Consumer Protection in The Digital Era in Tanzania-Paper in Kiswahili

You might also like

Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 17

WIKI YA HAKI ZA WALAJI DUNIANI

HAKI ZA MLAJI KATIKA ULIMWENGU


WA KIDIJITALI

Mada kwa Wadau wa Mlaji


Joshua Msoma
Afisa Mwandamizi Utetezi wa Mlaji

Machi 13, 2017


Dodoma
TUME YA USHINDANI 1
MPANGILIO WA MADA

Utangulizi

Historia

Umuhimu wa Kauli Mbiu - 2017

Wajibu wa Mlaji katika huduma za kijiditali

Mikakati endelevu ya Tume

Hitimisho
TUME YA USHINDANI 2
UTANGULIZI
 Tarehe 15 ya kila mwezi Machi ni siku ambapo
Walaji wa bidhaa na huduma kwa kushirikiana na
vyombo vinavyowatetea Duniani kote, huadhimisha
Siku ya Kimataifa ya Haki za Mtumiaji.

 Siku ya Kimataifa ya Haki za Mtumiaji


huadhimishwa kwa madhumuni ya kuwakumbusha
walaji haki na wajibu wao katika soko.

 Lengo ni kuwahamasisha kufanya maamuzi sahihi


kupitia taarifa sahihi kuhusu bidhaa/ huduma na
kuchukua hatua stahiki pindi wanapokutana na
changamoto katika soko.
TUME YA USHINDANI 3
HISTORIA
 Tarehe 15, Machi 1962
Raisi wa Marekani katika kikao cha Bunge
aliasisi haki nne za walaji kutokana na hotuba
yake juu ya utetezi wa watumiaji wa bidhaa na
huduma.
“If a consumer is offered inferior products, if prices
are exorbitant, if drugs are unsafe or worthless, if
consumer is unable to choose on an informed basis,
then his dollar is wasted, his health and safety may
be threatened, and national interest suffers.”
John F. Kennedy

TUME YA USHINDANI 4
... HISTORIA
 Haki nne (4) – J. F. Kennedy
i .Haki ya Usalama
ii. Haki ya Uchaguzi
iii. Haki ya Taarifa na
iv. Haki ya Kusikilizwa.
 Shirikisho la walaji Duniani
The International organization of Consumers Union
(IOCU) 1960, na baadae kubadilishwa kuwa
Consumer International (CI), lenye wanachama
zaidi ya 240 katika nchi 120 linafanya kazi ya
kutetea na kulinda maslahi ya walaji Duniani. (CI)
waliongeza haki tatu na kufikia haki saba.
TUME YA USHINDANI 5
... HISTORIA
 CI na Siku ya Haki za Walaji
Mwaka 1983 Siku ya Haki za Watumiaji Duniani
ilianzishwa na hufikia kilele kila tarehe 15 Machi –
“World Consumer Rights Day” (WCRD).

 Kauli Mbiu–‘’Haki za Mtumiaji katika


ulimwengu wa kidijitali”
Kaulimbiu hii imetafsiriwa kutoka katika Kauli Mbiu
ya Maadhimisho ya Siku ya Mtumiaji Kimataifa kwa
mwaka 2017 ambayo inasema ‘’Consumer Rights
in the Digital Era’’.

TUME YA USHINDANI 6
... HISTORIA
 Azimio la UN Namba 39/248
Aprili 9, 1985 Baraza la Umoja wa Mataifa
liliridhia Mwongozo na Sera za Kimataifa za
Kuwalinda walaji “Guidelines for Consumer
Protection (UNGCP)”. Mwaka 1999 haki moja
iliongezwa na kufanya uwepo wa haki nane (8)
zinazotambulika na kuridhiwa kimataifa mpaka
sasa. Marejeo ya UNGCP 2012 – 2015.
J.F.Kennedy – Haki (4)
CI – Haki (3)
UNGCP – Haki (1)

TUME YA USHINDANI 7
UMUHIMU WA KAULI MBIU - 2017
 Idadi ya Watumiaji - Bilioni 3 ulimwenguni (sawa
na asilimia 40 ya idadi ya watu ulimwenguni)
ikilinganishwa na asilimia moja tu ya idadi ya watu
ulimwenguni waliokuwa wakitumia huduma hizo
mwaka 1995.
 Tanzania - Septemba, 2013, Watumiaji zaidi ya
milioni 30.342 wamesajiliwa kwa ajili ya huduma
za fedha kupitia mitandao ya simu za mkononi.
 Miamala – kukua kwa kasi kwa miamala ya
mfumo wa kidijitali yenye changamoto
mbalimbali.

TUME YA USHINDANI 8
…UMUHIMU WA KAULI MBIU - 2017
Baadhi ya changamoto
 Sheria na kanuni dhidi ya kasi ya teknolojia.
 Uhalifu wa kimtandao usiojua mipaka ya nchi.
 Usalama wa taarifa za Watumiaji.
 Kukosekana kwa taarifa kamili (Non-disclosure-
gharama, riba, masharti n.k).
 Matangazo hadaifu.
 Taarifa binafsi za watumiaji kutumika bila idhini ya
wahusika.
 Usalama wa mali za Watumiaji.
 Maadili ya jamii – watoto na vijana?

