Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 58

BARAZA LA MITIHANI

LA TANZANIA
TAARIFA KUHUSU UFAULU WA WANAFUNZI KATIKA
UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) NA
MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE)
MAMBO YATAKAYOWASILISHWA
• UTANGULIZI
• GREDI NA MADARAJA YA UFAULU
• USAJILI NA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI NA WATAHINIWA
• UFAULU WA JUMLA KATIKA UPIMAJI WA DARASA LA NNE (SFNA) NA
MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE)
• CHANGAMOTO ZILIZOATHIRI KIWANGO CHA UFAULU WA
WANAFUNZI NA WATAHINIWA
• MAONI YA BARAZA
• MAPENDEKEZO
UTANGULIZI

• Baraza la Mitihani linaendesha upimaji na mitihani katika


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
• Upimaji na Mitihani huendeshwa kwa mujibu wa sera ya elimu
na mitaala iliyoidhinishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
• Baraza lina mamlaka ya kuidhinisha vituo vya mitihani,
kutunuku vyeti na kuendesha mitihani ya nje ya nchi kwa
wanafunzi wanaosoma wakiwa Tanzania.
UTANGULIZI….Inaendelea
• Lengo la Kuendesha Upimaji (STNA na SFNA) ni kubaini ujuzi na
maarifa aliyopata mwanafunzi.
• Lengo lingine ni kubaini changamoto wanazopata wanafunzi na
kutoa maoni na mapendekezo yenye lengo la kuboresha
ufundishaji na ujifunzaji.
• Lengo la Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni kubaini umahiri
ambao wanafunzi walipata katika kipindi cha miaka saba (Darasa
la I – VII).
• Taarifa hizi hutumika kufanya uamuzi wa watahiniwa wenye
umahiri kuendelea na elimu au mafunzo ya ngazi ya juu
(Sekondari au Vyuo).
UTANGULIZI….Inaendelea

• Uchambuzi wa kina kuhusu takwimu za matokeo ya Upimaji wa


Kitaifa wa Darasa la Nne na Mtihani wa Taifa wa Kumaliza
Elimu ya Msingi kwa miaka minne (2019 – 2022) umefanyika ili
kubaini mwenendo wa ufaulu.
• Uchambuzi huu wa ufaulu wa wanafunzi/watahiniwa
umezingatia viwango vya ufaulu kwa mujibu wa Kanuni za
Mitihani za mwaka 2016.
GREDI NA MADARAJA YA UFAULU

• Uchakataji wa matokeo ya SFNA na PSLE unazingatia Gredi


ambazo ni A, B, C, D na E.
• Katika ngazi ya SFNA, Gredi A hadi D ni Gredi za ufaulu na
Gredi E ni feli.
• Katika ngazi ya PSLE, Gredi A hadi C ni Gredi za ufaulu na
Gredi D na E ni feli.
• Gredi na Madaraja ya ufaulu katika matokeo ya SFNA na PSLE
vimeoneshwa katika Jedwali Na. 1.
GREDI NA MADARAJA YA UFAULU….Inaendelea

Jedwali Na. 1: Gredi za Ufaulu kwa Upimaji wa Kitaifa wa


Darasa la Nne (SFNA) na Mtihani wa Kumaliza Elimu ya
Msingi (PSLE)
Mfiko wa Alama Mfiko wa Alama kwa
Gredi Masomo Sita Maelezo
kwa Somo
A 41 - 50 241 - 300 Bora
B 31 - 40 181 - 240 Nzuri Sana
C 21 - 30 121 - 180 Nzuri
D 11 - 20 61 - 120 Inaridhisha
E 0 - 10 1 - 60 Hairidhishi
USAJILI NA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI NA WATAHINIWA

