Download as pptx, pdf, or txt
Download as pptx, pdf, or txt
You are on page 1of 72

UTANGULIZI WA

FASIHI YA KISWAHILI
KF 102

Prof. Aldin K. Mutembei (PhD)


Ofisi # 317 Jengo la Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, CKD
LENGO KUU na MUHIMU
Kuhusu Usomaji katika CKD

Kuwajibika na Kuondoa woga


Mambo ya Jumla kuhusu
Maisha ya Chuo Kikuu
• Wajibu wako kama Mwanafunzi
• KUSOMA:
→Usomaji wa binafsi;
→Nguvu ya Makundi;
→Kujisomea Maktaba (Majengo);
→Maktaba za Mkondoni.
Maisha ya Chuo…
• ZINGATIA UMUHIMU HUU:
Andika vizuri, kwa uwazi, na moja kwa moja
Uwe na mwonekano tofauti kama Mwanachuo
Kuna Mtu wa Mitaani (lugha, mavazi, ujengaji
hoja), na Mwana CKD
• Huwezi kusoma kwa makini hadi
Ujisake: Wewe ni Nani?
Maisha…MTU MWENYEWE
• Falsafa ya Sufi Bayazid
• Kujitambua, Kujithamini, Kujipenda (LUGHA,
mavazi na FIKRA)
• Unajitambua? Unaweza kumtambua mwingine.
• Unajithamini? Unaweza kumthamini mwingine.
• Unajipenda? Unaweza kumpenda mwingine
Maisha…TUNAVYOKUTARAJIA UWE

• Umekuja kusoma na Kuelimika.


Tunataka hatimaye kuona matunda ya Elimu Yako
• Umekuja kuhesabika kuwa miongoni mwa
wachache wenye bahati
Tunataka kuiona bahati hiyo
• Itumie bahati hiyo bila kuichezea
• Umekuja Kusoma na Kufaulu
Maisha…CKD Kikujengee UZALENDO:

