Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 22

FONOLOJIA

FONOLOJIA
• Fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya
sauti za kutamkwa zinazotumika katika lugha asilia mahususi
za binadamu.
• Fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa sauti
za lugha mahususi tu, hivyo, tunapata fonolojia ya Kiswahili,
fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kitiriki,fonolojia ya
Kifaransa, fonolojia ya Kimaragoli, n.k.
• Kipacha (2002) Fonolojia ni taaluma ya uchambuzi na
uchanganuzi wa mfumo wa vitamkwa vya lugha
maalumu na jinsi vinavyofanya kazi
• Massamba na wenzake (2004:6) wanaongezea fasili
hiyo kwa kusema kuwa taaluma hii hujihusisha hasa na
‘sharia au kanuni zinazoandamana na utoaji na utumiaji
wa sauti pambanuzi
• Fonolojia ni uchunguzi wa miundo ya lugha. Je, ni kwa
namna gani sauti zimepangika katika lugha.
Aina za fonolojia

• Fonolojia vipande
• Huchunguza sauti za lugha maalum.
• Hushughulikia uanishaji sauti
• Ufafanuzi sauti kwa sifa bainifu
• Mifanyiko ya kimofofonolojia
• Fonolojia arudhi
• Sifa za kiarudhi zinazoathiri sauti-mkazo, kidatu, kiimbo,
wakaa, silabi
Kazi/Umuhimu wa fonolojia

• Kila lugha ina sauti ngapi?


• Ni kwa namna gani sauti zinapangika katika lugha?
• Kuna michakato gani iliyopo wakati sauti zinaungana
kuunda neno?
• Kwa kiasi gani fonolojia maalumu huchangia kanuni
bia?
• Kiwango cha chini kabisa katika fonolojia ni FONIMU.
• Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza
kubadili maana ya neno
• Hivyo basi, fonimu ina maana, kwa kuwa inaweza
kubadili maana ya neno inapobadilishwa nafasi katika
neno husika
• Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika bohari la sauti ili
zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi ndiyo
fonimu
• Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya
fonimu za lugha hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine.
• Mathalani, Kiarabu kina fonimu (28), Kiswahili kina fonimu
(30), Kifaransa kina (33), na Kiingereza kina fonimu (44).
• Sauti ambayo huweza kubadilishwa nafasi yake katika neno
lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.
Alofoni

• Kipashio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo


fonimu moja hutamkwa na kuandikwa
tofautitofauti bila kubadili maana ya neno.
Mfano: Fedha/fadhaa na feza/fazaa,Heri na kheri.
Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya
fonimu (sauti) moja.
• Katika miktadha mingine, wataalam wanadai kwamba
fonimu ni umbo lilelile ila tofauti hutokea katika
utamkaji wa sauti-mf. K na K ya mpumuo; P na P ya
Mpumuo.
Mkazo
• Ni msisitizo/utamkaji wa neno kwa kutumia nguvu nyingi, hii
hulifanya neno au silabi kusikika zaidi kuliko mengine au silabi
zingine. Mf ba’rabara (sawasawa), bara’bara (njia), wa’lakini
(kasoro), wala’kini (kiunganishi)
• Pia kwenye sentensi:
• Waandika ‘meza (watu wanaoandaa meza)
• Wa’andika meza?
Kidatu

• Sifa ya kiarudhi inayobainisha kupanda na kushuka


kwa kiwango sauti.
• Sauti yaweza kuwa ya juu au ya chini kutegemea
msepetuko wa nyuzi sauti
• Sauti ya juu huonyesha hasira,na ya chini-huzuni au
masengenyo
Wakaa

• Muda unaotumika kutamka sauti Fulani.


• Kuna viwango 3 vya wakaa:mfupi, kawaida na mrefu
• Kiswahili huwa na wakaa mrefu na wa kawaida tu
• Wakaa mrefu hutumia [:].
• Mf-Kiinimacho-ki:nimacho; kaakaa-ka:ka:
Kiimbo

Upandaji/ushukaji wa mawimbi sauti


Kiimbo huadamana na kidatu (Kidatu cha chini, wastani
na juu) wakati wa kutamka sauti. Hata hivyo, kiimbo
hutokea sana katika: kutoa amri, mshangao, swali na
maelezo ya kawaida.
Silabi

• Ni nini? Umbo la matamshi ambapo sauti moja au zaidi


hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja.
• Huundwa na fonimu moja au zaidi.
• Kuna aina 2 kuu:
• Silabi huru/wazi-huishia kwa irabu.
• Silabu funge-huishia kwa konsonanti.
Miundo ya silabi ya Kiswahili sanifu
• I
• KI
• K
• K1/2II
• KKI
• KKKI [SKRUBU, SPRINGI]
• KK1/2II [MPENDWA]
Mifanyiko ya kimofofonolojia
• Ni nini?
• Mabadiliko yanayotokea wakati ambapo fonimu 2 huambatana katika
kuunda vipashio vikubwa kuliko fonimu.
• Hutokea kwa sababu sauti moja huathiri nyingine katika mazingira ya
utokeaji.
• Kuna aina mbalimbali za mifanyiko
AINA
• Udondoshaji-{mu}+{ti}, {Mu}+{toto}, {wa}+{alimu}
• Haukuja, hautaki, hauendi nk
• Cha+angu. Cha+ake nk
• Zi+etu, zi+enyu nk
• Wa+eupe; wa_enyewe nk
• Mvutano wa irabu
• Ma+ino
• Wa_ingi
• Wa+itu
• Ukaakaishaji
• Ki+angu
• Ki+ake
• Ki+ao
• Ki+akula nk
Tofauti kati ya fonetiki na fonolojia
• Mjadala na wanafunzi darasani.

You might also like