Sayansi Ya Virrusi Vya Korona Na Chanjo Ya Sinopharm

You might also like

Download as ppt, pdf, or txt
Download as ppt, pdf, or txt
You are on page 1of 14

Sayansi ya Virusi vya Korona

Virusi vinavyosababisha UVIKO-19


UVIKO-19 unasababishwa na virusi
aina ya Corona

Virusi hivi vina umbo la mviringo na vina


bahasha yenye asili ya mafuta iliyobeba
protini aina tatu tofauti (zimetofautishwa
kwenye mchoro kwa rangi ya kijani,
nyekundu na njano)

Protini iliyoonyeshwa kwa rangi ya kijani


inaitwa Spike (protini mwiba) husaidia
virusi hivi kunata na kuingia ndani ya
chembehai ya binadamu

Baada ya maambukizi, mwili wa


binadamu hutengeneza kinga mwili
dhidi ya protini mwiba zinazoweza
kuzuia maambukizi mapya
Sayansi ya Virusi vinavyosababisha UVIKO-19

Baada ya maambukizi, protini mwiba hujikunjua ili kuwezesha virusi kuingiza


vinasaba (RNA) ndani ya chembehai ya binadamu

Protini mwiba iliyokunjuka huficha makucha (epitopes) na kuufanya mwili


utengeneze kinga mwili hafifu dhidi ya virusi vya UVIKO-19

Chanjo za UVIKO-19 zimehandisiwa ili kutoruhusu protini mwiba kujikunjua, ili


makucha yake yote yaonekane, hali inayoufanya mwili utengeneze kinga mwili
nyingi zinazoulinda mwili dhidi ya maambukizi.

Kwa sababu hii, inashauriwa watu wachanjwe hata kama waliwahi kuugua ili wapate
kinga madhubuti, kwani kinga zao walizopata baada ya maambukizi halisia ni
dhoofu
Aina ya chanjo dhidi ya UVIKO-19

Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia virusi


vinavyosababisha UVIKO-19 vilivyouwawa, kwa mfano
Sinovac na Sinopharm

Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia kibebeo cha virusi


aina ya Adenovirus vilivyobebeshwa taarifa za
utengenezwaji wa protini mwiba, kwa mfano
AstraZeneca, Janssen na Sputnik V
Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia protini mwiba ya
virusi vinavyosababisha UVIKO-19 kwa mfano Novavax
na Abdala

Chanjo zilizotengezwa kwa kutumia messenger RNA


iliyobeba taarifa za utengenezwaji wa protini mwiba ya
virusi vya UVIKO-19, kwa mfano Pfizer na Moderna
Ubora na Usalama wa Chanjo za UVIKO-19
Ubora na usalama wa chanjo za Janssen
zilizoingia nchini ulihakikiwa na TMDA

Chanjo hizi zilipimwa kwa kutumia mitambo


ya kisasa inayoweza kuchambua vinasaba,
kupima homoni za uzazi, viatilifu, vijidudu,
vyuma nk. ili kuhakiki kama chanjo zina vitu
pekee vilivyoandikwa na waliozitengeneza

Uchambuzi wa vinasaba ulionyesha kuwa


chanjo zina kibebeo cha Adenovirus
kilichobeba protini mwiba ya UVIKO-19 kama
ilivyoandikwa na watenegenezaji na
hakukuwa na virusi au vijidudu vingine
vilivyopandikizwa

Halikadhalika, hakukuwa na homoni za uzazi,


viatilifu wala vyuma katika chanjo hizo na
hivyo zina ubora na ni salama
CHANJO YA SINOPHARM
UTANGULIZI

• Sinopharm ni moja ya chanjo za UVIKO-19 zilizoidhinishwa na


shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kwa ajili ya Mapambano ya
Ugonjwa huu wa UVIKO-19 tarehe 07 May 2021

• Chanjo hii ni mojawapo ya aina 5 za chanjo ambazo


zimeidhinishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kutumika nchini.

• Chanjo zingine zinazoruhusiwa kuingizwa na kutumika nchini ni


Janssen, Pfizer-BioNtech, Moderna, na Sinovac
UTENGENEZAJI WA CHANJO
YA SINOPHARM

• Chanjo hii imetengenezwa na Kampuni ya Kichina iitwayo


Beijing Institute of Biological Products Co., Ltd. (BIBP)

• Teknolojia iliyotumika kutengeneza chanjo hii inaitwa


Inactivated COVID-19 (VERO CELL) . Kimechukiliwa kirusi
halisi cha CORONA kikaingizwa kwenye Vero Cells (Seli
maalumu zilizotengenezwa kwa ajili ya kuotesha aina
mbalimbali za virusi kwenye Maabara za kisayansi) kisha
kikauawa kinasaba chake (inactivated) kwa kutumia dawa
iitwayo ß-propiolactone.
UTENGENEZAJI WA CHANJO
YA SINOPHARM

• Baada ya kuuawa, mchanganyiko wa


kirusi hicho cha SARS-CoV-2 antigen
unachujwa (Purified) kisha
kuchanganjwa kwenye kiongeza nguvu
ya chanjo (Adjuvant) kiitwacho
Aluminum Hydroxide tayari kwa
matumizi .
Utengenezwaji chanjo ya
Sinopharm…..
Utengenezwaji wa
Sinopharm……
• Mchanganyo huo wa Chanjo ya Sinopharm
unauwezo wa kuihadhiwa kwenye Jotoridi la 2-8°C
kwa miezi 24 (sawa na miaka 2)

• Mifano ya chanjo zilizotumia teknolojia ya kuua


kirusi au bakteria wasumbufu ni: Chanjo ya Polio,
Chanjo ya Kifua Kikuu (BCG), Chanjo ya Kuzuia
Kichaa cha Mbwa, Chanjo ya Mafua ya kirusi cha
Influenza,chanjo ya homa ya Ini aina A.
DOZI YA SINOPHARM
• Chupa moja ya chanjo ya Sinopharm imejazwa
dozi ya mtu mmoja.
• Chanjo hii inatolewa kwa mtu yoyote mwenye umri
kuanzia miaka 18 na kuendelea.
• Ili kupata kinga kamili ya UVIKO-19 kutoka kwenye
chanjo hii ya Sinopharm, NILAZIMA uchome dozi
mbili . Dozi ya kwanza siku ya kwanza na dozi ya
pili baada ya siku 21 (wiki 3) toka uchome dozi ya
kwanza.
DOZI YA SINOPHARM………
ANGALIZO:
•Dozi ya pili haitakiwi kuchelewa kutolewa zaidi ya siku
28 (wiki 4). Mtu akipitiliza zaidi ya siku 28, itamlazimu
kuanza upya zoezi hili la chanjo.

•Kinga kamili ya chanjo (Full vaccinated) inapatikana


baada ya Wiki mbili (Siku 14) toka umepata dozi ya
pili ya chanjo hii ya Sinopharm
MAUDHI MADOGO MADOGO
YA CHANJO HII YA
SINOPARM
 Dozi ya kwanza
• Maumivu ya sindano eneo ulilichomwa
• Kujisikia uchovu
• Maumivu ya Kichwa
 Dozi ya pili
• Hakuna maudhi yoyote yanaojitokeza baada
ya kuchoma dozi ya pili ya chanjo hii
NANI HARUHUSIWI KUPATA
CHANJO HII
• Mtu yoyote mwenye Mzio (Allergy) wa
mchanganyiko wowote wa dawa
uliotumika kutengeneza chanjo hii.

• Mtu yoyote Mwenye homa na joto ridi


lake lipo nyunzi 38.5 na kuendelea.

You might also like