• Uzalendo na Kupenda nchi yako. Kuwa tayari


kuipigania na Kuitetea
• Uzalendo wa Kupenda yaliyomo katika nchi
yako, kuyatangaza na kuyasimamia.
• Uzalendo wa kupenda lugha yako: kuitumia na
kuieneza.
• Ikiwa huwezi kujipenda, na kuwapenda
wengine, ni vigumu kupenda nchi yako.
Mihadhara ya Chuo na Usomaji
• Hujengwa kwa KUSIKILIZA na kuandika
kilichozungumzwa
• Sio kunakili tu yaliyoandikwa (notes)
• Sio kutoa tu nakala (photocopy)
• Jenga, uwezo wa
– kusikiliza, kutambua kilichosemwa
– Kuchukua unachoona kinafaa
– Kuandika yale yatakayokukumbusha kilichosemwa
• Kamwe usikariri. Ni makosa makubwa sana
kukariri, bila kuelewa inachosemwa. Hakikisha
hutoki nje ya darasa bila kuelewa kilichosemwa.
UHURU WA MAWAZO
• Jenga hali ya kujiamini.
• Jenga uwezo wa kutoa hoja.
• Anza taratibu, na jizoeze kutoa hoja.
• Usijitetee kama huna cha kujitetea, ila
• Usinyamaze ikiwa unalo la kusema.
• Kupinga kwa hoja kwa nia ya kukuza maarifa ni
tabia inayotarajiwa kwa msomi.
• Msomi mzuri hutoa mawazo yake bila woga na
kuwa tayari kukosolewa au kukosoa wenzake.
Uhuru wa Mawazo…
• Mwalimu si adui, ni rafiki anayetaka kupitia
kwake upande ngazi, ufike juu. Juu sana.
• Walimu wazuri huwaruhusu wanafunzi
kuwapita, na hujivuna pale wanapowaona
wanafunzi wao wakiwa katika nafasi
mbalimbali za juu: Kimasomo, Kimapato,
Kimaisha n.k
• Ninawatia moyo na kuwakaribisha katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
• Mmekuja kusoma, kuelewa na kufaulu!
Kazi ya Nyumbani
• Kila mtu asome na kutafakari Makala ya
mwaka 1971: Matumizi ya Kiswahili Nchini,
Shuleni na Vyuoni (J.K. Kiimbila) Katika
Kichocheo cha Uchunguzi wa Kiswahili, uk. 60
-69. Makavazi.
• Linganisha mawazo hayo ya zaidi ya miaka 40
na mawazo ya sasa. Je kuna kipi kipya?
– Novemba 21, 2018
Mihadhara: UTANGULIZI…
• Tunajifunza somo hili ili tugundue nini?
• Sanaa ni njia ya mwanadamu kujieleza
• Fasihi kama kioo cha jamii – kinaioneshaje
jamii?
• Lugha kama kioo cha fikra – kinazionesha
fikra zipi
• Lugha kama kichukuzi cha mila – inachukua
mila zipi
MIHADHARA
• Fasihi ni Nini?
• 1. HISI: Sio tu suala la hisia, bali ni uoneshaji
wa mahusiano baina ya watu; na watu na
dunia yao katika jamii kwa njia ya kisanaa.
• 2. KIOO CHA JAMII: Ni zaidi ya Kioo.
Haituoneshi tu, bali ni mjadala wa harakati za
mwanadamu katika kuyaingia maisha,
kuyatengeneza, kuyabadilisha, kuyaishi na
hatimaye kuachana na maisha.
Mihadhara…
• Fasihi ni Nini?
• 3. MAJADILIANO: Hujadili maisha kwa kipindi
fulani cha historia, historia yenyewe,
chimbuko la jambo na mustakabali wake.
• 4. ZAO LA HISTORIA, huiitika historia, na
huchongwa na historia.
• 5. NI SANAA ambayo hutengenezwa kutokana
na mchakato wa kihistoria na kiharakati katika
maisha ya jamii.
Chimbuko la Fasihi
• Hivi Fasihi ilitoka wapi? Na Je kila Jamii ina
Fasihi au Fasihi ni kwa wachache?
• Kuna Nadharia au Mitazamo 4
• 1. Chimbuko lake ni Mungu/Miungu (dhanifu)
– Imekuwapo duniani kama zawadi toka kwa mungu
kwa wateule wachache
– Mungu mwenyewe ni msanii Mkuu
– Nyimbo mf. Ooh Lulu
Chimbuko …/
• 2. Chimbuko lake ni nguvu ya miujiza au sihiri
– Kujaribu kukabiliana na kuyashinda mazingira.
– Kuchora, Kuchonga, Kujenga vijumba na kunuizia
– (SIKU HIZI) Kuombea vitambaa au Kifaa n.k
• 3. Chimbuko ni Mwigo
– Kuiga mazingira, sauti, mwonekano, wanyama, ndege,
nk
– Kubuni hali ya ufanano
– Ushairi ulichimbuka kutoka ktk kuiga
– Mwanadamu ni kiumbe wa uigaji, tokea mtoto
– Ni mwigo ukimaanisha uwakilishi wa jambo kwa
jingine. Ni taswira inayolenga kuonesha jambo
Chimbuko …/b
• 4. Chimbuko ni Mabadiliko ya Mwanadamu
(Yakinifu) katika kuyadhibiti mazingira
• Marx na Engels wanaingalia Fasihi kama zao la
mabadiliko katika maisha ya mwanadamu
ambayo hutawaliwa na
– Mfumo wa uzalishaji mali
– Uhusiano katika uzalishaji mali
– Mfumo na Uhusiano hutokeza MATABAKA
• Fasihi ni zao la Matabaka na Uhusiano katika
uzalishaji mali
• Katika uhusiano mwanadamu alihitaji lugha
Dhima ya fasihi
• Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea
mwulizaji anatoka katika tabaka lipi na kwake
fasihi ni nini.
• Kuburudisha
• Kuhimiza Kazi na Kujenga moyo wa kazi
• Kujenga tabia: Kuonya, Kuasa, Kufunza
• Kuelimisha
• Kuhifadhi kurithisha amali za Jamii (mila,
desturi, thamani n.k)
• Kukuza na Kuhifadhi lugha
Dhima…/
• Swali la Fasihi hufanya kazi gani, hutegemea
mwulizaji anatoka katika tabaka lipi na kwake
Fasihi ni nini.
• Kuendeleza harakati fulani katika Jamii
• Ujenzi wa Utaifa
• Kuleta Ukombozi: Hasa wa kifikra, kisiasa,
kiuchumi, kitabaka, kijinsia, n.k
• Fasihi ni zao la Kitabaka. Tabaka husaidiwa na
itikadi katika Kujiimarisha
• Itikadi: Mfumo wa mawazo, imani kuhusu
mahusiano na maongozi ya watu ktk Jamii
Dhima za Fashi ktk maisha
• UCHUMI
• ITIKADI
• SIASA
• UTAMADUNI
• FALSAFA
• UJUMI
Dhana ya fasihi ya Kiswahili
• Waswahili wenye hii Fasihi ni kina nani?
• Fasihi hutambulishwa kwa Lugha: Kiswahili
• Wenyeji wazungumzao Kiswahili katika Afrika
Mashariki na Kati na Visiwa vya Bahari ya Hindi
katika Mwambao wa Afrika mashariki
• Inayoeleza utamaduni na maisha ya Waswahili
• Rej. Mulokozi, 2017:Sura 3. Fasihi ya Waswahili,
Fasihi ya Kiswahili na Fasihi kwa Kiswahili (30-
33).
• Je Fasihi ya Kiswahili na Fasihi ya Kitaifa ni Dhana
ile ile? (Mutembei, 2004: Mulika No. 26).
Maendeleo ya Fasihi Katika Mifumo Mbalimbali
ya Maendeleo ya Binadamu
• Kwakuwa tumezungumza kuwa Fasihi ni chombo
cha mabadiliko ya Mwanadamu, tuyaangalie
mabadiliko hayo, tukijikita katika ufafanuzi wa Karl
Marx na Friedrisch Engels.
• Kuna Ujima
• Utumwa
• Umwinyi na Ukabaila
• Ubepari
• Ujamaa
• Uliberali
Sanaa, lugha na fasihi Wakati wa Ujima

