Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 12

MADA YA UONGOZI, UAMINIFU, UADILIFU NA UZALENDO NA STADI ZA

MAISHA

1. UONGOZI.
Uongozi ni mfumo wa kiutawala unaotoa fursa kwa Mtu au kikundi kidogo cha Watu
kuwatawala walio wengi katika Jamii,Taasisi,Jumuiya na hata katika vikundi vya
kijamii .Uongozi katika mfumo wa Maisha unaweza ukawa wa kidemokrasia,Udikiteta au
uongozi wa kichifu.Uongozi wa kidemokrasia unatoa fursa kwa wanachi kuchagua
viongozi/uongozi kwa kupiga kura za siri au za wazi baada ya wahusika wanaotaka
kugombea nafasi kuweka nia , kugombea na kuchaguliwa na wananchi.Aidha uongozi
wa kidikteta niwa mabavu,unyanyasaji ambao haukubaliki kwa jamii.Nchi ya Tanzani
uongozi wake niwa kidemokrasia ambapo Rais,Wabunge na Madiwani uchaguliwa kila
baada ya miaka Mitano.

WAJIBU WA KIONGOZI

Wajibu wa Kila kiongozi wa Serikali wa kuchaguliwa katika ngazi ya Jamii, Kitongoji,


Kijiji, Kata na Taifa ni pamoja na:

i. Kutambua na kuzingatia kuwa anao wajibu wa kuwahudumia wananchi na


siyo kuwa chanzo cha migogoro kwa jamii
ii. Kuhakikisha kuwa shughuli za Serikali zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu na hivyo Wananchi wanategemea kupata msaada wa tafsiri
sahihi ya Sheria katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku
iii. Kusimamia ulinzi na usalama wa Watu na Mali zao
iv. Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutolewa taarifa kwa ngazi
zote
v. Kusikiliza kero za jamii na kuzitafutia ufumbuzi wa muda muafaka
vi. Kusimamia utekelezaji wa Sera za Nchi kwa vitendo na kupima matokeo ya
utekelezaji
SIFA ZA KIONGOZI BORA

i. Awe mwezeshaji anayetumia mbinu za upangaji wa mipango shirikishi


ii. Ili kuwa na utawala bora ni lazima kuwa na viongozi bora, Kiongozi bora
anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
iii. Awe na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu bila
upendeleo wa aina yeyote
iv. Anahakikisha kwamba huduma zinatolewa kwa haki na usawa bila kujali imani na
itikadi za watu katika eneo lake,
v. Anashiriki kwa ukamilifu katika harakati za kuondoa umasikini na kupiga vita
rushwa
vi. Anahakikisha kuwa uongozi na utawala katika jamii, kitongoji, au Mtaa wake
unalingana na misingi ya Utawala bora

2. MAADILI KATIKA JAMII


Maadili maana yake uwepo wai misingi, kanuni na taratibu zinazoainisha tabia na
mienendo inayokubalika na isiyokubalika kwa Viongozi wa Umma na jamii nzima.
Misingi, kanuni na taratibu hizi zinatumika kuongoza mahusiano kati ya Viongozi wa
Umma, Watumishi wa Umma, Bodi mbalimbali za Kitaaluma, Vyombo vya Habari,
Wadau, Makundi mengine ya wananchi katika jamii na namna wanavyofanya mambo
yao kwa kuzingatia misingi ya utu na haki. Kwa jumla misingi, kanuni na taratibu hizi
zinawataka jamii na Viongozi wa Umma kufanya kilicho sahihi ikiwa ni pamoja na
kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi, uwajibikaji na uwazi.

