Professional Documents
Culture Documents
MAWASILIANO NA LUGHA
MAWASILIANO NA LUGHA
SARUFI YA KISWAHILI
Sifa za lugha
1) Lugha inahusisha sauti - kwa sababu lugha huhusisha sauti, huwa na uwezo
wa kutoa sauti.
2) Lugha ni kigezo kikuu cha mawasiliano hata ingawa hii sio njia tu pekee ya
kuwasiliana. Kuna nyingine nyingi- mavazi, sauti, ishara, mgusano na mtagusano
n.k
3) Lugha inahusisha sifa za unasibu
4) Lugha ni mali ya binadamu (wanyama hawana lugha )
5) Lugha inafuata taratibu fulani : sauti nasibu zenye kubeba maana
6) Lugha huhusisha shughuli ya kijamii
7) Watu hujifundisha lugha japo huzaliwa na uwezo wa kujifunza lugha
8) Lugha hukubalika kwa sababu ni kiungo hai
Mfano; msichana - Dem, Manyanga, Mbusi
Viambishi / mofu
Mofu au kiambishi nmi kipashio kidogo zaidi cha neno kilicho na maana ya kisarufi na
ambacho huambisha kwenye mzizi wa neno ili kuleta maana ikusudiwayo.
Mofu haiwezi kukatwakatwa zaidi kwani ikifanyiwa hivyo hupoteza maana.
Neno la lugha ya Kiswahili likiwa kamili huitwa leksimu
Leksimu ndio hubeba maana kuu na ndio hufasirika katika ubongo wa mzungumzaji
wa lugha husika .
Umilisi wa lugha haswa wa mzawa/mzaliwa wa lugha husika. Huielewi kutokana na
kufahamu maana yake kiisimu.
Leksimu hubeba mzizi na kiishio cha neno lenye maana kuu na ndio tunapata kwenye
kamusi za lugha husika kwa mfano; lima ni leksimu iliyojegwa na mzizi Lim na kisha a
Lim - a
1
cheka (Leksimu) (chek - a)
mzizi kiishio
Mzizi ni sehemu ya leksimu ambayo hubeba maana yake kuuu na sehemu hii
haibadiliki katu hata leksimu hiyo ikipanuliwaje .
Maneno yenye asili ya kibantu huishia /huchukua kiishio /a /kwenye mzizi ilhali maneno
yenye asili ya kigeni huchukua kiishio aidha /e/, /u/ au /i/
Kuna aina mbili za mizizi, ya leksimu.
2
-wa- Nafsi ya tatu wingi
-li- Wakati (uliopita)
-o- Kirejeshi( urejeshi)
-Samehe- Mzizi
-an- viambishi tamati -an- kiendelezi
-a- -a- kiendelezi
Nafsi (binadamu- kiumbe chenye uhai)
I. Mimi- Sisi (Ni-Tu)
II. Wewe- Nyinyi ( U-M)
III. Yeye- Wao(A-WA)
*Ainisha/ changanua/bainisha/ onyesha sehemu za kisarufi au ainisha mofu na
mofimu za sentensi:
a) Lisilonifurahisha.
Mofu mofimu (maana)
-li- kipatanishi cha ngeli
-si- kikanushi(ukanusho)
-lo- kirejeshi
-ni- mtendwa/ shamirisho
-furahi- mzizi
-sh- kiendelezi
-a- kiishio
b) Sijamchezesha
Mofu mofimu
-si- kikanushi/ukanusho
-ja- kipatanishi
-m- mtendwa/shamirisho
-chez- mzizi
-esh- kiendelezi
-a- kiishio
Mofu Mofimu
-si- kikanushi
-ja- wakati timilifu
-m- mtendewa/shamirisho
-chez- mzizi
-e- viendelezi
-sh-
-a- kiishio
Wakati mfano
Li- uliopita Nilimchezesha
Ta-unaokuja Nitamchezesha
Na-uliopo Ninacheza
Me- timilifu Nimecheza
Ku- Mazoea Nakuchezesha
c) Asiyetuogofya ogopa
Mofu Mofimu
A- Nafsi ya tatu umoja
-si- kikanushi/ukanusho
-ye- kirejeshi/urejeshi
3
-tu- shamirisho
-ogo- mzizi
-fy- kiendelezi
-a- kiishio
AINA ZA MANENO
Nomino
Ni neno linalotaja jina la kitu, mtu, mahali au jambo la udhahania.
Nomino tendaji katika sentensi huchukua sehemu ya kwanza ya sentensi ambayo huelezwa
na kiarifu au kitenzi.
Sehemu hii ya kwanza hujulikana kama kiima na aghalabu huchukuliwa na nomino au
kiwakilishi chake. Kuna aina mbalimbali za nomino.
Aina za nomino
Nomino jumla-kawaida
Nomino za jamii-makundi
Nomino za pekee
Nomino za wingi
Nomino za dhahania
Nomino vitenzi-jina
Vivumishi
Fungu la maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino/ kiwakilishi chake
Aina
Vivumishi vya Sifa: -zuri, -zito, -baya n.k.
Vivumishi viashiria
Visisitizi-papa hapa, papo hapo
Vimilikishi- vinatumia mizizi angu, ake, ako
Virejeshi-hurejelea kitu kilichotajwa tayari.
Mfano; hiyo, hicho hilo
4
Viulizi-hutumia mzizi ngapi na gani
Idadi-hutumia majina ya idadi kamili
Mfano; moja, mbili, tatu
Na idadi isiyo kamili
Mfano; chache, -ingi.nk.