• Takwimu za usajili na mahudhurio ya wanafunzi na watahiniwa


katika SFNA na PSLE, 2019 - 2022 zimebainishwa katika
Jedwali Na. 2.
………
USAJILI NA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI NA
WATAHINIWA….Inaendelea
Jedwali Na. 2: Usajili na Mahudhurio ya Wanafunzi na
Watahiniwa, SFNA, PSLE, FTNA na CSEE 2019-
2022
Waliofanya
Na. Ngazi Mwaka Waliosajiliwa
Idadi Asilimia
2019 1,786,729 1,666,154 93.25
2020 1,828,268 1,704,404 93.23
1. SFNA
2021 1,681,791 1,561,599 92.85
2022 1,718,896 1,592,600 92.65
2019 947,077 933,369 98.55
2020 1,023,950 1,009,586 98.60
2. PSLE
2021 1,132,084 1,108,023 97.87
2022 1,384,186 1,350,881 97.59
USAJILI NA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI NA
WATAHINIWA….Inaendelea
• Usajili wa wanafunzi katika ngazi ya SFNA ulishuka mwaka
2021.
• Katika ngazi ya PSLE usajili wa watahiniwa umeongezeka
kutoka watahiniwa 947,077 mwaka 2019 hadi 1,384,186 mwaka
2022 sawa na asilimia 46.15.
• Mahudhurio ya wanafunzi na watahiniwa katika SFNA na PSLE
yamekuwa yakipanda na kushuka.
• Katika PSLE mahudhurio yameshuka kutoka asilimia 98.55
mwaka 2019 hadi 97.59 mwaka 2022.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA PSLE

• Uchambuzi wa takwimu uliofanyika kuhusu ufaulu wa jumla


katika SFNA na PSLE ni kwa kipindi cha miaka minne (2019 -
2022).
• Uchambuzi huu umezingatia idadi na asilimia ya wanafunzi na
watahiniwa waliofanya Upimaji/Mtihani, waliofaulu na waliofeli
kwa kipindi husika.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
A. Ufaulu wa Jumla SFNA 2019 – 2022
Jedwali Na.3: Takwimu za Matokeo ya SFNA 2019-2022
WALIOFAULU (GREDI
A-D) GREDI A - C GREDI D GREDI E
WENYE
MWAKA
MATOKEO
IDADI % IDADI % IDADI % IDADI %

2019 1,665,863 1,531,120 91.91 1,154,748 69.32 376,372 22.59 134,743 8.09

2020 1,704,286 1,551,599 91.04 1,146,786 67.29 404,813 23.75 152,687 8.96

2021 1,561,516 1,347,554 86.30 973,574 62.35 373,980 23.95 213,962 13.70

2022 1,592,235 1,320,700 82.95 818,903 51.43 501,797 31.52 271,535 17.05
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Ufaulu wa wanafunzi katika SFNA umekuwa ukishuka mwaka
hadi mwaka kutoka asilimia 91.91 mwaka 2019 hadi asilimia
82.95 mwaka 2022.

• Ubora wa ufaulu umekuwa ukishuka ambapo idadi ya


wanafunzi waliopata gredi D na E imekuwa ikiongezeka kutoka
asilimia 22.59 hadi 31.52 na asilimia 8.09 hadi 17.05 katika
mwaka 2019 hadi 2022 mtawalia.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wasiomudu stadi
za KKK ni Manyara (4.27%), Mara (3.19%) na Rukwa (3.09%).
• Mikoa ya Dar es Salaam na Kagera ilikuwa na idadi ndogo zaidi
ya wanafunzi wasiomudu stadi za KKK ambao ni asilimia 0.02
na 0.15 mtawalia.
• Uchambuzi wa Ufaulu wa Jumla ulifanyika kwa masomo ya
Lugha (Kiswahili na English Language), masomo ya Hisabati na
Sayansi (Hisabati na Sayansi na Teknolojia) na masomo ya
Sanaa (Maarifa ya Jamii na Uraia na Maadili).
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
I. Masomo ya Lugha (Kiswahili na English Language)