1.2 Misingi ya Maadili ya kwa jamii na Viongozi wa Umma inahusisha yafuatayo:-

i. Kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kujali;


ii. Kujizuia na tamaa na kujiheshimu;
iii. Kujituma na kutekeleza majukumu kwa umahiri kufuatana na misingi ya
kitaaluma;
iv. Kufanya kazi bila upendeleo;
v. Kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni;
vi. Kuepuka Mgongano wa Masilahi;
vii. Kuepuka kupokea zawadi, fadhila au Masilahi ya kiuchumi yaliyokatazwa;
viii. Kutotoa, Kutopokea au kuomba rushwa; ix) Kutotumia mali ya umma kwa
Masilahi binafsi;
ix. Kuepuka matumizi mabaya ya madaraka;
x. Matumizi sahihi ya taarifa za umma; na
xi. Uwajibikaji na kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

Maana ya Ukiukwaji wa Maadili kwa jamii na Viongozi wa Umma; Ukiukwaji wa Maadili


ni kutenda jambo au kutekeleza majukumu ya umma kinyume na tamaduni za jamii
zinazokubalika, Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma au kushindwa kutenda jambo
linalotakiwa kwa mujibu wa Sheria. Ukiukwaji wa maadili ya jamii na Viongozi wa
Umma ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka; matumizi mabaya ya taarifa za
Serikali; vitendo vya rushwa; mgongano wa masilahi; kushindwa kutoa Tamko la
Rasilimali na Madeni; kutoa tamko la uongo la Rasilimali na Madeni; unyanyasaji wa
kijinsia; kuomba, kupokea, kushawishi na kujipatia Masilahi ya kifedha yasiyostahili;
kujipatia Masilahi ya kiuchumi yasiyostahili; kuingia mkataba na Serikali bila kutamka
Masilahi kwenye mkataba huo; na matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano.

Vipengele vya ukiukwaji wa maadili vinaelezewa kwa ufupi kama ifuatavyo:-

i. Matumizi Mabaya ya Madaraka Kiongozi wa Umma kutumia cheo, wadhifa na


madaraka yake kuweka shinikizo katika kuteua, kuthibitisha, kupandisha cheo
mtumishi, kuajiri, kuchukua hatua za kinidhamu, kutumia Rasilimali za Umma
kwa manufaa binafsi na kufanya maamuzi kinyume na Sera, Sheria, Kanuni na
Miongozo mbalimbali.
ii. Matumizi Mabaya ya Taarifa za Umma Kiongozi wa Umma kutoa taarifa za
Serikali za siri au za kawaida bila kufuata utaratibu kwa mtu ama watu wasio
husika ambazo anazitunza au amezipokea kwa kuaminiwa kutokana na madaraka
aliyonayo na kujinufaisha binafsi au vinginevyo na taarifa alizozipata wakati wa
kutekeleza majukumu ya Serikali.
iii. Unyanyasaji wa Kijinsia Matendo ya unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na
kushawishi, kulazimisha mahusiano ya kimapenzi au upendeleo wa kimapenzi na
mtu yeyote; vitendo vya kubaka; kunajisi au shambulio lolote la aibu; lugha ya
matusi na kudhalilisha.
iv. Vitendo Vya Rushwa Vitendo vya rushwa ni pamoja na kushawishi, kuahidi,
kusaidia, kujaribu kudai, au kuomba, au kupokea au kutoa mapato yasiyo halali
kwa nia ya kushawishi na kujipatia manufaa binafsi wakati wa kutekeleza
majukumu ya umma. Pia, vitendo vya rushwa vinahusisha kumdanganya mwajiri
kwa kutumia nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka, kutumia mali ya umma
kwa manufaa binafsi, upendeleo, kuhamisha mali iliyopatikana kwa njia ya
rushwa, matumizi mabaya ya mali ya umma na rushwa ya ngono.
v. Kushindwa Kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni Kiongozi wa Umma kushindwa
kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni yake, mwenza wake pamoja na watoto
wake walio na umri usiozidi miaka 18 ambao hawajaoa au kuolewa katika kipindi
cha siku thelathini baada ya kuajiriwa au kuteuliwa au kuchaguliwa na mwisho
wa kutumikia wadhifa bila sababu za msingi. Hii pia itahusisha Kiongozi wa
Umma kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni baada ya tarehe 31 Desemba kila
mwaka.
vi. Kutoa Tamko la Uongo la Rasilimali na Madeni Kiongozi wa Umma kutoa Tamko
la Rasilimali na Madeni la uongo ikiwa ni pamoja na kutoa Taarifa zisizo sahihi au
pungufu kuhusu Rasilimali na Madeni yake mwenyewe, mwenza wake pamoja na
watoto walio na umri usiozidi miaka 18 ambao hawajaoa au kuolewa.
vii. Kuomba, Kupokea, Kushawishi na Kujipatia Masilahi ya Kifedha yasiyostahili Hii
inahusisha Kiongozi wa Umma kuomba, kupokea au kushawishi kujipatia Masilahi
ya kifedha yasiyostahili.
viii.Kujipatia Manufaa ya Kiuchumi yasiyostahili Hii inahusisha Kiongozi wa Umma
kujipatia manufaa ya kifedha au mali isiyostahili au kumsaidia mtu mwingine
kupata manufaa ya kifedha au mali isiyostahili.
ix. Kuingia Mkataba na Serikali na Kutotamka Masilahi Binafsi Kwenye Mkataba huo
Hii inahusisha Kiongozi wa Umma kuingia mkataba na Serikali na kutotamka
Masilahi binafsi aliyonayo kwenye Mkataba huo. Masilahi binafsi kwenye mkataba
yanaweza kuwa ni ya moja kwa moja au vinginevyo.
x. Matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Hii inahusisha Kiongozi
wa Umma kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa namna ambayo anakiuka maadili ya Viongozi wa Umma.
ATHARI ZA UKIUKWAJI WA MAADILI