• Kuwaunganisha watu
• Umoja na Ushirikiano vilisisitizwa
• Lugha ilikuwa si changamani
• Fasihi – hasa simulizi ikihusisha maudhui
yasiyo changamani.
– Wema dhidi ya Ubaya
– Wahusika wanaowakilisha watu halisi
– Wahusika na uhusika wao katika jamii: miti,
wanyama ndege nk
Kipindi cha Utumwa
• Mabwana dhidi ya watumwa
• Kupumbaza watumwa na wao kuonekana
kuwa hiyo ni majaaliwa yao
• Watumwa kudai ukombozi
• Udhibiti wa kazi za kifasihi
• Matokeo ya udhibiti:
– Lugha ya mafumbo
– Wahusika changamani
Kipindi cha Umwinyi na Ukabaila
• Mamwinyi dhidi ya watwana
• Kupumbaza watwana na wao kuonekana kuwa
hiyo ni majaaliwa yao
• Kustarehesha mamwinyi na makabaila
• Udhibiti wa kazi za kifasihi
• Harakati za ukombozi
– Wahusika changamani
Kipindi cha Ubepari
• Ubepari ni nini
• Matabaka
• Migogoro ya wafanyakazi dhidi ya Mabepari
• Migogoro viwandani na mashambani
• Migomo
• Ukombozi
• Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui
hayo
• Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo
• Ni nini wajibu wako kama mhakiki
Kipindi cha Ujamaa
• Ujamaa ni Nini
• Ujenzi wa Taifa Jipya
• Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa
• Ujenzi wa Sera Mpya
• Usawa na Ushirikiano
• Vita dhidi ya Makabaila na Mamwinyi
• Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui
hayo
• Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo
• Ni nini wajibu wako kama mhakiki
Kipindi cha Mfumo wa Uliberali
• Maana
• Ni mambo gani mapya yanayojitokeza katika
kipindi hiki
• Soko huria ni nini na maudhui yake ni yepi?
• Utandawazi au Utandawizi
• Unajitokezaje katika fasihi
• Uhuru wa uandishi na athari za uhuru huo
• Tafuteni kazi za Kiswahili zinazoeleza maudhui
hayo
• Ni nini wajibu wa mwandishi wa kazi kama hizo
• Ni nini wajibu wako kama mhakiki
Tanzu za Fasihi
• 3:1. Fasihi simulizi
• 3:2. Fasihi andishi
• 3:3. Kufanana na kutofautiana
kwa fasihi simulizi na andishi
• 3:4. Fani na Maudhui katika
fasihi simulizi na andishi
3.1 Fasihi Simulizi
• Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na kubuniwa
kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa
njia ya mdomo na vitendo bila kutumia
maandishi (Mulokozi, 2017:38).
• Ni tukio linalofungamana na muktadha Fulani
wa kijamii.
• Mulokozi anatofautisha kati ya fasihi ganizi na
fasihi simulizi.
• Hakikisha unajua tofauti za dhana hizo kwa
usahihi
Changamoto katika
Maana ya Fasihi Simulizi

