Professional Documents
Culture Documents
Kanuni 10 Za Kutafasiri
Kanuni 10 Za Kutafasiri
Kanuni 10 Za Kutafasiri
MAANDIKO
TR MGINA LODI
UTANGULIZI
• Hoja za mwanzo:
• Hermeneutics- ni neno linalotokana na neno la
kiyunani hermeneuo lililo na maana ya “kutafsiri”
• II. Kuelewa kwa wasiotii kuta punguzwa (Ebra 5:11-14); wavivu kusikia,
kwakutumia akili na neno (utii) wamejua kupambanua mema na mabaya. Rum
1:24-25; walibadili kweli kuwa uongo
• III. Kuelewa kwa wanao tii kutaongezwa: Mamajusi wanapewa nuru kwa kutii
(Mth 2:1-5), Daudi anapata baraka kuu kwa kutii na kuongezewa ufahamu.
Zaburi 119:97-101
SURA YA PILI
KANUNI YA UVUVIO
• 1. Maandiko yote yamevuviwa na Mungu: uvuvio= “kupumulia ndani
ya” waaandishi wake walipumuliwa ndani yao. (2 Tim 3:16)
• Hii ina maanisha kuwa waliongozwa na Roho (2 Pet 1:20-21).
• C. katika maisha binafsi: himizo na imarisho; sio kila andiko laweza tumika katika
itikadi lakini maandiko yote yanaweza tumika katika huduma lakini sio yote
yatatumika katika maisha ya mtu binafsi. Mfano katika kuzidai ahadi katika maandiko.
Je ni nani anaweza kuzidai ahadi hizi? (Mt 10:17, 11:22, 26:34, Yoh 21:18, Mdo 5:9b,
9:16)
SURA YA TATU
KANUNI YA MUKTADHA
• KANUNI YA MUKTADHA: 1. kuelewa muktadha wa
kihistoria: neno hili linatokana na neno la kingereza context ambalo
linatokana na maneno mawili ya kirumi “con” (pamoja) na “textus” (fuma)
hivyo maana ya neno context ni “fuma pamoja”. Maana ya kila mstari wa
maandiko imefumwa pamoja na muktadha wa kihistoria na wakawaida.
• Muktadha huu una mambo kama: mwandishi na tarehe, waandikiwa,
tamaduni, tatizo lililopelekea kuandikwa kwa kitabu. Huwezi elewa mstari
kama hujajua umefumwa katika hali gani ya kihistoria (picha kwenye kanga)
• Hatua 3 za kubainisha muktadha wa kihistoria , hasa katika nyaraka ni.
• 1. jibu maswali ya muandishi a) alikuwa nani? b) je aliandika lini.
• 2. jibu maswali juu ya wasomaji a) wakina nani? b) wamji gani? c) hali ya ya
maisha (wayahudi au mataifa, tajiri au maskini?
• 3. tambua shida ambazo muandishi aliandika kutatua
SURA YA TATU: MUKTADHA
2: kuelewa muktadha wa kimaandishi
• Muktadha wa kimaandishi tuna maanisha maneno na mistari na
vifungo vyote vinavyo izunguka makala. ni mawazo yanayo kuja
kabla na baada ya makala.
• Ukijaribu kutoa makala katika muktadha wake utaharibu kila kitu.
• Hatua 5 za kuchunguza muktadha wa kimaandishi
• 1. taja kichwa kikuu cha kitabu/sehemu uliyo chagua.
• Ukitumia andiko moja tu unaweza kupata dhana zisizo sahihi kama vile:
• Usiwahubirie wamataifa bali wayahudi tu (Mt 10:5) usibebe pesa/ nenda bila viatu
(Mt 10:27) watemee watu mate kabla hujawaombea (Mk 8:23)
• 2. MUWEKE PUNDA MBELE: hatuchagui yale tunayo penda tu kuhubiri,; isome biblia
kwa makini juu ya yale unataka kuzungumzia.
• Ukiamua yale unataka kuhubiri kisha kwenda kutafuta mistari ya Biblia kuunga mkono
mahubiri yetu, nisawa na kuweka gari mbele ya punda.
• (mfano: Branham: aliomba usiku kucha akapata wazo kuwa hakuna utatu bali Yesu
pekee, aliweka gari mbele ya punda, alipata wazo kisha kwenda kutafuta maandiko ya
kumuunga mkono wazo lake. Alipata tu Yn 14:9; na hakuwaza kuhusu Yn 14:1, Yn
14:21; 23; 24; 25-26) lazima kutafasiri maandiko kwa upatano wa maandiko
mengine
SURA YA SITA
KANUNI YA UPATANO
• 3. TENA IMEANDIKWA: (Mt 4:5-7) tunapo toa maandiko kwenye Biblia
iwe kwa kusudi la kutoa muangaza, shetani alitumia “imeandikwa
kutaka kumuongoza Yesu gizani.