Chati Na. 1: Ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya lugha mwaka 2019 - 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Katika somo la Kiswahili, mwaka 2019 hadi 2022 ufaulu
ulikuwa mzuri. Aidha, mwaka 2020 ufaulu ulikuwa mzuri zaidi
ambapo asilimia 90.09 ya watahiniwa walifaulu.
• Katika somo la English Language, ufaulu wa wanafunzi
ulikuwa ukishuka kuanzia mwaka 2019 mpaka 2022 mfululizo
kutoka asilimia 81.09 hadi asilimia 71.72.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
II. Masomo ya Sayansi Jamii (Maarifa ya Jamii na Uraia na
Maadili)

Chati Na. 2: Ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi; na
Uraia na Maadili mwaka 2019 – 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Ufaulu wa wanafunzi kwa somo la Maarifa ya Jamii na Stadi
za Kazi mwaka 2019 ulikuwa mzuri kwa asilimia 95.26.
• Mwaka 2019 hadi 2020 ufaulu kwa somo la Maarifa ya Jamii
na Stadi za Kazi ulipanda kwa asilimia 0.2.
• Mwaka 2020 hadi 2021 na mwaka 2021 hadi 2022 ufaulu
ulishuka kwa asilimia 4.26 na 6.35 mtawalia.
• Ufaulu kwa somo la Uraia na Maadili ulikuwa mzuri kwa
mwaka 2019 na 2020.
• Mwaka 2019 kwenda 2020 ufaulu uliongezeka kwa asilimia 1.5
na kupungua kutoka mwaka 2021hadi 2022.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
III. Masomo ya Sayansi na Hisabati

Chati Na. 3: Ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya Hisabati,


Sayansi na Teknolojia mwaka 2019 hadi 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Katika somo la Hisabati, kwa kipindi cha mwaka 2019 hadi
2022, ufaulu wa wanafunzi ulishuka mfululizo kutoka asilimia
74.02 hadi 49.70.
• Katika somo la Sayansi na Teknolojia, ufaulu ulikuwa ukishuka
kutoka mwaka mmoja hadi mwingine.
• Kutoka mwaka 2019 hadi 2020 ulipungua kwa asilimia 7.33 na
mwaka 2021 hadi 2022 ulipungua kwa asilimia 4.57.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
B. Ufaulu wa Jumla katika PSLE 2019 – 2022
Jedwali Na. 4: Matokeo ya PSLE 2019-2022
WALIOFAULU
GREDI C GREDI D GREDI E
WENYE (GREDI A-C)
MWAKA
MATOKEO
IDADI % IDADI % IDADI % IDADI %

2019 932,189 759,737 81.50 446,200 47.87 149,259 16.01 23,193 2.49

2020 1,008,307 833,672 82.68 465,307 46.15 151,559 15.03 23,076 2.29

2021 1,107,460 907,802 81.97 606,419 54.76 194,851 17.59 4,807 0.43

2022 1,348,073 1,073,402 79.62 720,267 53.43 265,892 19.72 8,779 0.65
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea

• Ufaulu wa watahiniwa katika PSLE umekuwa ukipanda na


kushuka ambapo ufaulu wa juu zaidi ulikuwa asilimia 82.68
mwaka 2020.
• Uchambuzi wa ufaulu ulifanyika kwa Masomo ya Lugha (Kiswahili
na English Language), Masomo ya Hisabati na Sayansi (Hisabati
na Sayansi na Teknolojia) na Masomo ya Sanaa (Maarifa ya
Jamii na Uraia na Maadili) mwaka 2019 hadi 2022.
• Uchambuzi wa somo la Uraia na Maadili umefanyika kuanzia
mwaka 2021 ambapo somo hili lilitahiniwa kwa mara ya kwanza.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
I. Masomo ya Lugha (Kiswahili na English Language)