• Jina: Simulizi (kusimulia: Oral)


– Ganizi (inayoganiwa- narrative)
• Ufafanuzi:
– Kutungwa kichwani
– Kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na matendo
– Hakuna maandishi
• Ufafanuzi huu katika ulimwengu wa sasa
• Usimulizi katika Radio na TV
3.2 Fasihi Andishi
• Ni Sanaa ya lugha inayotungwa na
kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya
maandishi (Mulokozi, 2017:40).
• Hutegemea vipengele vitatu: mtunzi, msomaji
na mdhamini.
• Suala la udhamini hutofautiana kutegemea
utanzu wa fasihi andishi unaohusika
• Katika maandishi kunajitokeza changamoto ya
udhibiti
– Ni muhimu jamii ijihakikishie kushikiliwa kwa
maadii ambayo yameijenga jamii hiyo.
3.3 Kufanana na Kutofautiana
• Je fasihi andishi hufananaje na fasihi simulizi?
– Matumizi ya mbinu za usimulizi katika uandishi
– Matumizi ya wahusika na lugha za usimulizi
• Ni wapi zinakutana na wapi zinaachana?
– Zote ni sanaa za lugha
– Zote hujadili migogoro, matatizo na changamoto
za mwanadamu katika kuyakabili mazingira yake
– Hujadili maana ya kuwako, na mahusiano baina ya
mwandamu
– Huonesha masuala yahusuyo hisi na Imani
– Uchangamani wake hutofautiana
3.3 Kufanana na Kutofautiana/…
• Mabadiliko makuu kutoka katika kusikia
– Macho na Masikio ni viungo vikuu
• Kuingia katika kuona
– Macho yakawa kiungo kikuu
• Mabadiliko kutoka “neno” sauti, kuwa “kitu”-
alama ya maandishi. Alfabeti ikasimama kuwa
kiwakilishi cha sauti
• Neno lilisikika tu, alama sasa inaonekana na
kuweza kushikika (karatasi/Kitabu)
Fasihi Simulizi
• Chimbuko la fasihi simulizi
• Tuliangalia chimbuko la Fasihi kwa
ujumla.
• Je unadhani ni nini chimbuko la fasihi
simulizi?
• Je fasihi hii ilianzaje?
• Je ilikuwapo lini?
4:2. Maudhui na dhima
ya fasihi simulizi
• Tofauti kati ya maudhui na dhima ni nini?
• Tuliangalia dhima ya Fasihi kwa ujumla.
• Je unadhani ni nini dhima ya fasihi simulizi?
• Ufafanuzi wako uendane na vipindi katika
mabadiliko ya maendeleo ya mwandamu
• Je dhima hubaki ile ile au hubadilika? Kwa
vipi? Kwanini?
4:3. Fani na muktadha wa utendaji katika
fasihi simulizi
• Ifafanue dhana ya utendaji katika fasihi simulizi.
• Uainishaji wa fasihi simulizi bado ni changamoto.
• Je, igawanywe kwa kufuata:
• Uainishaji wa Balisidya,
• Uainishaji wa Taasisi ya Elimu,
• Uainishaji wa awali wa Mulokozi, 1996.
• Uainishaji wa Kobia,
• Uainishaji mpya wa Mulokozi, 2017:51- 62)
4:4. Uchambuzi wa tanzu na changamoto
zake
• Kutokana na Uainishaji, ni dhahiri kuwa
uchambuzi wa tanzu za fasihi simulizi una
changamoto kadha.
• Ni muhimu kuzifahamu changamoto hizo.
• Ni muhimu zaidi kuwa na msimamo unaoweza
kuutetea ni kwanini unapendelea uchambuzi
mmoja wa tanzu dhidi ya mwingine.
Moduli ya 5: Fasihi Andishi

