3 HCWs

You might also like

Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 70

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

UTOAJI WA CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA


KORONA (UVIKO-19)

MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA


UTANGULIZI
 Kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi
vya Korona (UVIKO-19) na kuendelea kusambaa kwa
ugonjwa huu hapa nchini, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua
mbalimbali kudhibiti kuenea kwa ugonjwa hapa nchini
 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo
imeandaa mafunzo ya utoaji wa chanjo ya virusi vya
Korona kwa watoa huduma wa afya nchi nzima
1.UVIKO-19
 UVIKO-19 unasababishwa na kirusi cha SARS-CoV-2
Jamii ya “Coronaviruses vinavyosababisha magonjwa
aina mbalimbali yenye dalili kama za mafua

 Virusi hivi vina umbo la mviringo na vina bahasha yenye


asili ya mafuta iliyobeba protini aina tatu tofauti
(zimetofautishwa kwenye mchoro kwa rangi ya kijani,
nyekundu na njano)
1.UVIKO-19
 UVIKO-19 unasababishwa na kirusi cha SARS-CoV-2
Jamii ya “Coronaviruses vinavyosababisha magonjwa
aina mbalimbali yenye dalili kama za mafua
 Dalili za UVIKO-19 ni Pamoja na: Homa, Kikohozi,
Mafua, Kuchoka Mwili, Kukosa Pumzi, Maumivu ya
Misuli ya Mwili

 Mtu yeyote anaweza kupata maambukizi ya ugonjwa


huu. Watu walio na umri zaidi ya miaka 60 na wale
wenye magonjwa mengine mfano kisukari, presha n.k
wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu na
kupelekea kifo
CHANJO YA
UVIKO -19
LENGO LA UTOAJI WA CHANJO YA UVIKO

Yafuatayo ni malengo makuu ya utoaji Chanjo dhidi ya


UVIKO-19:
 Kupambana na Ugonjwa huu unaozuilika kwa chanjo
 Kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Korona
 Kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu
CHANJO DHIDI YA UVIKO-19
 Chanjo ya UVIKO-19 inazuia ugonjwa unaosababishwa na
virusi vya Korona (SARS-CoV-2) kwa kuufanya mwili
kutengeneza kinga dhidi ya ugonjwa huu
 Chanjo hizi ni salama na bora kwa ugonjwa wa virusi vya
UVIKO 19. Chanjo hii ni bora kwa sababu inauwezo wa
kumpatia mtu aliyechanjwa kinga ya kupata ugonjwa mkali
na kifo
 Hii ni muhimu hususan kwa wataalamu wa afya, watu
wenye umri wa miaka 18+, walio katika
mazingira hatarishi kama vile wazee , na watu wenye
magonjwa ya muda mrefu,
2.CHANJO DHIDI YA UVIKO-19
 Chanjo ya UVIKO-19 zinatengenezwa kwa kufuata
matakwa ya ubora, usalama na ufanisi kama dawa na
chanjo zingine
 Kuna aina kuu nne za utengenezaji wa chanjo za UVIKO-
19
 Tofauti zao ziko ikiwa wanatumia:
 Kirusi kizima au bakteria;
 Sehemu tu za chembechembe ambazo husababisha mfumo wa
kinga; au
 Vifaa vya maumbile tu ambavyo hutoa maagizo ya kutengeneza
protini maalum hutumika na sio kirusi chote
2.CHANJO DHIDI YA UVIKO-19
 Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia virusi
vilivyouwawa mf. Sinovac, Sinopharm

 Chanjo zenye kibebeo cha virusi aina ya


Adenovirus vilivyobebeshwa taarifa za
utengenezwaji wa protini mwiba mf.
AstraZeneca, Janssen, Sputnik V
2.CHANJO DHIDI YA UVIKO-19
 Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia protini
mwiba ya virusi vinavyosababisha UVIKO-
19 mf. Novavax, Abdala

Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia


messenger RNA iliyobeba taarifa za
utengenezwaji wa protini mwiba ya virusi vya
UVIKO-19 mf. Pfizer, Moderna
CHANJO DHIDI YA UVIKO-19

 Aina ya chanjo
zilizopendekezwa
nchini Tanzania ni:
– Pfizer, Moderna (mRNA)
– Sinovac, Sinopharm
(Inactivated vaccines)
– Johnson & Johnson
(Adenovirus vector)
MAJADILIANO

MAJADILIANO
3.UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA ZITOKANAZO NA CHANJO
YA UVIKO-19

 UTUNZAJI…..