Athari za Ukiukwaji wa Maadili Zipo athari nyingi za ukiukwaji wa Maadili ya uongozi,


miongoni mwa athari hizo ni:-

i. Rasilimali za nchi kunufaisha wachache;


ii. Wananchi kukosa haki zao za msingi kutokana na rushwa na upendeleo;
iii. Taasisi za Umma kufanya kazi bila ufanisi;
iv. Viongozi wa Umma kujilimbikizia mali isivyostahili bila kujali hali za wananchi
wanaowaongoza;
v. Tofauti ya kipato kati ya walio nacho na wasio nacho na kukithiri kwa umasikini
miongoni mwa wananchi;
vi. Kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali;
vii. Kuongezeka kwa gharama za kuendesha shughuli za biashara, kiuchumi na
kijamii;
viii. Kupungua kwa kasi ya uwekezaji; ix) Kudhoofika kwa uchumi wa nchi;
ix. Wananchi kutotii sheria za nchi na hivyo kuhatarisha usalama na amani ya nchi;
na
x. Wananchi kukosa imani na Serikali yao.

NJIA ZA KUDHIBITI UKIUKWAJI WA MAADILI

2.3 Njia za Kudhibiti Ukiukwaji wa Maadili Njia zifuatazo zinaweza kutumika kudhibiti
ukiukwaji wa maadili:-

i. Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya maadili;


ii. Kuwepo mifumo madhubuti na taratibu za kuwalinda watoa taarifa juu ya
ukiukwaji wa maadili;
iii. Kuanzisha na kuimarisha miundombinu ya kimaadili kama vile kutenga bajeti kwa
ajili ya mafunzo na utekelezaji wa shughuli za maadili, kuimarisha utendaji wa
Kamati za Maadili na mifumo ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya
maadili;
iv. Mamlaka za nidhamu kutekeleza wajibu wao wa kusimamia watumishi walio chini
yao;
v. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu katika Sekta ya Umma,
Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia;
vi. Kuanzisha na kuimarisha dawati la malalamiko katika Wizara, Idara
zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za
Mitaa, Mashirika ya Umma na Taasisi nyingine za Umma;
vii. Kujumuisha masuala ya maadili katika tathmini za utendaji kazi za Watumishi wa
Umma;
viii. Kushirikisha watumishi katika masuala mbalimbali yanayowahusu kupitia mbinu
mbalimbali za ushirikishwaji;
ix. Kuanzisha mitaala ya maadili katika ngazi zote za elimu na mafunzo;
x. Kuwa na midahalo na mijadala kuhusu vihatarishi vya kimaadili na jinsi ya
kuvidhibiti; na
xi. Kuweka taratibu bayana za kuzuia na kudhibiti ucheleweshaji wa maamuzi.