• 2. Agano La Kale sio Agano letu: ilikuw kati ya Israeli na Mungu, wakristo
hawapo chini ya sheria ya kale (Rum 6:14, Yn 1:16-17, Gal 5:4): Yesu hakuja
kuharibu sheria ila kuitimiza, alikuja kutupatia haki kwa neema badala ya
matendo. Agano letu sio la kale bali jipya pamoja na Mungu (Rum 10:4)
• 3. Baadhi ya Masharti ya Agano la Kale hayafanywi upya katika Agano
Jipya: sheria ya agano la kale (1. utaratibu wa ibada 2. sheria za jamii)
zinapatikana katika vitabu vya walawi, kutoka, kumb, hesabu. Rangi gan?
Mavazi gani? Sadaka gani? Haya maswali yote yange jibiwa na sheria hii ya
utaratibu wa ibada. Chakula, hekalu , ukuhani na sadaka katika agano jipya
yame badilishwa kabisa. (1 Tim 4:1-5)
• hata sheria za jamii, ambazo zilikuwa zina simamia mahusiano katikati ya
mtu na mwenzake ni tofauti sana kwa sasa. (hutumpigi mzinzi mawe)
SURA YA SABA
KANUNI YA MAAGANO
• 4. Kanuni Za Maisha Maadilifu Za Agano La Kale zimerudiwa Upya Katika
Agano Jipya: tumekwisha angalia kuwa katika (Mathayo 5:17-20) Yesu hakuja
kuharibu sheria.
• Lakini: Yesu anasisitiza kanuni kuliko amri yenyewe kwakuwa kila amri ilikuwa
na kanuni nyumba yake:
• 1. katika amri ya kuua yeye alisema ni makosa kuchukia (Mt 5:21-24) 2.
Amri ya kuzini akasema tamaa ni mbaya (Mt 5:27-30) 3. katika amri ya viapo
alienda zaidi na kusema tutekeleze tuliyo ya ahidi (Mt 5:33-37)
• Neema haiondoi amri juu ya maadili na tabia, bali inaangazia kanuni iliyo
ndani ya sheria.
• 4. Afya: tuna lindwa na kupokea uponyaji (Yko 5:15) lakini bado miili yetu ni
dhaifu, lakini katika utimilifu wa ufalme huo hapatakuwa na huu udhaifu (ufu
21:4)
• 5. Mali: yeye hushughurikia mahitaji yetu (Mt 6:33) ukristo sio njia ya kujipatia
utajiri (1 Tim 6:5) utajiri tunao ahidiwa ni wa zaidi ya haya ya dunia (Lk 8:14)
SURA YA NANE
KANUNI YA UFALME
• 6. Mateso: kwa kiasi fulani baada ya kumpokea Kristo kwa kiasi fulani tunapata pumziko, lakini huu
ufalme ulikuja na mateso mapya (Mt 10:34 kuchukiwa) pia katika kupewa nidhamu na yeye kuna
mateso (Ebr 12:5-6) lakini kuna wale watakao vumilia mateso hadi mwisho nao wataponywa (Mt
24:13; Ufu 12:11)
• 7. Ulinzi: mara nyingi tunaona wazi wazi ulinzi wa Mungu kwetu, lakini hakuna mahali imeahidiwa
kuwa kwa wakati huu nguvu ya uharibifu haitakuwepo kabisa. Lakini katika wakati ujao Mungu ana
ahidi ulinzi (Isa 54:17)
• 8. Hukumu ya waumini: hata saa waumini wana hukumiwa (Yn 15:2, 1 Kor 11:30) lakini haitaishia
hapo bado ipo itakayo kuja (2 Kor 5:10)
• 9. Hukumu ya wenye dhambi : hata sasa huku yao tayari wameshatenganishwa na Mungu, pia
kuna matokeo ya dhambi zao kama hukumu ya dhambi. Lakini huku kuu inakuja (Ufu 20:12-13, Lk
16)
• 10. Hukumu ya shetani: shetani alishahukumiwa kwa kutupwa chini (Lk 10:18b-19) lakini pia
Kalvari alihukumiwa (Yn 12:31) lakini bado hajahukumiwa jumla (Efe 2:2) amehukumiwa kwa
kiwango fulani (Eze 28:11-19)
• 11. Mapenzi ya Mungu: ufalme wa MUNGU upo na kwa kiasi fulani mapenzi yake yapo lakini
hayajakua kwa ukamilifu ndio maana bado tunaomba (Mt 6:10)
SURA YA TISA
KANUNI YA MIFANO
• Tambua somo moja katika mfano: tambua muktadha wa kihistoria na
milima ya hoja za mafumbo.
• 1. ASILI YA MIFANO: ilikujua asili ya mifano lazima tujibu maswali ya
fwatayo.