 Chanjo za UVIKO-19 zinaweza kuhifadhiwa katika


makundi matatu; (takwimu za mpaka Desemba 2020)
1. Chanjo zinazoweza kuhifadhiwa kati ya nyuzi joto +2 mpaka +8 ºC
2. Chanjo zinazoweza kuhifadhiwa katika nyuzi joto -20 ºC
3. Chanjo zinazoweza kuhifadhiwa katika nyuzi joto -80 to -60ºC
3.UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 UTUNZAJI…..
 Kwa chanjo ziliko katika kundi la 1 na 2 hapo juu,
Mwongozo wa WHO pamoja na miongozo mingine ya
huduma za chanjo nchini itatumika kama ilivyo kawaida
 Kwa chanjo zilizo katika kundi la 3, uhifadhi wake
unahitaji uwekezaji mkubwa katika uhifadhi na uwezo
wa usafirishaji wa mnyororo wa baridi kali (Ultra Cold
Chain) Aidha unahitaji mafunzo ya ziada ya utunzaji wa
chanjo hizi
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 Usimamizi wa chanjo ya UVIKO-19 iliyohifadhiwa
katika nyuzi joto +2 mpaka +8 ºC
 Hakikisha chanjo pamoja na “diluents” zake zimewekwa pamoja na
kuwekewa alama. (bundling/labeling)
 Weka chanjo pamoja na “diluents” zake katika jokofu moja
 Fuatilia na urekodi joto mara kwa mara (> 2x / siku).
 Chunguza mabadiliko yoyote ya joto na inapokuwa tofauti urekebishe
haraka iwezekanavyo
 Tumia kontena au tray iliyo na lebo kwa vifuniko vya chanjo
visivyofunguliwa kuwezesha kuhesabu kwa urahisi
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19

 Usimamizi wa chanjo ya UVIKO-19 iliyohifadhiwa


katika nyuzi joto +2 mpaka +8 ºC
 Fuata kanuni ya “first manufacture/expiry, first out” kwa maana ya
kutumia kwanza chanjo zenye tarehe ya karibuni ya kumalizika muda
wake wa matumizi na / au zenye VVM II kupunguza upotezaji wa chanjo
 Rekodi na uondoe haraka chanjo zilizoharibika (wasted vaccines)
kulingana na miongozo ya kitaifa ya chanjo
 Pitia na huisha mpango wa dharura (contingency plan) ikiwa umeme
umekatika, au kuharibika kwa jokofu, au kuharibika kwa mnyororo baridi
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 Usimamizi wa chanjo ya UVIKO-19 iliyohifadhiwa
kwenye nyuzi joto -80 to -60ºC
 Pamoja na kanuni za ujumla za usimamizi wa mnyororo baridi
wa nyuzi joto +2 hadi + 8ºC, yafuatayo ni lazima kuzingatiwa
kwa chanjo zilizopo katika nyuzi joto -80 to -60ºC“Ultra Cold
Chain (UCC)”,:
– Fuata mwongozo uliopo maalum kwa usimamizi wa UCC,
– Tumia vifaa sahihi vya kujikinga (mfano. cryogenic gloves) kwa
wafanyakazi wanaosimamia UCC
– Fuata mwongozo na kutumia njia bora za kusimamia. na kutupa
nyenzo za mabadiliko ya awamu “(phase change material-PCM)’.
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19

 Mambo ya kuzingatia wakati wa kusafirisha chanjo


za UVIKO-19
 Ainisha eneo la kutolea chanjo na muda wa kuangalia joto la chanjo
 Tathmini hatari inayoweza kutokea na ucheleweshaji wa huduma
kutokana na sababu mbalimbali (Mfn. hali ya hewa), na weka mkakati wa
kupunguza hatari hizo
 Hakikisha una usafiri wa kuaminika na fedha za kutosha kwa ajili ya
mafuta kama yatahitajika
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19