HATUA ZINAZOWEZA KUCHUKULIWA KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA MAADILI

Hatua zinazoweza Kuchukuliwa Kutokana na Ukiukwaji wa Maadili ya Viongozi wa


Umma Kiongozi wa Umma anayekiuka Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma
anaweza kuchukuliwa hatua zifuatazo:-

i. Kutakiwa kutoa maelezo kuhusu mwenendo wake;


ii. Kufanyiwa uchunguzi wa awali na wa kina;
iii. Kufikishwa mbele ya Baraza la Maadili;
iv. Kuonywa na kupewa tahadhari;
v. Kushushwa cheo;
vi. Kusimamishwa kazi;
vii. Kufukuzwa kazi;
viii. Kutozwa faini;
ix. Kutakiwa kujiuzulu wadhifa alionao; na
x. Kupewa adhabu au kuchukuliwa hatua nyingine kwa mujibu wa sheria za nchi.

3. MAANA YA UZALENDO KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YETU

Uzalendo ni hali ya mtu kuwa na moyo wa kuipenda nchi yake, kulinda raslimali za
Taifa, kuenzi Tunu za Taifa (Utu, Amani, Mshikamano na Umoja), kuwajibika, kuwa
mwadilifu, kufanya kazi kwa bidii na kutetea maslahi ya Taifa kwa gharama yeyote.
Maendeleo ya Taifa lolote duniani yanategemea zaidi namna wananchi walivyo tayari
kujitolea kwa ajili ya Taifa lao na kushiriki kikamilfu katika mchakato wa kujiletea
maendeleo yao wenyewe, ikiwa ni pamoja na kujinasibisha na utekelezaji wa shughuli
za Serikali kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa, pamoja na kuunga mkono juhudi za
Serikali yao kuwajengea mazingira wezeshi ya kujiletea maendelo endelevu. Aidha,
Uzalendo unaanza kwa kutambua utu na asili ya utu ambavyo vimebebwa na Tunu za
Taifa zinazo tambulisha taifa na utaifa wa watu wake.

1.1 Maana ya Tunu za Taifa

Kwa tafsiri ya kawaida, tunu ni kitu adhimu, ni kitu cha pekee na pia ni utambulisho.
Tunu za Taifa ni masuala ya msingi ambayo hulitambulisha Taifa na utaifa wa watu
wake. Aidha, utendaji kinyume na tunu hizo hupelekea nchi kuingia matatani. Hivyo,
masuala yamustakabali wa nchi na ustawi na ufanisi wa watu wake hutawaliwa na
mfumo ambao sehemu zake ndizo TUNU za Taifa husika na viongozi wa juu katika
utawala wa nchi ndio wasimamizi na walinzi wakuu wa tunu za nchi yao. Hivyo viongozi
na wananchi wakizitambua, wakaziheshimu na kuwajibika ipasavyo katika kulinda tunu
za nchi, huingia katika daraja la uzalendo.

Kwa muktadha huu, Tunu za Taifa letu zinajumuisha masuala yafuatayo;-

i. Lugha yetu ya Kiswahili,


ii. Upendo, uwajibikaji, uzalendo, utu na udugu,
iii. Amani, utulivu, kuheshimiana na kuvumiliana,
iv. Umoja na mshikamano wetu,
v. Wimbo wa Taifa na Bendera ya Taifa,
vi. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar,
vii. Haki za kibinadamu na usawa wa kijinsia
Hata hivyo kwa miaka ya hivi karibuni Tunu hizi zimeonekana kupotea miongoni mwa
jamii yetu hivyo ipo haja ya kujenga moyo wa uzalendo ili kufufua, kuendeleza na
kurithisha tunu hizi kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