Chati Na. 4: Ufaulu wa watahiniwa katika masomo ya Kiswahili na English


Language mwaka 2019 - 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Ufaulu katika somo la Kiswahili ulikuwa mzuri kuanzia mwaka
2019 hadi 2022 kwa watahiniwa kupata Gredi A-C.
• Ufaulu huo ulikuwa ukipanda kutoka asilimia 87.25 mwaka 2019
hadi asilimia 89.50 mwaka 2022.
• Kwa upande wa somo la English Language, ufaulu wa
watahiniwa ulikuwa wa wastani (kuanzia asilimia 53.21 hadi
57.24) kwa kipindi cha mwaka 2019 hadi 2021.
• Ufaulu huo ulishuka kwa kiwango kikubwa zaidi mwaka 2022
ambapo ufaulu wa jumla ulikuwa asilimia 29.39.
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA PSLE….Inaendelea
II. Masomo ya Sayansi ya Jamii (Maarifa ya Jamii na Stadi za
Kazi na Uraia na Maadili)

Chati Na. 5: Ufaulu katika masomo ya Uraia na Maadili; na Maarifa ya


Jamii na Stadi za Kazi mwaka 2019 - 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
• Kwa somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, kuanzia mwaka
2019 hadi 2022 ufaulu ulikuwa mzuri kwa watahiniwa waliopata
Gredi A - C.
• Ufaulu ulipanda kwa kiwango cha juu mwaka 2019 (83.50%) na
kushuka mwaka 2020 (81.73), na mwaka 2021 (77.61%) na
kupanda kwa asilimia 4.26 kwa mwaka 2022 ambapo ufaulu
ulikuwa asilimia (81.87%).
• Katika somo la Uraia na Maadili, ufaulu ulikuwa mzuri kwa miaka
yote miwili, kuanzia mwaka 2021 hadi 2022.
• Mwaka 2021 ufaulu ulikuwa asilimia 71.21 na mwaka 2022 ufaulu
ulipanda kwa asilimia 0.02 ambapo ulikuwa asilimia 71.23 .
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA
PSLE….Inaendelea
III. Masomo ya Sayansi na Hisabati

Chati Na. 6: Ufaulu katika masomo ya Sayansi na Teknolojia, na


Hisabati mwaka 2019 hadi 2022
UFAULU WA JUMLA KATIKA SFNA NA PSLE….Inaendelea
• Katika somo la Hisabati, kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 ufaulu
ulikuwa ukishuka mwaka hadi mwaka.
• Katika somo la Sayansi na Teknolojia, ufaulu kwa mwaka 2019
ulikuwa mzuri kwa asilimia 83.50, mwaka 2020 ulipungua kwa
asilimia 0.65 na kuongezeka asilimia 0.43 kwa mwaka 2021.
• Mwaka 2022, ufaulu ulishuka kwa asilimia 11.65 ikilinganishwa
na ufaulu wa mwaka 2021.
KAZI YA KIKUNDI

Katika makundi, jadili kisha wasilisha changamoto


zinazopelekea wanafunzi/watahiniwa kushindwa
kujibu maswali kwa usahihi. Eleza hoja 2 kwa kila
somo.
CHANGAMOTO ZILIZOATHIRI KIWANGO CHA
UFAULU WA WANAFUNZI NA WATAHINIWA
A. Kukosa Uelewa wa Dhana Mbalimbali za Somo Husika
Wapo wanafunzi na watahiniwa ambao hawakuwa na umahiri
katika mada zote, hivyo walijibu maswali kinyume na matakwa
ya swali katika upimaji/mtihani husika.
Wapo wanafunzi wasiomudu stadi za Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu (KKK) hivyo, kushindwa kujibu kabisa maswali
yaliyoulizwa.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kwa mfano, katika Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne 2022, somo


la English Language katika umahiri Mkuu wa Comprehend Oral
and Written Information, kiwango cha ufaulu kilikuwa hafifu
(25.63%).
Umahiri huu ulijumuisha maswali 2 (Swali la 1 na 5) katika upimaji
ambapo ulikuwa na uzito wa jumla ya alama 20.
Wanafunzi walikuwa na kiwango cha chini cha ufaulu kwa sababu
walikosa stadi za kusikiliza na kuandika.
Swali la 1 lilikuwa na sentensi 5 ambapo kila sentensi ilikuwa na
maneno manne zilizosomwa kwa wanafunzi ili waandike kwa usahihi
maneno wanayosomewa. Sentensi zilikuwa kama ifuatavyo:
CHANGAMOTO….Inaendelea

These eggs are broken.