 Mambo ya kuzingatia wakati wa kusafirisha chanjo


za UVIKO-19
 Beba chanjo kwa mfumo wa ‘Bundling” wakati wa kupeleka na
hakikisha vifaa vyote vinapatikana wakati wote wa kuchanja
 Hakikisha nyaraka za takwimu zinazohitajika zimeandaliwa vizuri na
zinapatikana kabla ya kuondoka
 Kamwe usisafirishe dozi ambazo zimefunguliwa (open multi dose
vials)
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 USAFIRISHAJI
 Usafirishaji wa chanjo ya UVIKO-19 inayohitaji nyuzi
joto +2 hadi +8 ºC
 Tumia masanduku ya kusafirisha chanjo yaliyopendekezwa
na vifurushi vya kupoza vya kutosha na vilivyoandaliwa
vizuri
 Fuatilia hali ya joto ya chanjo, ikiwezekana tumia “data
loggers”, kwani hii inaruhusu ufuatiliaji katika kipindi chote
cha usafirishaji na kupakua data mwishoni mwa safari
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 Usimamizi wa chanjo za UVIKO-19 zilizofunguliwa
 Mara kwa mara angalia maelezo kuhusu “Multi Dose Vial
Policy” (MDVP) ya chanjo husika
 Kama tahadhari ya kudumisha usalama na ubora wa chanjo,
yafuatayo yanapendekezwa hadi habari zaidi zipatikane:
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19

 Kwa chanjo zilizofunguliwa, ikiwezekana, tumia “vaccine


carrier” tofauti na chanjo ambazo hazijafunguliwa na hakikisha
kuna kifaa cha kufuatilia hali joto
 Chanjo zote zilizofunguliwa (za kuchanganya na zisizo za
kuchanganya) zinapaswa kutupwa masaa 6 baada ya
kufunguliwa au mwisho wa huduma ya uchanjaji; au yoyote
kati ya hizo ambayo itatangulia
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 Usitumie chanjo zilizofunguliwa ikiwa imevuka hali joto
inayohitajika.
 Kamwe usiweke chanjo zilizofunguliwa sehemu yenye joto
kali, mwanga au jua
 Kamwe usirudishe chanjo zilizofunguliwa kwa matumizi
– Aangalizo; Chanjo zilizofunguliwa zisitumike baada ya masaa sita
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA KWA CHANJO ZA UVIKO-
19
 Kurudisha Vifaa “Reverse Logistics”
 Kurudisha vifaa (Reverse logistics) ni mchakato wa kuchukua chanjo
ambazo hazijatumiwa kwa lengo la kuziondoa kwenye matumizi au
kutumia tena
 Sababu za kurudisha vifaa ni pamoja na:
 Uhitaji wa kupeleka chanjo kwenye maeneo mengine yenye hatari zaidi ya ugonjwa
(UVIKO-19)
 Kurudisha chanjo isiyotumika kwenye ngazi ya juu (wilayani/mkoani/taifa) mwishoni
mwa zoezi la uchanjaji (ikiwa inafaa)
 Wakati wa mapumziko ya kampeni au kusitisha uchanjaji kwa muda
 Kusimamisha huduma ya chanjo kwa sababu nyingine yoyote
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA ZITOKANAZO NA
CHANJO ZA UVIKO-19
 Usimamizi wa taka hatarishi katika kituo cha kutolea
huduma
1. Utupaji wa Sindano
 Tumia sindano za kuzima kiotomatiki “auto-disabled syringes(AD syringes) na uzitupe kama taka
hatarishi.
 Bila kurudisha sindano “recapping”, tupa sindano iliyotumika ndani ya makasha maalum. (Safety
Box)
 Usijaze makasha ya taka zaidi ya robo tatu ya uwezo wake au hadi kwenye mstari mwekundu
uliopo kwenye kasha.
 Hakikisha kasha limeandikwa vyema na alama ya vitu vya kuambukiza.

