UAKIFISHAJI

You might also like

Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 7

Uakifishaji/Punctuation

Uafikishaji unatuwezesha kuyasoma yale yameandikwa kwa urahisi na kuyaelewa


vilivyo. Iwapo maandishi yetu hayataakifishwa vilivyo, basi itakuwa vigumu sana
kuyasoma na kuyaelewa.
Uakifishaji basi inahusu:
1. Nafasi(space)
2. Herufi kubwa(capital letters)
3. Kituo kikuu/nukta/kitone ( . )(full stop)
4. Koma/kituo/mkato ( , )(Comma)
5. Alama ya kiulizi ( ? )(Question mark)
6. Nukta na koma ( ; )(Semi colon)
7. Nuktambili ( : )(full Colon)
8. Kihisi ( ! )(Exclamation mark)
9. Parandesi/mabano ( )(brakets)
10. Kistari kirefu ( _ )(dash)
11. Kistari kifupi ( - )(Hyphen)
12. Mkwaju ( / )(stroke)
13. Ritifaa ( ' )(Apostrophe)
14. Alama za usemi ( " " ) ( ' ' )(Quotation Marks)
15. Nukta za dukuduku ( ... )(Dots)
Nafasi

Kuacha nafasi ya kutosha baina ya neno


moja hadi lingine.
Kamwe tusishikanishe maneno yasiyostahili
wala tusikate maneno yasiyostahili. 
k.m:Makau ame enda nyumbani – Makau ameenda nyumbani.
Shisia na Alele ndiowerevu – Shisia na Alele ndio werevu.
Herufi kubwa

Herufi kubwa:Hutumika;
Mwanzoni mwa sentensi.
Mwanzoni mwa nomino/majina kama
vile: Nairobi, Uganda
Kituo kikuu ( . )

Kituo kikuu/nukta/kikomo/kitone ( . )
Hutumika:
Mwishoni mwa sentensi: k.m tutafika alfajiri na
mapema.
Kufupisha maneno: S.L.P. (Sanduku la posta).
Bw. Juma (Bwana Juma)
Kutenga kiwango cha kitu kama vile : fedha,
kilomita, kilo n.k. Sh 6.80 (shilingi sita na senti
themanini).
Kilomita 2.5 (kilomita mbili na nusu).
KOMA

Koma/kituo/mkato ( , )
Hutumika:

Mahali msomaji anapopumua au anapotua. k.m.


Nilipokula na kushiba, nilifunganya virago vyangu na kuondoka.
Tunapoandika anwani:
Shule ya Bidii,
S.L.P. 20400,
HOMA BAY.
Kutenganisha orodha ya maneno. k.m Alinunua mkate, maziwa,
sukari na kahawa.
Kutenganisha sentensi za masharti k.m. Nikijitahidi, nitafua dafu.
Alama Ya Kiulizi

Alama ya kiulizi/kiulizo ( ? )
Hutumika Kuulizia swali linalohitaji jibu k.m
:Je, utafika shereheni?
: Je,Umesoma ?
:Unataka kusafiri leo?
:Nikifanya bidii utanipa zawadi?
Alama Za kunukuu/Usemi
Hutumika kuonesha usemi ulionukuliwa.
Hutumika kutaja majina rasmi au yasiyo rasmi katika
sentensi.

Mfano
Baada ya mgomo, walimu walisema "Tutarejea darasani”
Alipoingia”Mamba” watu walikimya

You might also like