Viwakilishi
Hivi ni maneno ambavyo huwepo wakati nomino haijatajwa. Hufanya kazi ya kuwakilisha
kitu kinachorejelewa pasi kutajwa.
Mfano; Wake ametoweka badala ya, mtoto wake ametoweka
Kilichonifurahisha badala ya kitu kilichonifurahisha.
Kadri tulivyo na aina ya vivumishi; ndivyo tulivyo na aina ya viwakilishi isipokuwa;
1. viwakilishi ngeli
2. Viwakilishi vya nafsi
Wao waliondoka
Kitenzi/ kiarifa/kiarifu
Ni neno linalotupasha habari au linalotuarifu kinachotendwa au kutendewa nomina au
kiwakilishi chake.
Mfano; Mtoto anapikiwa chakula (anatendewa)
Mwanafunzi anaandika (anatenda)
Rudisha ni hodari (t)
Yeye si mwelekezi makini (t)
Kiatu ki sakafuni (t)
Wao wamekuwa wakipigana tangu Jana.
5
wangali uwanjani.
Kiunganishi
Ni neno au fungu la maneno linalounganisha wazo moja na lingine. K.m na, isipokuwa nk.
Vihusishi
Ni neno au fungu la maneno linalounganisha uhusiano kati ya kitu na kingine, jambo na
linguine au mtu na mwingine.
Vihusishi vya wakati, kabla ya, mbele ya, mpaka, hadi n.k
Vihusishi vya mahal; mpaka, nyuma ya, mbele ya.
Vihusishi vya kiwango, mpaka, hadi, pomoni n.k
Vihisishi
Haya ni maneno yanayoonyesha hisia za kindani na zinazoleta mchomo wa moyo
hudhihirisha hisia mbalimbali.
Ili kuwepo na sentensi sahihi, basi maneno haya lazima yapangwe kwa mpangilio mahususi
wa kisintaksia.
Katika sintaksia, tunarejelea jinsi maneno yanavyo ungana na kuhusiana ili kuunda sentensi
zenye maana.
Sharia ya kisintaksia ni kuwa sentensi ianze na nomino au kiwakilishi chake ambacho huitwa
kiima ikifuatiwa na kitenzi au kiarifa muundo wa sentensi kisintaksia ni:
N/W+T
Hata hivyo, nomino au kiwakilishi hiki kinaweza kuambatanisha na maneno mengine
yanayolenga nomino au kiwakilishi hicho na maneno haya huwa ni kivumishi na kitenzi.
Baada ya nomino au kiwakilishi (kiima), sentensi hufuatwa na kiarifa au kitenzi ambacho pia
kinaweza kuambatanishwa na maneno mengine na maneno hayo huwa ni; kielezi pamoja na
nomino tendewa.
Sentensi hii, ili iweze kuleta maana kamili ni sharti iwe na upatanisho wa kisarufi unaofaa.
6
Ni wazi [kuwa kijana na samba wako katika ngeli moja ( kikundi kimoja ) kitu na chuo
kikundi kingine kimoja na jitu na tunda katika kikundi kingine tofauti
Makundi haya yamebainika kwa kuzingatia viambishi awali vinavyo tangulia kila kitensi. Hii
ni dhahiri kuwa, kigezo cha kisintaksia kinachotumikoa katika sarufi ndicho
kinachokubualika kuainisha ngeli na huzianmisha ngeli kwa kuzingatia viambishi awali
kwenye vitensi ili kuleta upatanisho wa kisarufi .
Kwa kuzingatia kigezo hiki tuna makundi yafuatayo ya ngeli.
7
Nomino za Kiswahili kwa kutumia kigezo hiki , hufanywa kwa kuangalia namna
vipashio mbalimbali katika sentensi vinavyochulua na kukabiliana hali inayoitwa
upatanmisho wa kisarufi
Mfano: kijana amefariki
Simba ameuwawa
Kitu kikubwa kimenunuliwa
Chuo kikuu kimefunguliwa
Jitu lilo limemwangamiza
Tunda kubwa limeozea mtini
Ni wazi kuwa kijana na samba wako katika ngeli moja ( kikundi kimoja )
Kitu na chuo kikundi kingine kimoja na jitu na tunda katika kikundi kingine tofauti Makundi
haya yamebainika Kwa kuzingatia viambishi awali vinavyotangulia kila kitensi. Hii ni
dhahiri kuwa, kigezo cha kisintaksia kinachotumika katika sarufi ndicho kinachokubalika
kuanisha ngeli nza huzianisha ngeli kwa kuzingatia viambishi awali kwenye vitenzi ili
kuleta upatanisho wa kisarufi. Wza ama ‘a’ au ‘yu’ – hali ya umoja na ‘wa’ – hali ya wingi
kwenye sentensi . Hujumlisha majina ya vitu vyenye uhai.
a) Binadamu ‘
b) Wadudu
c) Wanyama
d) Ndege k.k
8
Ngeli ya U (14)
Upatanisho wa kisarufi katika hali ya umoja na wingi kwenye vitensi huchukua kiambishi
awali U
a) Nomino za n geli hii ni vitu vya kidhahania vinavyofikirika tu.
Mfano: Utukufu, uchangamfu, umaskini
b) Umoja wa sehemu ya vitu vidogo
Mfano: Ufito, ushanga
c) Baadhi ya majina ya nchi
Ngeli ya YA
Huchukua upatanisho wa kisarufi YA katika hali ya umoja na wingi:
Huwakilisha nomino za vitu visivyoweza kuhesabika, vitu vyenye umajimaji
Mifano: marashi, manemane, maziwa n.k.