Chombo hiki kwa kawaida huwa na akrabu. Akrabu ni sawa na vijiti. Kuna akrabu fupi ionyeshayo saa (dakika sitini) na ile ndefu ionyeshayo dakika. Ya tatu ambayo pia ni ndefu, huonyesha sekunde. Akrabu fupi inapomaliza nzunguko mmoja huwa imechukua muda wa saa kumi na mbili. Kwa hivyo basi, akrabu hii fupi huchukua muda wa saa moja “kwenda” kutoka nambari moja hadi ile nyingine. k.m. kutoka moja hadi mbili. Nayo akrabu ndefu ya dakika, huchukua dakika sitini au saa moja kufanya mzunguko mmoja. Ile ndefu ya sekunde (nukta) hutumia dakika moja (sekunde sitini) kuzunguka mduara mmoja.