• A.mfano ni nini?: ni hadithi fupi, rahisi na yenye maana ya kiroho. B.
kwanini Yesu alifundisha kwa mifano:
• 1. kwa sababu ya usalama: kwakuwa alikuwa aki laani mafarisayo na
wenye mamlaka alitakiwa kutumia lugha ambayo wasingeweza
kumshitaki. 2. alihitaji kufananisha ukweli: njia nzuri ya kujifunza ni
kuhusisha kitu na kingine, ukweli mpya unapaswa kujengwa juu ya
ukweli wa zamani. 3. kwa sababu inashinda pingamizi za watu: mfano
alio pewa Daudi na Nathani ilikuwa njia ya kumfanya Daudi asiwe na
pingamizi pindi atakapo ambiwa makosa yake. (2 sam 12:1-4) 4.
alifundisha kwa mifano kama aina ya hukumu: waliifanya mioyo kuwa
mizito, walipewa neno lakini hawakutaka kusikia kanuni ya mbinguni ni
“tumia au uipoteze” (Mt 13:10-15)
SURA YA TISA
KANUNI YA MIFANO
• C. Jinsi Wengine Wanatumia Mifano Kwa Kuifanya Kuwa Mafumbo (Kuifanya Iwe
Ya Kiroho Zaidi): kufanya mfano kuwa fumbo ni kosa kubwa sana, usifanye mfano
kuwakilish mambo tunayo fikiria.
• Hatua tatu za kutafasiri Mfano:
• A. Bainisha muktadha wa kihistoria wa Mfano: tambua hali ya asili ya huu mfano
kutolewa (jibu maswali; Yesu aliwatolea mfano kina nani, na kwanini aliutoa huo
mfano: katika mfano wa msamari (Lk 10:25-37) alimtolea nani= mwalimu wa
sheria, kwanini aliutoa: mwanasheria alikuwa akimjaribu Yesu, pia alitaka
kujihakikishia mwenyewe.
• B. Tambua milima michache ya hoja za mafumbo katika mfano: mfano katika
mfano wa “Msamaria mwema” kuna milima mitatu ya hoja: 1.mtu aliye jeruhiwa
(akiwakilisha wale wenye mahitaji) 2. Msamaria mwema (akiwakilisha jirani
anayejali) 3. kuhani na mlawiiiii (wakiwakilisha majirani wasio jali).
• C. Tambua somo kuu linaloelezwa na Mfano: usitafute somo zaidi ya moja katika
mfano. Katika “msamaria mwema” somo ilikuwa “kuwa jirani mwema kwa wale
walio na mahitaji”
SURA YA TISA
KANUNI YA MIFANO
• Tofauti ya kutafsiri na kutumia Mifano: kutafasiri mfano ni
kueleza maana yake, baada ya kutafsiri mfano mhubiri au
mwalimu anapaswa kuutumia.
• Mfano: “Msamaria mwema” mhubiri/mwalimu anapaswa
kutumia somo la mfano huu, kwa kugusia wa watu wenye
shida. Walio poteza mali zao, Wakristo wanatakiwa kuwa
majirani wema kwao.
• kufanya mfano kuwa fumbo ni hatari kwa sababu
hakuonyeshi maana asilia ya ujumbe ambao Yesu
alifundisha.
• Usifanye kuwa fumbo, tafasiri kwanza mfano kisha tumia
makala yenyewe.
SUYA YA KUMI
KANUNI YA UNABII
• Lengo ni kutafsiri unabii kwa roho ya
unyenyekevu, kwa kuzingatia muktadha wa
kihistoria,lugha ya mafumbo na sheria ya
utimilifu kwa wingi.
• vitabu na vifungu kuhusu unabii ni baadhi ya
sehemu ya Biblia ambazo ni vigumu sana
kuelewa.
SUYA YA KUMI
KANUNI YA UNABII
• Muhtasari
• Muhtasari wa miongozo mitano, kwa kutumia mfano wa Mathayo 24:4-8
• A. Muktadha wa Kihistoria
• jibu maswali haya.
• 1. ulitolewa kwa kina nani? kwa wanafunzi
• 2. lini? muda mfupi kabla ya kusulubiwa
• 3. kwanini? Yesu alikuwa amesema hekalu litabomolewa, wanafunzi
wake waka muuliza itakuwa lini, ipi dalili ya kuja kwako, na mwisho wa
dunia (Mt 24:3) hivyo alitoa unabiii kujibu maswali yao.
• B. Lugha ya mafumbo.
• -”uchungu wa kuzaa” hapa Yesu analinganisha wakati dhiki na utungu
wa mwanamke akizaa. hapa ni kuwa dhiki za 24:4-7 zinaonyesha dalili za
mwanzo wa wakati hup.
SUYA YA KUMI
KANUNI YA UNABII