KISWAHILI

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 9

Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

ELIMU YA KIADVENTISTA
SHULE YA SEKONDARI MBEYA ADVENTIST
MTIHANI WA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA KWANZA, 2024
KISWAHILI

MUDA: SAA 2:30 20 MEI, 2024

Maelekezo.

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10 ).


2. Jibu maswali yote katika sehemu ZOTE.
3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
4. Andika majina yako kamili katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) hadi (x), kasha andika herufi ya jibu hilo katika
jedwali linalofuata.
(i) Dhima kuu ya lugha katika mawasiliano ni ipi kati ya hizi zifuatazo?
A. Kutambulisha utamaduni D. Kuelimisha jamii
B. Kutunza historia E. Kuburudisha jamii
C. Kupashana habari
(ii) Aina ya neno inayotoa maelezo zaidi kuhusu kielezi huitwa
A. Kivumishi D. Kiwakilishi
B. Kielezi E. Kihisishi
C. Kitenzi
(iii) Kati ya sentensi zifuatazo ni ipi inakosa la kimuundo?
A. Juma anausa masiwa
B. Wangu motto anapenda kusoma
C. Mashirikiano kati ya Tanzania na Kenya yameimarika
D. Leo tutafua nguo zetu
E. Nilimkuta hayupo
(iv) Utanzu gani wa sarufi unajishughulisha na mfumo wa sauti katika lugha mahususi?
A. Sintaksia D. Pragmatiki
B. Fonolojia E. Mofoloji
C. Semantiki
(v) Kiwango cha nguvu kinachoambatanishwa na utamkaji wa silabi Fulani katika neon
huitwa
A. Kiimbo D. Shada
B. Lafudhi E. Lafudhi
C. Kidatu
(vi) Ipi ni seti sahihi ya vipengele vya umbo la nje la kazi ya fasihi?
A. Muundo, wahusika, falsafa
B. Wahusika, dhamira na matumiziyalugha
C. Mtindo, matumizi ya lugha na falsafa
D. Muundo, mandharinawahusika
E. Mandhari, wahusika na migogoro
(vii) Lugha ya Kiswahili ina aina ngapi za vitenzi?
A. Mbili C. Tano
B. Tatu D. Nne
Ukurasa wa 1 kati ya 9
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

E. Nane
(viii) Alama zinazotumiwa kuwakilisha sauti za lugha huitwa
A. Fonimu D. Herufi
B. Mofimu E. Alofoni
C. Vitamkwa
(ix) Nyenzo kuu ya fasihi ni
A. Fanani D. Mtindo
B. Hadhira E. Lugha
C. Wahusika
(x) Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana Zaidi yamoja?
A. Joni amempigia mpira
B. Nipe sahani ya kulia
C. Kaka amefua nguo
D. Eva amenunua kanga
E. Suedi amenunua mbuz

Ukurasa wa 2 kati ya 9
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

(i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) (viii) (ix) (x)

2. Oanisha maelezo yanayopatikana katika SAFU A na dhana zinazopatikana katika SAFU B


SAFU A SAFU B
(i) Hushughulikia jinsi neno linavyotamkwa A. Semantiki
(ii) Hushughulikia jinsi neno linavyoundwa B. Silabi
(iii) Huhusika na mpangilio wa sentensi katika C. Sauti
lugha D. Mofolojia
(iv) Hushughulikia maana za maneno katika lugha E. Fonolojia
(v) Sehemu ya neno inayotamkwa mara moja na F. Sintaksia
kwa pamoja kama fungu moja la sauti G. Kiimbo
H. Lugha
I. Mkazo

(i) (ii) (iii) (iv) (v)

Jibu maswali yote

3. Chagua jibu sahihi na iandike herufi ya jibu katika kisanduku ulichopewa mwisho wa swali
hili;

(i) Maneno haya ni aina gani za maneno; ubao, njaa, muziki, panzi, gwaride ni;

A. Kiwakilishi C. Nomino
B. Vihusishi D. Vitenzi

(ii) Lugha ni mfumo wa sauti za _______

A. Mawasiliano C. Nasibu
B. Fasihi D. Maumbo

(iii) Neno MWANANCHI lina silabi ngapi?