1.2 Mzalendo ni nani;


Mzalendo ni mtu yeyote anayeishi katika nchi fulani na kufuata sheria za nchi na
analinda na kuviheshimu vitu vya nchi yake. Aidha, ili mtu atambulike kama mzalendo
inabidi awe na sifa zifuatazo:-
i. Kuzaliwa nchini na angalau mzazi mmoja au wote wawili wawe ni wazawa;
ii. Kuona fahari yeye kuzaliwa nchini bila kuona aibu wala haya;
iii. Ni lazima awe mwaminifu wa kulipa kodi, kutoibia nchi kwa njia yeyote;
iv. Kutokuwa mharibifu au mvujaji wa mali na rasilimali za nchi;
v. Kuwapenda watu wote, hata viongozi wanaoijenga nchi bila kujali aina ya chama,
udini, ukabila wala rangi yake;
vi. Kuwapinga kwa nguvu zote raia wote wanaobomoa na kuharibu nchi hata kama
ni wa chama chake, dini yake, kabila lake, rangi yake au ndugu na jamaa zake;
vii. Kusaidiana na viongozi wake kuijenga nchi bila kujali chama, dini, kabila wala
rangi yake;
viii. Kuweka juhudi kubwa katika kuisema na kuitangaza nchi yake vizuri ndani na nje
ya mipaka yake;
ix. Kupenda vitu vinavyoihusu au kutoka au kutengenezwa nchini mwake kama
lugha, utamaduni, vyakula, bidhaa za viwanda, timu za michezo, wana michezo
wake, na kila kitu kizuri kinachotokana na nchi yake; na

x. Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu,


majirani na marafiki kuwa wazalendo kwa kuipenda na kujitoa kwa ajili ya nchi
yao.

1.0 Hali Halisi ya Uzalendo Nchini

Dhana ya uimarishaji Uzalendo hapa nchini ilianza tangu miaka ya 1960 ambapo
jitihada mbalimbali zilifanyika ikiwa ni pamoja na: Maandalizi na utekelezaji wa falsafa
na sera kama vile Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha ambazo
zilikuwa na lengo la kuimarisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano miongoni
mwa wananchi wa Tanzania licha ya tofauti zao za asili, maeneo wanayotoka, rangi,
kabila na dini. Aidha, jitihada nyingine ni:- kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa;
Chuo cha Kivukoni kilichofundisha na kuzalisha Makada wa Siasa ya Ujamaa na
Kujitegemea, kufundishwa kwa somo la uraia katika Shule za Msingi na Sekondari na
Somo la Elimu ya Maendeleo (Development Studies) katika Vyuo Vikuu.
Hata hivyo, pamoja na jitihada hizo historia inaonesha kuwa, tangu miaka ya 1990 hadi
sasa, hali ya uzalendo hapa nchini imedorora. Hii inadhihirika kutokana na: Uwepo wa
baadhi ya Watanzania wanaokwepa kulipa kodi,Ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya
Watanzania; Kukithiri kwa vitendo vya rushwa, baadhi ya Watanzania wanao saliti Taifa
letu kiuchumi na kisiasa, ubadhirifu wa mali za Umma ikiwemo utakatishaji wa fedha;
Baadhi ya Watanzania kutotunza siri za nchi; Ubinafsi na kutumia madaraka ya Umma
kwa maslahi binafsi kwa baadhi ya watu wanaopewa dhamana ya kuongoza; Baadhi ya
Watanzania kudharau maadili ya Taifa letu; Kuanza kujitokeza kwa vikundi katika jamii
vyenye viashiria vya misimamo mikali ya kupinga jitihada za serikali za kuwaletea
wananchi wao maendeleo