 Funga kisanduku cha usalama kabla ya kuipeleka sehemu maalumu ya kuhifadhia taka
3. UHIFADHI, UTUNZAJI, USAFIRISHAJI, NA USIMAMIZI WA TAKA ZITOKANAZO NA
CHANJO ZA UVIKO-19

2. Utupaji wa vichupa vya chanjo


 Weka vichupa vya chanjo vilivyotumika; chanjo ambazo hazijafunguliwa
na zilizomaliza muda wake wa matumizi (expired) na chanjo zilizopata
joto kwenye mfuko mwekundu wa taka, au kwenye chombo cha
biohazard
 Vichupa vya chanjo vilivyopasuka viainishwe kama taka hatarishi
 Hakikisha mifuko / makontena yamewekewa alama sahihi ya vitu
vinavyoambukiza.
 Funga vyombo kabla ya kusafirishwa hadi kwenye eneo la kushughulikia
taka
MAJADILIANO

MAJADILIANO
4.UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO

1. Usafi wa mikono: tumia kitakasa mikono au maji safi yotiririka


na sabuni.
2. Zingatia ustaarabu wa chafya au kukohoa.
3. PPE: vaa barakoa
4. Tumia njia salama za utupaji wa taka na sindano
5. Zingatia usafi wa mazingira
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
1. Usafi wa Mikono:
 Watoa huduma za chanjo wanapaswa kuwa na mikono safi
wakati wote wakitoa huduma;
 kabla ya kuvaa na kuvua PPE (k.v. barakoa)
 kabla ya kuandaa chanjo
 kila baada ya kutoa huduma ya chanjo kwa mteja
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO

 Matumizi ya “gloves”
 Haishauriwi kutumia “gloves” wakati wa kutoa chanjo za
ndani ya misuli isipokuwa kama kuna majeraha
 Kama zikitumika hazibadilishi umuhimu wa kunawa mikono
baada ya kila huduma ya uchanjaji
 Haishauriwi matumizi ya vitakasa mikono ukiwa umevaa
“gloves
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
2. Matumizi ya Barakoa
 Wakati wa kutoa huduma za chanjo barakoa zifuatazo
zinashauriwa
 Barakoa ya matibabu (medical mask) - kwa mfanyakazi wa afya
 Barakoa ya matibabu au ya kitambaa kwa mteja anayepata huduma
ya chanjo

 Hakikisha unavaa barakoa muda wote wa kutoa huduma za


chanjo
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Hatua sahihi ya uvaaji na utoaji wa barakoa

Uvaaji:

Utoaji:
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Uandaaji wa huduma ya utoaji chanjo
 Ifahamishe jamii na vikundi lengwa mahali na muda wa kutoa
chanjo.
 Andaa eneo salama la kutoa huduma ya chanjo na uhakikishe
una idadi ya kutosha ya:
 Chanjo na vifaa vyake
 Vifaa vya kutosha vya mnyororo baridi
 Sindano
 Barakoa na vifaa vya PPE
 Makasha ya takataka (sefety box)
 Vifaa vya kuchukulia taarifa
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Uandaaji wa sehemu ya kutolea
 Hakikisha maingira ya kutolea chanjo ni safi
 Hakikisha kuna hewa ya kutosha eneo la huduma ya chanjo
 Fungua madirisha na milango iwapo eneo la huduma ya chanjo ni ndani. Ikiwa
nje,chagua eneo lenye hewa ya kutosha.
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Uandaaji wa sehemu ya kutolea chanjo:
 Hakikisha angalau umbali wa mita 1 katika pande zote kati ya mtu na
mtu (Physical distancing)
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Zuia mikusanyiko kwa wanaopata huduma
 Chunguza wanaokuja kupata huduma ya chanjo iwapo
wana magonjwa ya njia ya hewa kabla ya kuwapatiwa
huduma ya chanjo
 Weka kikomo cha watu unaotarajia kuwachanja ili
kupunguza mikusanyiko na watu kusubiri kwa muda
mrefu kupatiwa chanjo
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Mtiririko wa wateja na mpangilio wa ukaaji wakati wa
uchanjaji
 Hakikisha kuna njia moja ya wateja kuingia (one-way flow) kwenye eneo la
uchanjaji
 Hakikisha unakaa kwa upande na sio ana kwa ana wakati wa utoaji wa huduma za
chanjo
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
Mtiririko wa Utoaji wa Huduma za Chanjo
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
 Utoaji wa chanjo za ndani ya misuli (Intramuscular
injection)
 Safisha mikono kabla na baada ya huduma ya chanjo kwa maji tiririka na sabuni.
 Shikilia sindano ya AD na vidole, na kidole gumba upande wa bomba wakati
sindano ikiangalia juu
 Nyosha taratibu ngozi kwa mkono mwingine na sukuma sindano haraka kwa
pembe ya 90 ° chini kupitia ngozi kwenye misuli
 Sukuma plunger vizuri, usisogeze sindano chini ya ngozi
 Vuta sindano haraka na vizuri kwa pembe sawa na ilivyoingia
 Tupa sindano ndani ya safety box
UTOAJI WA HUDUMA YA CHANJO
MAJADILIANO