A. Mbili C. Nne
B. Moja D. Sita

(iv)Mkisi amekwenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama aina gani ya neno?

Ukurasa wa 3 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

A. Kiunganishi
B. Nomino
C. Kielezi
D. Vitenzi

(v) Aina ya neno inayofafanua zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi huitwa ___

A. Kielezi C. Kivumishi
B. Kihisishi D. Kitenzi

(vi)Kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo?


A. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti
B. Kupanda na kushuka kwa sauti
C. Kuzungumza na kushusha mawimbi ya sauti
D. Kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti.
(vii) Wageni wetu walikaribishwa vizuri sana. Neno sana ni aina gani ya neno?

A. Kielezi C. Nomino
B. Kivumishi D. Kiwakilishi

(viii) Dhima kuu ya lugha katika mawasiliano ni ipi kati ya hizi;


A. Kupashana habari
B. Kuburudisha jamii
C. Kutambulisha utamaduni
D. Kutunza historia
(ix)Mawasiliano huweza kufanyika kwa njia ya ishara, maandishi na ……………….
A. Kuangalia C. Misemo
B. Mdomo D. Masomo
(x) Milio ya ndege, wanyama na viumbe wengine sio lugha kwa sababu?
A. Huleta maana tofauti
B. Haileti au haitoi maana
C. Huvutia watu
D. Hutumiwa na viumbe na sio watu. .
i ii iii Iv v Vi vii Viii Ix x

4. Oanisha sentensi zenye matumizi ya vivumishi katika Orodha A na aina ya kivumishi husika
kutoka Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.
FUNGU A FUNGU B

Ukurasa wa 4 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

i) Walimu wetu walileta kitabu darasani A. Kivumishi cha sifa


ii) Wanafunzi wale wanafanya mazoezi B. Kivumishi cha kuuliza
darasani C. Kivumishi cha idadi
iii) Wanakijiji wangapi wanapiga kura? D. Kivumishi cha jina
iv) Watoto watatu wamesimulia hadithi E. Kivumishi kimilikishi
F. Kivumishi kioneshi
v) Askari hodari amemkamata mwizi

FUNGU A I Ii iii Iv v

FUNGU B

5. (a) Bainisha miundo ya silabi zilizopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:


(i) Watakapokunywa________________________________________________
(ii) Uzalendo_______________________________________________________
(iii) Maendeleo______________________________________________________
(iv) Chakula________________________________________________________
(v) Ng’ombe_______________________________________________________
(vi) Ukweli_________________________________________________________
(vii) Skrubu_________________________________________________________
(b)Eleza sababu tatu zinazofanya lugha kuwa sauti za nasibu.
(i) _______________________________________________________________
(ii) _______________________________________________________________
(c) lugha ya Kiswahili hutamkwa kwa utaratibu wa kufuata silabi. Tenganisha silabi katika
maneno yafuatayo; mfano, lala-$la$la$, baba-$ba$ba$

(i) Shusha ……………………………………………………………..


(ii) Ua ………………………………………………………………………..
(iii) Gharama ………………………………………………………………………..
(iv) Mpiganaji ………………………………………………………………………..
(v) Vilevile ………………………………………………………………………..
(vi) Shangwe …………………………………………………………………………..
(vii) Sukukuu…………………………………………………………………………..
(viii) Kinanda…………………………………………………………………………..
(ix) kiswahili…………………………………………………………………………..

Ukurasa wa 5 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

6. Scola ni mwanafunzi mgeni katika darasa lako la kidato cha kwanza , kila mara huchanganya
sana maneno wakati wa kuainisha. Msaidie Scola kubainisha aina za maneno yaliyopigiwa
mstari katika sentensi zifuatazo.