He arrived late yesterday.
They come from America.
Elizabeth can speak English.
Our grandfather walks slowly.
 Kielelezo Na. 1 ni mfano wa jibu la mwanafunzi aliyeshindwa
kuandika kwa usahihi sentensi alizosomewa.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kielelezo Na. 1: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
Wapo wanafunzi walioshindwa kuandika neno lolote la
Kiingereza katika sentensi walizosomewa kama inavyoonekana
katika Kielelezo Na. 2.

Kielelezo Na. 2: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi


CHANGAMOTO….Inaendelea
Wapo wanafunzi walioandika kwa usahihi maneno katika
sentensi kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 3.

Kielelezo Na. 3: Sampuli ya jibu sahihi kutoka kwa wanafunzi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
• Katika PSLE 2022, umahiri wa Comprehend Oral and Written
Information ulikuwa na asilimia ndogo zaidi ya watahiniwa waliofaulu
(13.37%).
• Mtahiniwa alipaswa kuonesha uelewa wa jambo alilosomewa au
kusoma, kisha kujibu maswali kwa usahihi kulingana na jambo hilo.
Kwa mfano, swali la 45 lilikuwa;
“Anyone who will bring back the princess alive will marry her.” the king
announced. What made the king to give such a promise?
• Jibu sahihi lilikuwa, because he remembered what happened to his
wife/because he wanted his daughter back.
CHANGAMOTO….Inaendelea
• Watahiniwa waliotoa majibu yasiyo sahihi hawakuweza kuelewa
kifungu cha habari walichosomewa. Kielelezo Na. 4 ni sampuli
ya jibu lisilo sahihi katika swali hilo.

Kielelezo Na. 4: Sampuli ya jibu lisilo sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
• Katika somo la Uraia na Maadili (PSLE) 2022 swali lifuatalo
lilitoka katika umahiri wa kuheshimu Jamii na lilikuwa:
Rushwa ni miongoni mwa changamoto za maendeleo katika
taifa. Ni tunu zipi mbili za taifa zinaweza kutumiwa katika
kupambana na rushwa nchini Tanzania?
• Kielelezo Na. 5 kinaonesha sampuli ya jibu la mtahiniwa
aliyekosa maarifa ya kutosha juu ya dhana iliyotahiniwa.

Kielelezo Na. 5: Sampuli ya jibu lisilo sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
• Watahiniwa walioweza kujibu swali kwa usahihi walielewa
dhana kuhusu tunu mbili za Taifa zinazoweza kutumiwa
kupambana na rushwa nchini Tanzania kama inavyoonekana
katika Kielelezo Na. 6.

Kielelezo Na. 6: Sampuli ya jibu sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
• Katika somo la Hisabati (PSLE) 2022, swali la 41 lililopima
umahiri wa watahiniwa katika kufumbua mafumbo yanayohusu
uwiano sahili lilikuwa;
Bwana Nguvumali alinunua mbegu za mahindi kwa sh 1,600. Ikiwa
bei ya kilogramu 1.75 za mbegu za mahindi sokoni ni sh 11,200, je,
alipata kiasi gani cha mbegu za mahindi?
Kielelezo Na. 7 kinaonesha jibu lisilo sahihi la mmoja wa
watahiniwa.

Kielelezo Na. 7: Sampuli ya jibu lisilo sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
• Majibu sahihi ni kama yanavyoonekana katika Kielelezo Na. 8.

Kielelezo Na. 8: Sampuli ya jibu sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
B. Kujibu Kinyume na Matakwa ya Maswali Yanayoulizwa au
Kutokujibu Baadhi ya Maswali
• Wapo wanafunzi na watahiniwa wanaojibu maswali bila kufuata
maelekezo yaliyobainishwa.
• Wapo wengine ambao hawaandiki jibu lolote.
• Kwa mfano katika somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi
(PSLE) 2022 swali la 45 lilikuwa;
Utamaduni ni uhai, utambulisho na tunu ya taifa inayorithishwa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Je, mambo yapi mawili
yanaathiri utamaduni wa jamii za kitanzania?
CHANGAMOTO….Inaendelea
• Watahiniwa walioshindwa kujibu swali hilo kwa usahihi
kutokana na kushindwa kuelewa mahitaji ya swali ni kama
inavyoonekana katika Kielelezo Na. 9.