• 5:1. Fasili mbalimbali za fasihi andishi


• 5:2. Chimbuko na maendeleo ya fasihi andishi
ya Kiswahili
• 5:3. Tanzu na kumbo za fasihi andishi ya
Kiswahili
• 5:4. Fani na maudhui katika fasihi andishi
5.1. Fasili mbalimbali za fasihi andishi

• Litteratura: Kitu kilichonukuliwa kwa


maandishi.
• Kazi za kiubunifu zinazotumia lugha ili
kuwasilisha wazo Fulani.
• Kuwakilisha desturi, mila, utamaduni wa jamii
kwa njia ya kisanaa
5:2. Chimbuko na maendeleo ya fasihi
andishi ya Kiswahili
• Kutokea katika fasihi simulizi
• Kazi za mwanzo za ushairi katika hati za
kiarabu
• Riwaya ya Uhuru wa Watumwa
• Kazi za tafsiri
5:3. Tanzu na kumbo za fasihi andishi ya
Kiswahili
• 5.3.1 Tamthilia
• 5.3.2 Riwaya
• 5.3.3 Ushairi
5.3.2 Fasihi Andishi - Tamthilia
• Msingi wa sanaa yoyote ile ni uigaji.
• Msanii huangalia kitu halisi, kisha hukiiga na kukitoa
kwa njia fulani. Akifanya hivyo, usanii wake huwa ni
kiwakilishi tu.
• Maisha huwa ni mwigo: Mf. Ktk dini twaambiwa
maisha halisi yatakuwa mbinguni. Unavyoishi sasa
ndivyo utakavyokuwa huko juu (yaani hapa sisi sio
halisi). “Tunapita tu” mahali kwetu ni pengine n.k
• Matendo ya mila, utani nk, huwa ni uigazi
• Miviga na sherehe ni uigaji
Tamthilia msingi wake ni Uigaji
• Tamth.- andiko la kiuigizaji lenye kuonesha
matendo na maneno. Ni igizo la kifasihi
lililokusudiwa kutendwa (kuigizwa) jukwaani
kwa ajili ya hadhira fulani.
• Istilahi ya tamthilia inatokana na neno
mithali, (mithili) yaani mfano, au ishara
ambalo msingi wake ni uigaji. Si kitu halisi.
• Katika tamthilia, wahusika, matendo yao na
nafasi zao humathilisha watu, matendo au
nafasi halisi katika jamii. Wamathili
Tamthilia/Onesho/Mchezo
• Tamth.- andiko la kiuigizaji lenye
kuonesha matendo na maneno
• Mlama, 1983: Tamthilia ni sanaa ya
maonesho, ambayo huwasilisha ana
kwa ana tukio fulani kwa hadhira kwa
kutumia usanii wa utendaji (vitendo,
uchezaji, ngoma, uimbaji n.k)
• Sanaa za Maonesho ni Nini?
Maana ya Sanaa za Maonesho
• AINA 3 za SANAA
– Za Uonesho-:- Uzuri umo katika kuona=
uchoraji, uchongaji, nk.
– Za Ghibu-: uzuri wake umo katika kusikia.
ushairi, upigaji muziki,
– Za vitendo:-Uzuri wake umo katika kuona na
kusikia vitendo.
– Aina zinajadiliwa kupitia katika UZURI. Je
kazi/dhima?
S.M ni Sanaa za Vitendo
• Kitendo cha sifa 4
–Mchezo
–Mchezaji
–Uwanja wa kuchezea
–Watazamaji
Udhaifu wa mtazamo huo
• Mchezo
• Sifa 4 tu
• Tamth. Ni ya Kigeni. Je S.M
za asili?
Maana kwa kuzingatia Uafrika: Ni tukio
la kijamii lenye sifa:
• Dhana Inayotendeka
• Uwanja wa Kutendea
• Watendaji
• Hadhira
• Kusudio la Kisanaa
• Muktadha wa Kisanaa
• Ubunifu (umathilishaji)
Sanaa zaMaonesho za Kiafrika
• Sherehe
– Unyago/Jando, Kutoa jina, kuota
meno (hatua kwenda nyingine)
• Ngoma:
(chombo,kitendo,sherehe)
• Kusalia mizimu
• Kupatikana mapacha n.k
Sana za Maonesho za Magharibi
• Mahali pa kuonea. Kinachotendwa
• Drama
– Mpangilio wa maneno huambatana na
utendaji wa wahusika
– Kuna uigizaji (wa tabia/matendo)
– Huegemea katika maandishi
– Mpangilio wa jukwa, taa, rangi,sauti. n.k
Historia ya Tamth. Afrika Mashariki
• Waingereza Kenya (Iliandaliwa kuwa
mahali pa kuzamia na kukaa )
• Ujio na Makazi ya Walowezi
–Kuchukuliwa kwa mashamba na
Ardhi. (Taz. Mulokozi, 2017:22-23)
–Kuanza kurejeshwa kwa maaskari
–Mpango wa kuwapumbaza
–Ujio wa mtaalamu: Mwalimu
Kenya: Usuli wa kazi za Hyslop
• 1944 Mfanyakazi Jeshini
– Akaanzisha kitengo cha elimu jeshini
kuwatumbuiza askari 30,000 Mash. Ya
kati (Waganda, Kenya na Wa Tz)
– Muziki na Tamthilia, na Filamu
• Mf. 1945: Filamu ya Akili Mali