Mfano: Asha anapenda kusali.


Asha ni nomino
a. Wewe umepata zawadi nzuri.
__________________________________________________________________
b. Kilimanjaro ni mlima mrefu.
__________________________________________________________________
c. Baba amekwenda shambani.
__________________________________________________________________
d. Mwalimu mpole anafundisha kwa ustarabu darasani.
__________________________________________________________________
e. Lo! Umechelewa , mwalimu ameondoka.
__________________________________________________________________
f. Kalamu zipi haziandiki?
__________________________________________________________________
g. Yeye ni mpole sana ijapokuwa anaongea sana ukimkosea.
__________________________________________________________________
h. Maua ni bibi yangu mrembo .
__________________________________________________________________
i. Mwanana alikuwa anataka kula ugali kiholela.
__________________________________________________________________
j. Wazuri hawajiuzi mtaani.
__________________________________________________________________

7. (a) Panga majina yafuatayo kwa mtiririko unaotakiwa;


i. Zawadi
ii. Juma
iii. Annarose
iv. Matayo
v. Kalamu
(b) Andika kwa mpangilio mzuri kialfabeti
i. .....................................................................
ii. .....................................................................
iii. .....................................................................
iv. .....................................................................
v. ....................................................................

Ukurasa wa 6 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

8. (a) Pigia msitari vivumishi katika maneno yafuatayo;


i. Mtu huyu anaimba vizuri
ii. Wale wanacheza mpira mzuri
iii. Yeye ni mchawi katika kijiji hiki
iv. Wale wa shangazi wamefaulu
(b) Taja aina za vitenzi
i. .........................................................................
ii. .........................................................................
iii. ...........................................................................
(c) Tunga sentensi kwa kutumia
N+T
W +V + T + E
T

9. (a) Taja maneno ya msingi matano (05) yanayopatikana katika maana ya


lugha
(i)
……………………………………………………………………………………..

(ii)
…………………………………………………………………………………….

(iii)
……………………………………………………………………………………

(iv)
……………………………………………………………………………………

(v)…………………………………………………………………………………
(b) Fafanua matumizi ya ishara zifuatazo kwa binadamu huwa na maana ipi kwa kadri ishara
hizi zitumikavyo.

I. Kutikisa kichwa kwa kupandisha juu na kushusha chini maana yake ni


____________________________________________________________
II. Kuinua juu na kushusha chini mabega
____________________________________________________________

(c) Kwa kuzingatia lafudhi na matamshi sahihi bainisha maneno yenye makosa katika
sentensi zifuatazo.
i. Ntoto wangu anaumwa……………………………………………
ii. Nimepata ujumbe wenye taharifa mbaya………………………………………………….
iii. Kurara badara ya kutafuta kazi kufanya kunasababisha umaskini…………………………

Ukurasa wa 7 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

iv. Ama kweri erimu haina mwisho…………………………………………………


v. Rafiki yangu naja………………………………………
Andika upya sentensi hizo kwa kusahihisha makosa uliyoyabaini
i. …………………………………………………………………………………………..
ii. ……………………………………………………………………………………………
iii. …………………………………………………………………………………………….
iv. ……………………………………………………………………………………………
v. ……………………………………………………………………………………………
10. (a) Sijuti wala sidanganyiki hii ni misemo ambayo hutumiwa na watoto wawili ambao ni
fasihi simulizi na fasihi andishi .Onesha tofauti tano(5) za fasihi simulizi na fasihi andishi ili
misemo yao ikubalike.

FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI

(i)

(ii)

(iii)

(iv)

(v)

(b) Orodhesha vipengele ya FANI na MAUDHUI

FANI MAUDHUI

Ukurasa wa 8 kati ya 6
Jina la Mwanafunzi: _________________________________________

Ukurasa wa 9 kati ya 6

You might also like