NILITAMANI

You might also like

Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 9

NILITAMANI

Mwandishi: Phibbian Muthama


Wanatimu wa Simba 3A
1) Aaron Njugi- Nahodha
2) Andrew Muraguri- Naibu wa Nahodha
3) Antwan Mwangangi
4) Adam Otieno
5) Darrel Njoroge
6) Tyler Maina
7) Ian Irungu
8) Imani Mathenge
9) Rodney Mulei
10) Muhsin Shabban
11) Anthony Kariuki
MUHTASARI
• Mhusika mkuu wa hadithi hii ni Tumaini, msichana mmoja aliyehamia
Tanzania kutoka Kenya. Ana matumaini mengi anapofika Tanzania kwamba
atapata ajira na kujitoa kutoka umaskini. Alipofika, alisaidiwa na rafiki yake
Nina aliyemsaidia sana; alimtembeza sehemu nyingi pamoja na kumpa
chakula na pa kuishi. Tumaini anamwonea Nina wivu kwa kuwa ana mume
mzuri, na wana nyumba bora na maisha mazuri. Anaamua kujikaza ili Maisha
yake iwe kama ya Nina.
• Tumaini anapohisi kuwa Nina amemsaidia kutosha, anaamua kuondoka na
kuenda mjini. Anapanda matatu inayompeleka kutoka Kigamboni, mji
alipokuwa, hadi soko la mji wa Kariokoo. Ingawa hana pesa, anamdanganya
utingo kuwa alipoteza kipochi chake. Baadaye, anaenda kuomba kazi katika
ofisi ya mabasi za Tahmeed, ambayo anakumbuka yakiwa Kenya.
• Anashukiwa kuwa tapeli (mtu anayedanganya watu ili kupata pesa kutoka
kwao) lakini hatimaye, anapewa shilingi elfu tano za Tanzania. Anaambiwa na
jamaa yule kuwa iwapo atapata kazi, atampigia Tumaini simu. Kwa hayo,
Tumaini ananunua mboga na kuenda nazo kumwona rafiki yake, Jenifa,
akisema kwamba si vyema kufika kwa nyumba ya mtu mkono mtupu.
• Jenifa anafurahi kumwona Tumaini na mboga hizo. Wanakaa pamoja kwa wiki
tatu. Kwa bahati mbaya, Tumaini bado hajapata kazi. Jenifa anaanza kukasirika
kidogo, kwa kuwa Tumaini hamsaidii kulipia mahitaji lakini anatumia sabuni
yake na kula chakula chake. Alifikiri arudi nyumbani Kenya, lakini akaona kuwa
hangekuwa na jibu kwa bibi (nyanya) yake, Farida, na mwana wake, Radhi,
ambao aliwaacha.
• Siku moja, Nina anampigia simu na kumtumia pesa. Tumaini anafurahi na
kuamua kuenda Coco Beach. Anakaa huko, akitazama bahari. Ghafla, anasikia
sauti ya gari. Mwanaume mtanashati ajabu anashuka na kumwendea Tumaini.
Anamdanganya kuwa ametoka Kenya, na kuwa amemwona Tumaini katika mji
wa Westlands awali, lakini Tumaini anakataa.
• Wanaendelea kuzungumza. Bwana yule, anayeitwa Romeo, anampenda
Tumaini Zaidi, kiasi cha kumwomba Tumaini aende naye kula chamcha katika
hoteli fulani. Wanaondoka katika gari lake Romeo la Audi Q5. Humo, Romeo
anamwambia Tumaini kuwa anataka awe mke wake. Tumaini anakubali.
• Garini, Romeo anampapasapapasa (anamgusagusa polepole kwa mkono) na
papo hapo, Tumaini anagundua kuwa Romeo si mtu, bali ni jini! Rangi ya sura
yake inabadilika kuwa mweupe tena mwekundu. Romeo anapigiwa simu na
mtu anayesema kuwa damu yake Tumaini inahitajika kwa haraka sana.
Hatimaye, Tumaini anatorokea msitu mmoja ili kujiokoa, bila hata kutaama
nyuma yake.
MAUDHUI
• 1) UMASKINI
• Tumaini anasema kuwa hajala tangu siku iliyopita, kwamba amekunya
tu chai ya rangi, ishara ya umaskini wake.
• Tumaini anaonyesha umaskini wake anaposema kuwa ana matumaini
kuyashinda maisha ya umaskini na ukosefu wa mahitaji ya kimsingi.
• Tumaini anamwambia jamaa wa ofisi za mabasi kuwa anahitaji nauli,
chakula na ajira; ishara kuwa hana chochote wala lolote.
2) HISANI
• Nina anampa Tumaini mahali pa kuishi kwa miezi mitatu. Anashughulikia
mahitaji yake yote. Baadaye, anamtumia pesa bila hata kuulizwa.
• Jenifa anamsaidia Tumaini kwa kumpa mahali pa kuishi kwa wiki tatu.
Anashughulikia mahitaji yake.
• Tumaini aliruhusiwa kusafiri bila kulipa nauli.

3) MATUMAINI
• Tumaini ana matumaini kuwa atayashinda Maisha ya umaskini na ukosefu wa
mahitaji ya kimsingi.
• Tumaini anasema alifika Tanzania kwa kuwa alikuwa na matumaini kuwa
angepata maisha mema.
4) UDANGANYIFU
• Tumaini anamdanganya Jenifa kuwa alikuwa amekula tayari ili ampunguzie
gharama ya chakula.
• Tumaini anadanganya utingo kuwa alikipoteza kipochi chake cha pesa.
• Tumaini anadanganywa na Romeo eti anadai awe mkewe, kumbe ni jinni
anayetaka damu yake!

• 5) KAZI
• Tumaini anatafuta kazi ya aina yoyote mjini. Anaenda kwa ofisi za mabasi ya
Tahmeed na kuomba kazi huko.

• 6) URAFIKI
• Tumaini amejaliwa na marafiki wawili wazuri, Nina na Jenifa, wanaomsaidia
kwa hali na mali.

You might also like