1945:- Vita iliisha akarudi Uk


Hyslop…
1953: Alirudi Kenya kama Mwl. wa
Shule akikazia Tamth.
Tamth Zake zikafanyiwa majaribio na
kisha kuchapishwa tokea 1957.
Wanafunzi wake walifanya majaribio
kama hayo na kazi zao zikachapwa
baadaye.
Nchini Tanzania
• Hali ya Sanaa hii Tanzania
–Uigaji wa zile za Uingereza
–Vichekesho
–Udhati
–Azimio
–Baada ya Miaka ya 1970
Tanzania hadi miaka ya 1960
• Tangu 1922 zilikuwa zikiigizwa
mashuleni
• Mashindano ya Maigizo tangu 1960
• 1967: Youth Drama association
• 1968: Wakati Ukuta (E. Hussein)
• 1970: Alikiona (E. Hussein)
Urithi wa Waingereza, Tz.
Kwa Tanzania:- Kazi za Shakepeare
Julius Ceasar, Macbeth, Merchants of
Venice
Maana yake haikueleweka kwa Wa Tz.
Walioziigiza hawakuzielewa. Walizikariri
tu. Waliona fahari kuzungumza na kuvaa
kama Wahusika wa Kiingereza.
Kazi za Hyslop na Athari kwa Wanafunzi
Mgeni Karibu (G.Hyslop, 1957)

Afadhali Mchawi (G.Hyslop, 1957)