Kielelezo Na. 9: Sampuli ya majibu yasiyo sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
C. Watahiniwa Kukosa Stadi ya Kukokotoa na Kutumia
Kanuni Mbalimbali
• katika somo la Hisabati SFNA 2022 swali la 3 (d) lilikuwa:
Joel alinunua redio na kuiuza kwa shilingi 60,500/=. Ikiwa alipata
faida ya shilingii 20,000/=, je aliuza kwa shilingi ngapi?’
• Wapo wanafunzi walioshindwa kuunda mlinganyo ili
kukokotoa jumla ya fedha iliyotumika kununulia redio hiyo.
Mfano mmojawapo wa majibu yasiyo sahihi umeoneshwa katika
Kielelezo Na. 10.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kielelezo Na. 10: Sampuli ya jibu llisilo sahihi.


• Katika Kielelezo Na. 10, mwanafunzi alijumlisha gharama ya
kununua redio na faida, badala ya kukokotoa tofauti ya
fedha hizo ili kupata gharama ya kununua redio kama
inavyoonekana katika Kielelezo Na. 11.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kielelezo Na. 11: Sampuli ya jibu sahihi.


CHANGAMOTO….Inaendelea
D. Watahiniwa Kukosa Umahiri wa Lugha
• Wanafunzi/Watahiniwa katika masomo mbalimbali
yanayofundishwa kwa kutumia lugha ya Kiingereza hushindwa
kujenga hoja kutokana na kutokuwa na umahiri wa kutosha
katika matumizi ya lugha ya Kiingereza.
• Changamoto hii husababisha wanafunzi kuandika sentensi
zisizo na mantiki katika kujibu maswali, kushindwa kujenga
hoja na kufanya tathmini ya jambo kutokana na swali
aliloulizwa na wakati mwingine kutumia lugha ya Kiswahili.
CHANGAMOTO….Inaendelea
• Kwa mfano, katika somo la English Language PSLE 2022
swali la 43 lililotokana na kifungu cha habari lilikuwa:
Imagine Maguvu was caught by the robbers in the process of
rescuing the princess. What do you think would happen to him?
• Baadhi ya watahiniwa waliandika maneno waliyoyanakili kutoka
katika kifungu cha habari walichokisoma. Maneno hayo
hayahusiani na swali lililoulizwa.
• Kielelezo Na. 12 ni sampuli ya majibu yasiyo sahihi kwa swali
hilo.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kielelezo Na. 12: Sampuli ya jibu lisilo sahihi.


• Katika Kielelezo Na. 12, mtahiniwa aliandika maneno aliyoyanakili kutoka
katika kifungu cha habari alichokisoma kwani alishindwa kujieleza kwa
kutumia lugha ya Kiingereza.
• Kielelezo Na. 13 ni sampuli ya jibu sahihi kwa swali hilo.
CHANGAMOTO….Inaendelea

Kielelezo Na 13: Sampuli ya jibu sahihi.