TUME YA USHINDANI 9
HAKI ZA MLAJI
 Haki ya Kupata Mahitaji Muhimu
 Haki ya Usalama
 Haki ya Kupata taarifa
 Haki ya Uchaguzi
 Haki ya Kusikilizwa
 Haki ya Kulipwa Fidia
 Haki ya Kupatiwa Elimu
 Haki ya Mazingira Mazuri na Endelevu

TUME YA USHINDANI 10
WAJIBU WA MTUMIAJI KATIKA HUDUMA
ZA KIDIJITALI
Tume ya Ushindani (FCC) kama chombo kinachotekeleza
sheria mama ya kumlinda mtumiaji (Sheria ya Ushindani
Namba 8 ya mwaka 2003), kwa kushirikiana na mamlaka
nyingine (BOT, TCRA, nk.) inaendelea kuhakikisha kila
mtumiaji wa miamala ya kidijitali anafaidika na matumizi
salama ya mfumo huu wa maisha ya kisasa.
Vile vile, Tume ya Ushindani inaendelea na kupokea,
kupitia na kusajili mikataba ya mtumiaji inayoandaliwa na
mtoa huduma (ikiwemo ya huduma za kidijitali) ili kuondoa
masharti yanayomkandamiza mtumiaji na kukwepa
uwajibikaji.

TUME YA USHINDANI 11
WAJIBU WA MTUMIAJI KATIKA HUDUMA
ZA KIDIJITALI
Pamoja na jitihada inazochukuliwa katika kumlinda
mtumiaji, bado mtumiaji huyo anawajibika:-
 Kuhakikisha anatumia mitandao salama na inayoaminika.
 Kujiridhisha na sera za usalama na usiri za mtandao husika.
(kusoma, kuelewa na kuzingatia).
 Kutunza kumbukumbu zake binafsi katika hali ya usalama yakini.
 Kupata taarifa sahihi kabla ya kutumia mitandao hiyo;
 Kutoa taarifa na kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka husika ili
kutanzua migogoro au malalamiko yake kuhusu huduma
zisizoridhisha;

TUME YA USHINDANI 12
…WAJIBU WA MTUMIAJI KATIKA
HUDUMA ZA KIDIJITALI
 Toa taarifa za kulipia miamala kwa biashara/taasisi
unayoifahamu na kuiamini.
 Weka kumbukumbu sahihi za miamala yako ya
kidijitali.
 Pitia mara kwa mara taarifa zako na kumbukumbu
zako kwa kubaini utofauti usioufahamu.
 Badilisha nywila yako mara kwa mara.
 Toa taarifa unapogundua tatizo mara moja kwa
vyombo husika.
 Shirikisha/uliza kabla ya kufanya maamuzi.
 Badilishana taarifa zako kwa umakini mkubwa.
TUME YA USHINDANI 13
MIKAKATI ENDELEVU YA TUME
Tume ya Ushindani (FCC) – Imechukua na inaendelea
kuchukua hatua za muda mfupi na mrefu ili kumlinda mlaji wa
kitanzania dhidi ya mienedo potofu na hadaifu ya kimasoko:-
 Kuanzisha rasmi maadhimisho ya Siku ya Haki za Walaji
Duniani nchini Tanzania – 2009.
 Kushirikiana na taasisi na asasi mbalimbali katika kumtetea
na kumlinda mtumiaji.
 Kutekeleza sheria ya kumlinda mtumiaji.
 Kushiriki katika kutengeneza sheria mbalimbali za kumlinda
mlaji (Electronic Transaction Act 2015, The National
Payment System Act 2015, Tanzania Electronic
Transactions Act 2015 and Electronic Money Regulations
2015 n.k).

TUME YA USHINDANI 14
…MIKAKATI ENDELEVU YA TUME
 Uandaaji wa mkakati wa kumlinda mtumiaji wa
huduma za kifedha kwa kushirikiana na wadau wa
kisekta.
 Kutoa elimu ya kumlinda mtumiaji kwa njia mbalimbali.
 Kushirikiana na wadau wa Elimu kutengeneza na
kuingiza elimu ya mtumiaji katika mitaala.
 Utafiti na uchunguzi wa kimasoko kubaini mienendo
potofu na hadaifu sokoni.
 Kushiriki katika kuandaa Azimio la Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa Namba 70/186 Kuhusu Utetezi
wa Mtumiaji Desemba 22, 2015.

TUME YA USHINDANI 15
HITIMISHO
 Tume ya Ushindani imejizatiti katika kutetea na
kusimamia haki za watumiaji wote kwa kutekeleza
na kusimamia vyema Sheria ya Ushindani.
 Jitihada zaidi zinahitajika si kutoka kwa wadau wa
huduma za kijiditali tu, bali kutoka kwa wadau wote
katika kusambaza elimu ya mtumiaji ili kuleta
chachu kwa walaji kuchukua hatua stahiki katika
kutetea haki zao.
 Tume ya Ushindani inatoa rai kwa wadau
mbalimbali katika vikundi, taasisi au mdau mmoja
mmoja kutoa ushirikiano wa dhati katika kampeni
hizi za uhamasishaji wa umma kuhusu masuala ya
kumtetea na kumlinda mtumiaji nchini.
TUME YA USHINDANI 16
AHSANTENI
KWA
KINISIKILIZA

www.competition.or.tz
info@competition.or.tz

TUME YA USHINDANI 17

You might also like