2.1 Lengo kuu la kukuza Uzalendo


Ni kukuza moyo wa uzalendo na mapenzi ya Watanzania kwa nchi yao, ili washiriki
katika ujenzi wa taifa lao. Moyo wa uzalendo utawawezesha wananchi kuipenda nchi
yao, kulinda rasilimali za nchi, kuwajibika, kuwa waadilifu, kutunza siri za nchi na
kutetea maslahi ya Taifa.
2.2 Walengwa katika kukuza moyo wa Uzalendo
Walengwa wa uzalendo ni pamoja na;-
i. Wanasiasa;
ii. Wafanyabiashara;
iii. Taasisi za Umma na Binafsi;
iv. Watu Mashuhuri katika jamii
v. Viongozi wa Asasi za Kiraia (Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali na Taasisi za
Dini);
vi. Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vii. Watoto; Vijana;
viii. Watumishi wa Umma;
ix. Wazazi/walezi;
x. Walimu;
xi. Wizara mbalimbali za Kisekta (Watunga Sera na Miongozo ya Kisekta);
xii. Watanzania wenye ufuasi mkubwa miongoni mwa jamii (Celebrities);
xiii. Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii na jamii yote kwa ujumla.

2.3 Matokeo yanayotarajiwa kwenye Ukuzaji wa Moyo wa Uzalendo


Moyo wa uzalendo ukikuzwa na kuendelezwa, matokeo yafuatayo yatapatikana;-
i. Kuwepo kwa Taifa lenye uelewa wa pamoja kuhusu dhana ya uzalendo,
umuhimu wa Utaifa na mshikamano wetu;
ii. Uwepo wa makundi mbalimbali ndani ya jamii hasa vijana kuipenda nchi yao,
historia na urithi wao, utamaduni wao na kuyaishi maadili ya nchi yao;
iii. Uwepo wa vijana wanaotumia fursa mbalimbali zilizopo kujikwamua kiuchumi;
iv. Uwepo wa vijana wanaowajibika kwa kujitolea na kufanya kazi kwa bidii na
kibunifu zaidi;
v. Uwepo kwa tungo nyingi za nyimbo za kizalendo;
vi. Ulinzi wa Tunu za Taifa;
vii. Kuwepo kwa mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza uzalendo
nchini;
viii. Kupungua kwa matukio ya upokeaji na utoaji Rushwa na ukwepaji wa kodi
ambapo rasilimali zinazopatikana zinatumika kuboresha huduma za jamii;
ix. Uwepo wa Hati safi kwa Taasisi za Umma kutokana na taarifa za Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali;
x. Kuongezeka kwa maadili mema miongoni mwa wanajamii;
xi. Utayari wa wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika
nchi yao;
xii. Utayari wa wananchi kujitoa katika ulinzi na usalama kwa ajili ya kuilinda nchi
yao; na
xiii. Wananchi kuwa na ari ya kudhamini na kutunza mali na miundombinu ya nchi.

4.0 Hitimisho

Kwa kuzingatia mustakabali wa ajenda ya ujenzi wa Taifa, suala la kukuza moyo wa


uzalendo kwa raia wote ni jambo la msingi katika kuleta umoja wa kitaifa na
mshikamano ndani ya jamii. Uzalendo unapaswa kuonekana katika Utu wetu, Uadilifu;
Umoja; Uwazi; Uwajibikaji;
Hivyo, ili kukuza moyo wa Uzalendo nchini wadau mbalimbali watahusika kulingana na
mahitaji ya wakati husika ili kufikia azma ya kujenga taifa lenye mshikamano miongoni
mwa raia wake. Aidha, tunalo jukumu la kuiendeleza na kuilinda nchi yetu kupitia
uzalendo uliotukuka na wenye kujipambanua wazi wazi kila wakati, hususan kwenye
masuala ya mustakabali na ustawi wa nchi yetu.

4. STADI ZA MAISHA KATIKA KUJENGA TAIFA LINALOENDELEA


Stadi za maisha ni maarifa yanayotarajiwa kumsaidia mtu kuishi vyema

Maisha ni muambatano wa muda pamoja na matukio, hivyo ni muhimu kufahamu kuwa


muda unavyozidi kwenda ndipo kiumbehai kinapopata nafasi ya kupita katika matukio
mbalimbali yaliyo mazuri na mabaya, amayo yote huhitaji hekima na maarifa katika
kuyapitia hususan yaliyo mabaya.

