
madhihirisho yake ndio maana Petro akafunuliwa
kuwa huyu ni Mwana wa Mungu aliye hai aleluya!

By Brother Paulo Evarist Koba 70


MWANANGU TIMOTHEO

Mimi ni Matokeo ya neema(upako) ulio juu ya watu


wengi ambao wameyaathiri Maisha yangu iwe kwa
kukutana nao au bila kukutana nao mfano ni Baba
yangu wa kiroho Bishop Paul Israel Shaban,
mchungaji Peter mahenge, Bishop Gwajima, Pastor
benny hinn, Kenneth e hagin, Apostle arome osayi,
Apostle edu, michael koulinous, shepherd bushiri,
pastor serijo mkonda, Brother Enock Israel Nashon,
na Bishop Dickson kabigumila

By Brother Paulo Evarist Koba 71


MWANANGU TIMOTHEO

Vitabu vinginevyo vilivyoandikwa na mwandishi.


1. USICHOCHEE MAPENZI
2. KIJANA ALIYEOKOKA NDANI YA BABILONI
3. MAHALI PA SIRI PA MUNGU
4. UELEWE ULIMWENGU WA ROHO
5. USIMZIMISHE ROHO MTAKATIFU
6. SAFARI YA MTUMISHI WA MUNGU
7. RAFIKI YANGU ROHO MTAKATIFU
8. SIRI YA KUNENA KWA LUGHA
9. KUHUSU MALAIKA
10. SIRI YA MUZIKI
11. TUNDA LA ROHO
12. ROHO SABA ZA MUNGU
13. KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
14. MIMI NI MWANAMKE
15. NIPO SINGLE
16. KUTUMIKA CHINI YA MTUMISHI WA MUNGU
17. UPONYAJI WA MOYO ULIOUMIZWA
18. KUVUNJA MADHABAHU ZA UKOO
19. MWANAUME HALISI
20. MWANAMKE NA MAHUSIANO
21. SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI
22. WAHENGA WA IMANI-01
23. KIJANA MWENYE MGUSO.
24. USHINDI DHIDI YA PUNYETO.
25. UTAJIRI WA KUNENA KWA LUGHA.
26. MIKONO YA WALIONITANGULIA.
27. MAONO YA KIROHO.
28. UELEWE UPAKO
29. KWANINI UMTUMIKIE MUNGU KWA BIDII
30. NAMNA YA KUTUNZA UPAKO
31. NGUVU YA MANENO
32. TOENI PEPO
33. CHAKULA CHA MWAMINI
34. JE NIMKUBALIE ?
35. UKWASI WA NENO LA MUNGU
36. KWANINI SIUMWAGI
37. NINI KITATOKEA NIKIFARIKI
38. KUOKOKA NI NINI ?
39. HEKIMA ZA MAMA KUKU

By Brother Paulo Evarist Koba 72


MWANANGU TIMOTHEO

Kwa Mawasiliano Na Kujifunza Zaidi

Ikiwa umeguswa na ujumbe wa kitabu hiki, una swali,


una Maoni, ushauri, ushuhuda au unahitaji vitabu
vingine, Unaweza kuwasiliana moja kwa moja na
mwandishi;

PAULO EVARIST KOBA

Kupiga & meseji: +255 783 428 460, +255 673 428 461

Barua pepe: paulokoba395@gmail.com

Pia unaweza kupata mafundisho zaidi kutoka kwa


PAULO EVARIST KOBA kupitia;

Barua pepe: paulokoba395@gmail.com

Facebook: EVARIST KOBA

Instagram: paulo_evarist_koba12348

WhatsApp: +255 783 428 460

By Brother Paulo Evarist Koba 73


MWANANGU TIMOTHEO

Ungana nami Kuwahudumia Wengi

Shauku kuu ya mwandishi PAULO EVARIST KOBA ni


Kuona watu wengi wanafikiwa, wanabadilishwa na
Kuinuliwa kwa kweli iliyojengwa juu ya msingi wa
neno la Mungu.
Pia huwa ninatembea mashuleni na mavyuoni hivyo
basi kama kuna nafasi usisite kunitaatifu kama Roho
Mtakatifu atakusemesha mimi kuja hapo pia
unaweza kusapoti Katika ujenzi wa studio zetu ili
tuwe tunapost mafundisho hewani na kuwafikia
wengi zaidi na malengo kwa huu mwaka ni kuwaleta
kwa Yesu Watu Elfu kumi 10,000.
Hivyo Unaweza kuungana nami kuhakikisha Dunia
inajazwa maarifa ya Mungu nisaidie Ili yawe na
uhalisia kwa Maombi yako, mali yako, kutupa guess
za kuhudumia mashuleni, mavyuoni na hata
makanisani pia unaweza kusapoti kwa fedha yako
kwa ajili ya kutiwa nguvu na kwa ajili ya bando.
Ikiwa umeguswa kufanya chochote tafadhali tumia
vyanzo Vifuatavyo kufanya jambo na Mungu
atakubariki.
By Brother Paulo Evarist Koba 74
MWANANGU TIMOTHEO

Tigo Pesa: +255 673 428 461 (Philomena)


Airtel Money:+255 783 428 460 (Philomena )

Mungu akubariki kwa utoaji wako

By Brother Paulo Evarist Koba 75


MWANANGU TIMOTHEO

KUHUSU MWANDISHI
Naitwa Paulo Evarist Koba nimeokoka na nampenda sana YESU,
Muhitimu wa ngazi ya astashahada pale kwenye chuo cha
ufundi cha DIT.
Niliokoka Mwaka 2014 nikiwa kidato cha tatu huko shuleni
nilipokua nasoma elimu ya sekondari, tangu hapo Maisha
yangu yamebadilika kabisa.
Ninaabudu kanisa la Gilgal Revival Church pia ni mtoto wa
kiroho wa mchungaji Paulo Israel Shaban.
Haya maarifa nimejifunza Kupitia kwa Baba yangu wa kiroho
Askofu Paul Israel Shaban na watu kama Bishop Kabigumila, na
mchungaji Peter Mahenge, na Mwl Christopher Mwakasege.
Kama umeguswa na huduma hii na una ushuhuda kuhusu hiki
kitabu basi karibu kwa namba za hapo chini pia unaweza kutoa
sadaka Yako Ili kutoa sapoti karibu kwa mawasiliano ya hapo
chini pia kwa ushauri na msaada wa kiroho karibu sana kupitia
Email ifuatayo paulokoba395@gmail.com na mawasiliano ya
0783428460 au mitandao ya kijamii nitafute kama Evarist
Koba.

By Brother Paulo Evarist Koba 76

You might also like