MAJADILIANO
5.UFUATILIAJI WA MAUDHI YATOKANAYO NA
CHANJO YA UVIKO-19 (AEFI)
 Maudhi yatokanayo na chanjo ni tukio la mabadiliko
kufuatia huduma za chanjo (AEFI) ambayo:
 Hufuata baada ya huduma ya chanjo
 Sio lazima kuwa na uhusiano wa sababu na matumizi ya chanjo
 Inaweza kuwa dalili mbaya ambayo mpokeaji wa chanjo analalamika
 Inaweza kuwa mabadiliko yasiyokuwa ya kawaida ya maabara, ishara
au ugonjwa uliogundulika na watumishi wa afya kutoka kwa mteja wa
aliyepata chanjo
UFUATILIAJI WA MAUDHI YATOKANAYO NA
CHANJO YA UVIKO-19 (AEFI)
 Sababu/aina za maudhi yatokanayo na chanjo

1. Maudhi yatokanayo na bidhaa zilizo ndani ya chanjo (Vaccine product-related reaction):

Husababishwa na chanjo kwa sababu moja au zaidi kutokana na bidhaa iliyo ndani ya chanjo

2. Maudhi yatokanayo na changamoto inayohusiana na kasoro ya chanjo (Vaccine quality defect-related


reaction):

Husababishwa na chanjo kwa sababu ya kasoro moja au zaidi ya ubora wa chanjo husika au kifaa chake cha
uchanjaji kama inavyotolewa na mtengenezaji

3. Maudhi yanayohusiana na makosa ya uchanjaji (Immunization error-related reaction):

Husababishwa na utunzaji usiofaa wa chanjo, matumizi au usimamizi


4. Maudhi yatokanayo na wasiwasi wa chanjo (Immunization anxiety-related reaction):

Yanayotokana na wasiwasi juu ya chanjo na hofu ya sindano

5. Tukio la kubahatisha:

Tukio linalotokea baada ya chanjo lakini halisababishwi na chanjo au mchakato mzima wa uchanjaji
MAUDHI MALIMBALI YATOKANAYO NA
CHANJO ZA UVIKO-19 (AEFI)
 Kama chanjo yoyote ilivyo, chanjo za UVIKO-19 zinaweza kusababisha athari chache, za muda mfupi, kama
vile homa ya kiwango cha chini, maumivu au ngozi kuwa nyekundu eneo ulipochomwa sindano.

 Athari hizi ni za kawaida na huisha baada ya siku chache

 Madhara makubwa au ya kudumu ya chanjo yanawezekana lakini ni nadra sana kutokea.

 TMDA inaendelea kufuatilia usalama wa chanjo hizi ili kuangalia madhara yanayoweza kujitokeza baada ya
matumizi ya muda mrefu kwa lengo la kulinda afya ya jamii
UFUATILIAJI WA MAUDHI YATOKANAYO NA
CHANJO YA UVIKO-19 (AEFI)
Fomu ya kuripoti maudhi yatokanayo na chanjo
UFUATILIAJI WA MAUDHI YATOKANAYO NA
CHANJO YA UVIKO-19 (AEFI)
 Aina za maudhi ya kutolea taarifa
 Toa taarifa/ripoti ya maudhi yote ambayo yameletwa kwako.
 Jaza fomu za kuripoti na uzitume kwa msimamizi wako.
 Jaza taarifa zote zinazopatikana na kwa usahihi iwezekanavyo.
 Toa taarifa/ripoti ya maudhi ambayo sio mabaya kulingana sera ya
nchi ya kutoa taarifa
 Ikiwa kuna maudhi makubwa, mjulishe msimamizi wako na/au mtu
anayehusika na kushughulikia maudhi mara moja (kwa simu) na
ujaze fomu ya kuripoti ndani ya masaa 24
UFUATILIAJI WA MAUDHI YATOKANAYO NA
CHANJO YA UVIKO-19 (AEFI)
MAJADILIANO