Kuna msemo wa lugha ya Kiswahili unaosema kuwa "Kuishi kwingi ni kuona mengi":
maana halisi ni kuwa mtu aliyemtangulia mwenzake kiumri anakuwa na uzoefu mkubwa
sana kwa sababu mambo ambayo amekwisha kuyaona ni mengi katika kuishi kwake.
Kupitia uzoefu huo ndivyo mtu huyo anapata mbinu nyingi za kumwezesha yeye
kukabiliana na nyakati zote katika maisha yake.
Haina maana ya kwamba mtu mwenye umri mdogo, kwa sababu ya kuwa na uzoefu
mdogo wa kimaisha, basi anapaswa kukosa busara na hekima za kumwezesha yeye
kuishi vizuri.
Mtoto au kijana anaweza kuwa na hekima kama ya mzee kwa kujifunza stadi za maisha
ambazo ni kama zifuatazo

1. Stadi binafsi
2. Stadi za kijamii
3. Stadi za maamuzi sahihi[3]
Stadi binafsi
Hizi ni mbinu au kanuni ambazo zinamwezesha mhusika kuwa na uwezo mkubwa wa
kujitambua, kwanza kiundani zaidi, kwa maana ya hisia, uwezo, madhaifu na nafasi
yake katika jamii. Stadi binafsi ni muhimU sana kwa sababu zinamwezesha mhusika
huyo kujijengea hali ya kujiamini kutokana na kuitambua thamani yake katika jamii
inayomzunguka.
Ili kuwa bora katika stadi binafsi mhusika anapaswa kuwa na uwezo katika vitu
vifuatavyo: kujitambua, kutambua mahitaji na kuweka malengo katika maisha.
Stadi za kijamii
Hizi ni stadi ambazo humjenga na kumwezesha mhusika kujua naamna ya kuishi na
watu kwa upendo na amani na kujenga ushirikiano ulio bora. Vifuatavyo ni vipengele
muhimu ambavyo vinamthibitisha mtu kuwa stadi za kijamii:

1. uwezo wa kujenga mahusiano mazuri na watu wanaomzunguka


2. uwezo wa kujitawala kifikra na kuepuka misukumo hasi
3. uwezo wa kutambua na kujihusisha katika kusaidia changamoto za wanajamii
4. mawasiliano mazuri
Stadi za maamuzi sahihi
Hizi ni stadi ambazo zinamwezesha mhusika kufanya maamuzi sahihi wakati wa
changamoto na yanapotokea machaguo mengi. Kama ilivyo katika stadi nyingine hizi
pia zina kanuni ambazo ndizo msingi wa kupatikana kwa maamuzi sahihi, nazo ni kama
ifuatavyo.

1. mawazo chanya
2. ubunifu wa kimawazo
3. maono ya mbeleni
4. uwezo wa kufanya maamuzi
Vyanzo vya stadi za maisha
Watu hujifunza/kuiga stadi za maisha katika sehemu, makundi au watu mbalimbali ila
sehemu au vitu ambavyo ndio msingi wa stadi za maisha ni hizi zifuatazo.
Familia zetu
Hapa tunajifunza na kuiga vitu kutoka kwa wazazi au ndugu zetu kwa sababu tunaishi
nao kwa muda mreefu, hususani katika kipindi cha ukuaji wetu ambacho ndicho
kipindi vichwa vyetu vinapodaka na kukariri mambo mengi
Taasisi za kielimu
Hapa mara nyingi ni kupitia maarifa tunayopata kwa kufundishwa
na wakufunzi hususadi shuleni, vyuoni na kadhalika.
Jamii zetu
Tofauti na familia kuna kundi jingine kubwa ambalo linatuzunguka, hivyo lenyewe pia
lina mchango katika kutujenga kifikra na kuendeleza stadi zetu za kimaisha.
Imani/Dini
Imani tofautitofauti zimekuwa zikitoa mafunzo mengi ya kidini ambayo yamekuwa
yakihusika katika kuwajenga waumini wake. Kwa mfano imani ya Kikristo imekuwa
ikifundisha juu ya amri kuu ya upendo, kitu ambacho ni stadi muhimu inayowezesha
mtu kuishi vizuri na watu katika jamii yake.

You might also like