Baadaye waandishi wengine


wakaibuka na kuendelea kuandika:
Nakupenda, Lakini… (H. Kuria, 1961)
Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (G.
Ngugi, 1972)
Mtawa Mweusi (Ngugi wa Thiong’o)
Maudhui ktk Tamthilia za Mwanzo
• Vichekesho zaidi (Taz. Fasihi III, 1983)
• Masuala ya rushwa katika jamii, urithi,
• Magendo ya dawa Vs. Uaminifu (fitina)
• Kumchagulia mtu mchumba
• Umaskini ktk ndoa Vs. Mapenzi ya kweli
– Umri ktk Ndoa. (Mzee ana pesa, Kijana ana
mapenzi)
– Mapenzi ktk Ndoa: Wanandoa hutafuta nini?
Kabla ya Azimio (Hazikuchapishwa)
• Vichekesho (Taz. Kiango ktk Kisw)
– Kuwacheka washamba
– Kuwacheka wazungu weusi
• Kufuata kampeni mbalimbali (ujinga,
maradhi, uvivu, n.k)
Baada ya Azimio hadi miaka ya 1970
• Wakati Ukuta (E. Hussein,1968)
• Kinjektile (E. Hussein, 1969)
• Tiba (Nkwera, 1969)
• Mashetani (Hussein 1971)
• Aliyeonja Pepo (F. Topan, 1970)
• Hatia (P. Muhando, 1972)
• Tambueni Haki Zetu (P. Muhando, 1973)
• Heshima Yangu (Muhando, 1974)
Athari za Azimio la Arusha
• Umuhimu wa Azimio
• Kulikuwa na hali gani
• Watu walilitafsirije?
• Azimio lilisema nini
• Wanafasihi walilitafsirije?
Dhamira kutokana na Azimio la Ar
Tafuta Tamthilia za wakati huo
Kuondoa unyonyaji
Kuwabeza wasaliti
Kujenga Umoja
Kuhimiza ufanyaji kazi
Kila mara kumbuka yale yaliyotokea
katika jamii. Fasihi ni zao la jamii katika
kipindi maalumu cha historia
Miaka ya Ukombozi 1970 - 1980
Ukombozi kutokana na nini
Sura mbalimbali za ukombozi
Ujinga (elimu), Usawa, Mila, Uhuru n.k
Tafuta tamthilia za kipindi hiki:-
Mashetani, Damu Imemwagika, Tone la
Mwisho, Dhamana mabatini, Mkwava wa
Uhehe n.k
Tamthilia za Ebrahim Hussein
• Alikiona (1969)
• Kinjeketile (1969)
• Wakati Ukuta (1970)
• Mashetani (1971),
• Jogoo Kijijini na Ngao ya jadi (1976)
• Arusi (1980)
• Jambo la Maana (1982)
• Kwenye Ukingo wa Thim (1988)
Baadhi ya Tamthilia za Muhando
Hatia 1972
Tambueni haki zetu, 1973
Heshima yangu, 1974
Pambo 1975
Harakati za ukombozi 1982
Nguzo mama 1982
Abjadi yetu, 1983
Lina ubani 1984
Baada ya 1980
• Je baada ya 1980 kuna mwelekeo
maalumu unaoweza kuelezwa kuhusu
tamthilia (fasihi) ya Kiswahili kama
ilivyokuwa kwa miaka ya Uhuru, Azimio,
Ukombozi?
Ni maudhui ya aina moja? Kwanini?
• Giza Limeingia, 1980
• Ayubu, 1984
• Ngoma ya Ng’wanamalundi (1999)
Baada ya Miaka ya 1980…
• Kaptula la Marx, 1999
• Ngome ya Mianzi, 2000
• Amezidi (1995)
• Nje Ndani (2017)
• Tafuta tamthilia nyingine na uangalie
zinaeleza nini. Je unaweza kuziweka
katika mkabala upi? Tetea uamuzi wako
kwa hoja za kitaaluma
Tamthilia za Kiswahili Kenya
Tazama kazi za hawa wafuatao:
• Ngugi wa Thiong’o
• Jay Kitsao
• Nyaigoti Chacha
• Kithaka wa Mberia n.k
• Tafuta tamthilia nyingine na uangalie zinaeleza
nini. Je unaweza kuziweka katika mkabala upi?
Tetea uamuzi wako kwa hoja za kitaaluma
• Athari za utandawazi ktk tamthilia za Kiswahili
kwa TZ na Ky ni zipi?
5:4. Fani na maudhui katika fasihi andishi

• MAUDHUI: Tumezungumzia
• Dhamira mbalimbali.
• Ujumbe
• Migogoro
• Msimamo (anasimamia upande upi)
• Mtazamo (zuri/baya), dhanifu/yakinifu/dini
• Falsafa (Nini, kwanini na Kwa vipi)
Fani katika Fasihi Andishi
• Muundo (mpangilio/mfuatano)
• Mtindo (tofauti za uandishi)
• Wahusika
• Mandhari
• Lugha (Tamathali, Methali, Taswira nk)
• Jina la Kitabu (Anwani)
Ujielezaji kwa namna mbalimbali

MAENDELEO YA KENYA 1900


MAENDELEO YA KENYA 2014

You might also like