Download as ppt, pdf, or txt
Download as ppt, pdf, or txt
You are on page 1of 20

Mpango wa biashara

inayoanza
Paul Pm Ndomba
Mob: +255 712 288 012; Email: ndopa4@yahoo.com
Skype ID: Maprosoo2; Fb: mcndomba Maprosoo

“Wanaoongoza vyombo vya usafiri, wanaweza kwenda kokote


wanakotaka kufika bila kupotea; ili mradi tu wawe na ramani zenye
vipimo sahihi”

12/18/23 mcndomba 1
Matarajio ya mada hii ujue;
1. Maana ya mpango wa biashara
2. Umuhimu wa kuwa na mpango wa biashara
3. Waandaaji na watumiaji wa mpango wa
biashara
4. Namna ya kuandika mpango wa biashara
5. Jinsi ya kutumia mpango wa biashara

12/18/23 mcndomba 2
Kupanga ni nini?
Kupanga ni kuchagua matendo yanayotumia
muda na rasilimali za kifedha ili kuzitumia kwa
ufanisi/uchache ili kupata matokeo makubwa
ama mazuri
Watu wanajua kupanga, ila wanatofautiana
katika namna ya kupanga na namna ya
kutekeleza vizuri walichopanga

12/18/23 mcndomba 3
Kauli hizi ni za kweli
1. Asiyepanga chochote, tayari amechagua
kushindwa
2. Asiyepanga vizuri, anapanga vizuri namna ya
kushindwa
3. Asiyetekeleza anachopanga vizuri, anatekeleza
kushindwa
4. Anayetekeleza vizuri aliyepanga vizuri,
amechagua kufanikiwa vizuri
Idadi kubwa ya watu inatekeleza mipango yao kwa
kauli namba 1 hadi 3 na ndio maana wengi
wanashindwa
12/18/23 mcndomba 4
1. Mpango wa biashara ni nini?
Mpango wa biashara ni andiko linalofafanua
namna biashara mpya itakavyoanzishwa au;
namna biashara iliyopo itakavyopanuliwa ama
kuundwa upya
Unahitaji mpango mzuri wa biashara kabla ya
kuanza shughuli yoyote ya kuanzisha biashara
mpya au kupanua uliyonayo

12/18/23 mcndomba 5
2. Umuhimu wa mpango wa biashara

i. Unaongeza mafanikio katika biashara yako


ii. Unaonyesha dira ya kutekeleza shughuli na
namna ya kutumia rasilimali zilizopo
iii. Utaweza kujua muda uliojiwekea kupata
malengo ya kumiliki biashara yako
iv. Utawezesha kujua vyanzo vya mapato
v. Ni rahisi kufanya tathmini ya biashara yako
vi. Unawezesha kuchanganua shughuli
zilizopo; nani, wapi, lini, zana, vipi, ngapi, nk
12/18/23 mcndomba 6
Hasara inayopatikana inaashiria
 Kutokuwa na mpango mzuri
 Kutekeleza vibaya mpango mzuri
 Kutekeleza vizuri mpango mbaya
 Kuto kutekeleza kilichopangwa vizuri
Kupata faida nzuri ni lengo la kila
mfanyabiashara
Anapopata faida kubwa inaweza kuashiria kuwa
mpango wa biashara ulipangwa na
kutekelezwa vizuri
12/18/23 mcndomba 7
3. Waandaaji na watumiaji
Mpango kazi huandaliwa kwa ajili ya;
1.Wamiliki wa biashara au mradi
2.Mameneja watakaoendesha mradi huo
3.Wawekezaji walio tayari kukupa mitaji yao
4.Wajumbe wa kikao cha utendaji (bodi)
5.Kitengo cha usajiri wa biashara au mradi
6.Kupata ruzuku au kukopeshwa fedha na benki
au mtu makini

12/18/23 mcndomba 8
Watumiaji wanapenda kujua yafuatayo;

1. Je, kazi maalumu ya biashara inatekelezeka au la?


2. Watendaji/wasimamizi wa mradi wanasifa?
3. Gharama za biashara kabla ya kuuza bidhaa
zenyewe ni zipi?
4. Fedha za kulipia gharama hizo zitatoka wapi?
5. Je, bidhaa yako itapata soko la uhakika?
6. Mauzo yataleta mapato yanayotosha gharama za
shughuli na kuongeza mtaji?
7. Je, mapato yatatosheleza ulipaji wa deni, gawio la
faida kwa waliotoa mtaji na kuacha faida?
Majibu ya maswali hayo ni mafanikio ya biashara yako
12/18/23 mcndomba 9
Nani anapaswa kuandaa?
 Mpango wa biashara yako unapaswa kuandaliwa na
wewe mwenyewe
 Kama biashara yako inagharimu mamilioni ya shilingi
za kitanzania, unaweza kushirikiana na wataalamu
wa kifedha/ wahasibu/ watu wazoefu katika aina ya
biashara yako
 Meneja wa biashara anapaswa kuwepo wakati wa
mchanganuo wa biashara
 Kama meneja hakuwepo anapaswa kuelezwa kwa
ufafanuzi wa karibu ili ajue na kuelewa kilichopangwa