MAONI YA BARAZA

• Baraza la Mitihani la Tanzania lilibaini kuwa, mambo yaliyochangia


wanafunzi na watahiniwa wa Shule za Msingi kutokufanya vizuri
katika Upimaji na Mitihani ya Taifa kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 ni
kama ifuatavyo:
 Wanafunzi na watahiniwa kutokuwa na maarifa ya msingi au
ufahamu wa dhana mbalimbali zilizotahiniwa kwa mujibu wa
mtaala wa ngazi husika.
 Kukosa stadi ya kukokotoa na kutumia kanuni mbalimbali.
 Kukosa umahiri wa lugha ya Kiingereza.
 Kushindwa kubaini matakwa ya swali.
• Changamoto hizi zikitatuliwa, ufaulu wa wanafunzi na watahiniwa
unaweza kuongezeka.
HITIMISHO
• Kati ya masomo sita (06) yaliyofanyiwa upimaji ngazi ya SFNA,
somo la Hisabati lilikuwa na ufaulu wa chini wa asilimia
49.70 mwaka 2022 ikilinganishwa na masomo mengine
ambayo ufaulu wake ulikuwa kati ya asilimia 69.00 na 95.50.
• Katika masomo sita (06) yaliyotahiniwa katika PSLE, somo la
Hisabati lilikuwa na kiwango cha chini cha ufaulu wa asilimia
53.29 na 57.63 mwaka 2022 na 2021 mtawalia.
• Pia, somo la English Language lilikuwa na kiwango cha chini
cha ufaulu wa asilimia 29.39 na 48.02 mwaka 2022 na 2021
mtawalia. Masomo mengine yalikuwa na ufaulu wa kuanzia
asilimia 62.90 na 89.50.
KAZI YA KIKUNDI

Katika makundi, jadili kisha toa na


kuwasilisha mapendekezo matatu kwa kila
somo ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji
wa masomo hayo.
MAPENDEKEZO

• Baraza la Mitihani la Tanzania linashauri yafuatayo ili kuboresha


ufaulu wa wanafunzi na watahiniwa kwa wakati ujao:
Katika masomo ya Lugha, walimu watumie vifungu vya
habari (masimulizi) vilivyopo katika vitabu vya kufundishia
katika kuwawezesha wanafunzi kupata umahiri mahususi
husika.
Vifungu hivyo vya habari vitumike kama nyenzo ya kutolea
ngazi za juu za stadi katika maeneo yote ya lugha kama
yalivyobainishwa katika Muhtasari husika.
Katika vitabu vya kufundishia, vifungu hivyo vimewekwa
mwanzo wa kila umahiri mahususi unaoenda kufundishwa.
Njia hii itawapa wanafunzi uwezo wa kusoma na kusikiliza
kwa ufahamu.
MAPENDEKEZO….Inaendelea
Katika somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi, walimu
wawaalike wataalamu wa masuala ya ushirikiano wa
kimataifa ili waeleze kwa kina malengo, faida na changamoto
za kuanzishwa kwa Jumuiya za Kikanda, Afrika na Kimataifa.

 Aidha, katika ufundishaji wa matukio ya kihistoria, walimu


watumie zana kama vile picha katika kuonesha nyakati
mbalimbali na vifaa vilivyotumika au matukio yaliyotokea
katika nyakati hizo.
MAPENDEKEZO….Inaendelea
Katika somo la Hisabati, walimu wawawezeshe wanafunzi
kuunda kanuni mbalimbali za kimahesabu na kuzitumia
katika kukokotoa hesabu hususani katika eneo la maumbo.
 Aidha, walimu watumie vitu au matendo halisi katika kufundisha
ili kurahisisha uelewa wa dhana mbalimbali kwa wanafunzi.

Katika somo la Sayansi na Teknolojia, walimu wawaongoze


wanafunzi kufanya ziara za kimasomo kwa ajili ya kujifunza
misingi mbalimbali ya Sayansi na Teknolojia. Kusoma kwa
vitendo kutawasaidia wanafunzi kujifunza na kutumia dhana za
kisayansi na kiteknolojia kwa urahisi zaidi na hivyo kuwa mahiri
katika maeneo hayo.
MAPENDEKEZO….Inaendelea
Katika somo la Uraia na Maadili, walimu watumie mbinu
shirikishi kujenga umahiri kwa wanafunzi.
Mbinu kama vile kujifunza kwa majadiliano, igizodhima,
picha, michoro na hadithi fupi vitawawezesha wanafunzi
kuelewa umuhimu wa kudumisha amani na umuhimu wa
Jumuiya za kikanda na kimataifa
MWISHO

ASANTENI KWA KUSHIRIKI

You might also like