MAJADILIANO
6. TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
 Uhifadhi na ufuatiliaji wa takwimu husaidia
yafuatayo:
 Hutoa uthibitisho wa kupata huduma ya chanjo
 Hutumika kufuatilia maendeleo na utumiaji wa chanjo
 Hutoa habari za usimamizi wa chanjo na usambazaji
 Inaarifu ufanisi na usalama wa chanjo kupitia ufuatiliaji
wa maudhi yatokanayo na chanjo (AEFI)
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
 Kadi ya chanjo itakuwa na taarifa zifuatazo:
 Maelezo binafsi na mawasiliano ya mpokeaji wa chanjo
 Chanjo aliyopata mhusika na dozi ikiambatana na:
 Tarehe ya chanjo
 Aina ya chanjo
 Dozi aliyopata
 Namba ya kundi la chanjo husika (batch/lot number)
 Jina la kituo
 Muhuri / saini
 Tarehe ya dozi inayofuata (ikiwa inafaa)
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
 Rekodi za kituo cha huduma zitakuwa na taarifa
zifuatazo:
 Taarifa za kadi ya chanjo pamoja na:
 Mawasiliano ya mtu aliyepewa chanjo
 Taarifa hatarishi za mtu aliyepewa chanjo (risk factors)
 Maudhi kufuatia chanjo (AEFI)
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
Tally sheet
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
Kadi/Cheti cha Chanjo
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
Rejesta ya Kituo
TAKWIMU NA UFUATILIAJI WA
CHANJO YA UVIKO-19
Repoti ya Mwezi
MAJADILIANO

MAJADILIANO
7.UHAMASISHAJI NA UELIMISHAJI
JAMII KUHUSU CHANJO YA UVIKO-19
Lengo ni kuhakikisha kuwa jamii inahamasika na kuelewa
umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19 ili kupata ushirikiano.
Katika kutekeleza hili, ni muhimu kufanya yafuatayo:
 Kuandaa na kuendesha mikutano ya uhamasishaji wa
chanjo ya UVIKO-19
 Kuelimisha jamii juu ya athari za UVIKO-19
 Kuandaa mipango ya uhamasishaji na uelimishaji katika
vijiji/vituo vya afya na kusimamia utekelezaji
UHAMASISHAJI NA UELIMISHAJI
JAMII KUHUSU CHANJO YA UVIKO-19
 Kutembelea nyumba kwa nyumba ili kuelimisha jamii
kuhusu umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19
 Kuwajulisha wahusika kuhusu tarehe za utoaji huduma za
chanjo katika kituo cha huduma
 Kutoa msaada au usimamizi wakati wa utoaji wa chanjo
 Ufuatiliaji wa uhamasishaji na uelimishaji wa jamii kuhusu
uelewa juu ya UVIKO-19
 Kutambua taarifa za uzushi/za kupotosha kuhusu chanjo
ya UVIKO-19 na kuzisahihisha au kuwasilisha ngazi ya juu
UHAMASISHAJI NA UELIMISHAJI
JAMII KUHUSU CHANJO YA UVIKO-19
 Vituo vya kutolea huduma ya chanjo ya UVIKO-19
viratibu na kupanga namna ya kuhamasisha na
kuwashirikisha watendaji wa kata/ vijiji (WEO/VEO),
viongozi wa dini na watu mashuhuri wa maeneo husika ili
kusaidia kuhamasisha jamii
 Pia inashauriwa kutumia njia za uhamasishaji
zinazotumika katika jamii husika mfano vituo vya redio
vilivyopo maeneo husika, megaphone, ngoma na filimbi
kuhamasisha jamii
UHAMASISHAJI NA UELIMISHAJI
JAMII KUHUSU CHANJO YA UVIKO-19
FOMU YA UHIARI WA KUPATA CHANJO DHIDI YA
UVIKO-19
FOMU YA UHIARI WA KUPATA CHANJO DHIDI YA
UVIKO-19
MAJADILIANO

MAJADILIANO
Asante Sana

You might also like