12/18/23 mcndomba 10
4. Namna ya kuandika mpango wa
biashara

Sura muhimu za mpango wa biashara


i.Utangulizi na historia fupi ya biashara
ii.Wasifu na malengo ya biashara
iii.Bidhaa au huduma itakayotolewa
iv.Menejimenti na utawala
v.Masoko na uuzaji
vi.Mahitaji ya kifedha
vii.viambatanisho

12/18/23 mcndomba 11
a) Utangulizi & historia fupi ya biashara

Andika mhutasari mfupi wa biashara unayopendekeza


kuianzisha. Zungumzia kwa ufupi maeneo yafuatayo;
Jina la biashara yako
Hali halisi ya biashara kama yako mtaani/nchini
Hali ya uchumi na kubadilika kwa tabia ya matumizi ya
wateja
Masoko na urahisi wa kuuza
Hitaji la mtaji na makisio ya faida
Umahiri wa meneja au wasimamizi wa biashara yako
kwenye soko kwa urahisi

12/18/23 mcndomba 12
b) Wasifu wa malengo ya biashara
Changanua hali halisi ya biashara au huduma unayotoa au
unayokusudia kutoa, na weka malengo ya biashara yako.
Zingatia;
Utume na njozi ya biashara yako (mission&vision)
Nembo au alama ya bidhaa kama ipo
Lengo mahususi la biashara
Mahali biashara ilipo
Malengo katika muda mfupi na mrefu
Uimara na udhaifu wa biashara yako
Fursa na vitisho vinavyowakabili
Namna unavyoweza kuchangamkia fursa na kukabiliana na
vitisho kwa mafanikio
12/18/23 mcndomba 13
c)Bidhaa au huduma itakayotolewa

Fafanua kwa undani namna bidhaa ilivyo, unavyokusudia


kuizalisha, kuiboresha na kuifanya ipenye kwenye soko.
Zingatia;
Orodha ya bidhaa au aina ya huduma utakazotoa
Malighafi ya kutengenezea
Mchakato wa kuitengeneza hadi ikamilike
Picha au mchoro wake kama upo
Ulinganifu wa bidhaa/huduma za wengine zinazofanana
na yako
Mbinu za kuwashinda washindani
Matokeo/faida watakayopata watumiaji wa bidhaa/huduma
yako
12/18/23 mcndomba 14
d) Menejimenti na utawala

Eleza umahiri wa meneja, elimu na uzoefu wake, mipango ya


kujiendeleza na kuendeleza wafanyakazi wengi
Taja idadi za biashara au mradi wako
Idadi ya wafanyakazi na namna utakavyowalipa
Onyesha chati ya mfumo wa utawala
Eleza utekelezaji wa majukumu ya kila siku
Utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya kazi zilizokamilika kwa siku
Taratibu za vikao na namna ya kuviendesha
Udhibiti wa ndani katika manunuzi, utunzaji wa malighafi, bidhaa,
vifaa na fedha
Taratibu za kisheria. Mf. Kujisajili, utambulisho wa mlipa kodi (TIN
no).,nk

12/18/23 mcndomba 15
e)Masoko na uuzaji
Fafanua kwa ufupi yafuatayo;
Walengwa wa bidhaa au huduma yako. Nani,
wapi, lini, vipi, namna gani, nk
Utakavyoipenyeza kwenye soko
Wapi bidhaa yako itasambazwa
Namna ya kuwajulisha watumiaji. Mf. Redio, tv,
magazeti, nk
Namna ya kupanga bei ya kuuzia

12/18/23 mcndomba 16
f) Mahitaji ya kifedha

 Taja fedha zinazotakiwa kuanzisha biashara yako


 Eleza vyanzo vya mapato
 Eleza kiasi kitakachotosha kuendeshea shughuli zote
(working capital)
 Kama ni mkopo au msaada taja kiasi utakacho
changia
 Taja idadi na thamani ya vifaa unavyohitaji
 Andika taarifa ya utendaji, mauzo na matumizi
 Andika taarifa ya ukuaji wa mtaji

12/18/23 mcndomba 17
g) Viambatisho

Viambatisho vinavyotakiwa ni kama;


Picha za bidhaa
Mfano wa fomu kutoka kwa wateja wanaotaka
kununua bidhaa (customers’ order forms,) nk

12/18/23 mcndomba 18
5. Jinsi ya kuutumia mpango kazi

 Namna ya kuutumia ni kurejea katika kila


kipengele na kuona jinsi kinavyotekelezwa
kama ndivyo kilikuwa kimepangwa
 Ni muhimu pia kuandaa mpango mkakati
ambao utaonyesha muda wa kuanza na
kukamilisha kila kipengele
 Utataja kila muhusika na majukumu yake
 Zana atakazotumia na watu atakaoshirikiana
nao

12/18/23 mcndomba 19
.

 Asanteni

12/18/23 mcndomba 20

You might also like